London, Southampton & Salisbury UK, 2008

London Bridge

 

Yap! Nimerudi tena London ila safari hii nimekuja bila watoto na experience yangu ilikua tofauti. Tulifikia Hilton Tower Bridge Hotel mambo yalikua yako poa. Nilisema kuwa nitarudi tena maana hii ni London bwana hahaa…naona sikuchukua hata muda mrefu kurudi maana nilikuwepo hapa February na sasa niko hapa September the same year. Tulikaa hapa kwa siku tatu na kuchukua train kuelekea Southampton. Safari hii tulikuja London kwa ajili ya harusi ya mtoto wa kaka yake mume wangu ambayo ilikua inafanyikia Southampton. Along the way to Southampton nilifurahishwa na country side ya nchi hii ni kuzuri na kupendeza sana.

Baada ya kufungwa ndoa wote tulielekea kwenye reception ambayo ilikua inafanyikia kwenye country house iliyopo nje kidogo ya mji, ambapo nasi tulilala hapa.

Harusi ilifanyikia kwenye nice old small church in Southampton. Siku ya kwanza tulilala mjini hapa kwenye B & B na siku iliyofuata ambayo ni siku ya harusi tulihamia kwenye Country House ambapo reception ndio ilikua inafanyikia huko.

Reception ilikua nzuri sote tulifurahi sana. Siku iliyofuata tuliamua kuelekea Salisbury kwenda kuangalia Stonehenge. Nimefurahishwa na Southampton nadhani kama ningekuwa naishi UK  ningechagua kuishi huku pako poa.

Nilifurahi sana nami kufika hapa Stonehenge ambayo ni one of the most famous sites in the world. Inasemekana kuwa ilikuwepo hapo tangu 2,500 BC wanasema hata kabla ya hapo. Ni kweli wanavyosema inashangaza haya mawe yalifikishwaje hapa maana eneo zima la karibu hakuna mawe  kama haya. Hicho ndicho kinanifanya kupenda historia za zamani maana zinakufanya ufikirie kwa undani sana.

Baada ya kushangaa shangaa tulichukua train na kurudi zetu London ambapo tulilala usiku mmoja na siku inayofuata tulikua tunaelekea zetu France.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *