Bangkok Thailand, July 2011

Montien Hotel

 

Tulifikia Montien River Side hotel ambayo ipo karibu na Chao Phrya river. Next day tulibook dinner Cruise ya hotelĀ  kwa bahati mbaya haikuwa na watu wengi siku hiyo so ilikua iko cancel ikabidi tujaribu kubook another dinner cruise kutokana kuwa late dinner cruise nyingi zilikua ziko full booked. Tukapata kwenye White Orchid River Cruise ambayo ikatokea kuwa quite interesting

Hotel inatoa service ya bus ambalo linapeleka wageni sehemu mbali mbali including kwenye malls mbali mbali kwa ajili ya shopping, mi safari hii nikaamua kwenda Capital Mall watu wengi wanaoenda hapo ni local wageni ni wachache sana. Ilikua ni good choice kwani nilikuta kulikua na vitu vingi ambavyo ni tofauti na kwenye malls nyingine pia bei zake hazikuwa mbaya sana. Nilipapenda nafikiri next time nikirudi lazima nipite hapa pia.

Jioni tulijiandaa kwa ajili ya kwenda dinner cruise ambap walikuja kutuchukua maana usafiri wa kwenda na kurudi ulikua included. Kila kitu kilienda sawa huduma yao ilikua poa mpaka pale tulipojikuta tumeshakalishwa ndani ya boat tayari kwa safari. Kwanza meza yetu ulikua karibu sana na spika ambapo muda wote wa dinner sauti ya music ilikua kubwa sana na nyimbo zenyewe walizokua wanapiga haziendani kabisa na wakati wa dinner, tukaona kweli safari hii tumepatikana. Chakula chenyewe hakikuwa kizuri na kutokana na boat yenyewe kuwa kubwa watu walikua wengi ni tofauti sana na dinner cruise ambazo tumezoea kwenda nyingi zinakuwa zinatoa huduma za ki Thai zaidi kuanzia chukula, music mpaka dancing show. Hii ilikua zaidi kwenye mchanganyiko tu na mchanganyiko wenyewe haukupendeza kabisa. Kitu nachoweza kusifia kuwa ni boat nzuri na ukiwa nje ya boat unapata view ya kukata na shoka kwa hilo tulifurahia sana maana tulispend muda wetu mwingi nje kukimbia kelele ya spika hahahaaaa…Kwa ujumla hatukufurahia kabisa, afadhali yangu mimi ila hubby alikuwa so sad. Siku iliyofuata tulikua tunaelekea zetu Krabi, what a night!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *