London, UK. Feb, 2008

Around London Tower

 

Imenichukua miaka mingi atimaye kufika hapa. London ilikua ni chaguo langu la kwanza katika miji ya Europe. Swali ni kwamba je, nimekuta kama nilivyokua nafikiria? Nadhani naweza sema hapana labda kwa sababu nimefika hapa baada ya kufika miji mingine ya Europe or kwa sababu nilikuja kipindi kibaya cha winter na labda sababu nilikua na watoto wadogo chini ya miaka 2. Nilikua hapa karibu 2 weeks niliweza tembelea sehemu ikiwemo Buckingham Palace, London Eye, Thames River Boat, London Tower, Harrods kwa some shopping pia kufanya City Tower kwenye London’s famous Red Bus.

Kitu ambacho nilipenda sana ni kuona majengo ya zamani ambapo London wamefanikiwa kuyaacha na kufanya mji uwe na sura yake ya kipekee, safi sana.

Kitu kingine ambacho niligundua hapa ni kwamba mji uko busy sana. Kwa upande wangu napenda kuishi sehemu zilizotulia sana, kwenye miji mikubwa napenda kwenda kutembea kwa muda fulani tu, lakini si kuishi.

Kwa ujumla kipindi hiki sikuenjoy London kabisa kwanza hali ya hewa ilikua ni mambo ya mvua mtindo mmoja. Pili, nadhani London si kwa ajili ya watoto wadogo maana nakumbuka kuna train station nyingine hazina escalator na unatakiwa kutumia ngazi za kawaida, shughuli ilikuwepo kwenye baby pram. Sijui wanaoishi hapa wanafanyaje wakiwa na watoto wadogo kwenye hizo train station, pia kuna mengi tu kama baby changing rooms na kadhalika. Nikilinganisha na nchi nyingine kama Australia wanajali sana vitu kama hivi. Lazima nitarudi tena kutembea kama unavyojua ni London bwana hahaaaa…Cheers London until next time!

 

2 thoughts on “London, UK. Feb, 2008”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *