Category Archives: Switzerland

Geneva, Swiss 2008

Geneva

 

Ilikua raha sana¬† eti tunaenda Geneva for lunch hahaaa…hivyo ndio ilivyokua na kujikuta nimeingia na mimi Geneva. Nimekua na hamu ya kuja mji huu tangu nilipokua nafanyia kazi kwenye mashirika ya wakimbizi. Tulifika hapa tukitokea Paris by train tulikua na a day ya kuvinjari na kutizama mji chap chap kabla ya kuanza safari usiku ya kuelekea London. Nia yetu hasa ilikua ni kuutizama mji na tukiupenda basi turudi tena siku nyingine kwa hakika tuliupenda na lazima turudi tena.

Tulitumia muda wetu ipasavyo tulifanikiwa kwenda sightseeing, shopping and kula lunch na my new friend Jeruto. Tulifurahi sana kuona na Jeruto ambae yeye anaishi hapa Geneva ilikua nice of her kuja kutusalimia and have lunch with us, thanks Jeruto big hug from us.

Kwa ujumla nimeipenda Geneva, mji ni msafi sana kila unapopita kuko poa, ilinikumbusha Sydney Australia maana nako kusafi kweli.  Nilifanikiwa kufanya kiji shopping kidogo ambapo nilifurahi kuna maduka mengi na vitu vizuri sana. Siku yetu iliisha ikiwa na mafanikio makubwa, muda wetu wa kuondoka uliwadia. Cheers Geneva until next time!