Iceland, 2008

Geysir

 

umekuja hapa special kwa ajili ya kutizama Aurora(Northern lights) and  Geysir, Tulitokea Heathrow Airport to Reykavik. Moja kwa moja tulichukua gari ambayo tulikodi na kuanza safari yetu ya kuelekea Geysir ambapo ndio tumekodi Cottage for 4 nights. Ilikua mara yangu ya kwanza kuwa kwenye snow nilipenda sana, ila baridi yake sasa ilikua kiboko nadhani ningekua naishi hapa ningesema vingine.  Pia nilifurahishwa na milima ambayo imefunikwa na barafu along the way inapendeza sana kuona weupe kila mahala. Tulivyofika kwenye cottage tulifurahishwa na chaguo letu, ndani kulikua very warm na kumetulia sana. Kulikua pia na holiday houses nyingine pembeni yetu.

Hizi cottage ni holiday houses ndani kuna kila kitu muhimu ambacho kinahitajika. The cottage was heated with Volcanic hot spring water ilikua safi sana. Pia nje kulikua na jacuzzi ambalo nalo lilikua na Hot Spring Water, inapendeza sana ukiwa ndani ya maji jinsi yalivyo na joto zuri huku snow ikiwa inakudondokea.

Tuliupenda huu mji wa Geysir, ulikua uko kimya sana. Tulikua kama wenyeji wa hapa just drive around na kuenjoy natural wonders. Pia kufanya shopping ndogo kwenye mini supermarket iliyopo karibu na cottage then kurudi home, kuko very peaceful.

Pia tulitembelea sehemu mbali mbali around Geysir. Kipindi hiki kilikua cha winter kwa hiyo snow ilikua kila sehemu mpaka kwenye river. Ila wanasema kuwa kipindi cha summer huwa pia kunapendeza sana, ningepende kurudi tena kipindi cha summer nadhani kuna uzuri wa aina yake hapa.

Baada ya siku zetu kuisha hapa tulielekea mji mkuu wa Iceland Reykavik. Tunasikitika hatukuweza kuona Aurora kipindi hiki nadhani itakua next time tena. Tulikaa mjini Reykavik kwa siku moja na kesho yake tulipanda ndege na kuelekea London.

Kwa ujumla nimepapenda sana Geysir, kuko very peaceful. Iceland kwa ujumla ni pazuri sana na hakika lazima turudi tena nchi hii. Cheers Iceland until next time!

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *