Mexico City, Mexico 2004

The view from the Pyramid of the Sun

 

Holiday hii ilikua part ya our 2months honeymoon. Tulifika hapa tukitokea Las Vegas ambapo ndio tulipanda ndege yetu ya kuja hapa. Tulikuja mji huu kwa ajili ya kwenda kutembelea Teotihuacan Pyramids. Tulikua na siku 2 tu hapa Mexico City ambapo siku ya kwanza tuliitumia kuuzunguka mji na siku ya pili tuliimalizia kwenye pyramids.

Siku ya pili ilivyofika tulianzia moja kwa moja kuelekea kwenye pyramids ambapo kuna umbali kama kilometres 40. Tunaambiwa Teotihuacan Pyramids zimekuwepo about 2,000yrs ago. Pia inasemekana kuwa huu mji ulikua ni kati ya miji mikubwa duniani enzi hizo, ilikua na watu kama 200,000.

Tulivyofika tulishangaa kuona the beauty of this place yaani ilikua inapendeza sana. Ukikaa na kufikiria watu miaka hiyo waliwezaje jenga sehemu nzuri na kubwa kama hii bila kuwa na urahisi wa vitendea kazi. It’s real amazing.

Tulivyokua kwenye pyramids wacha kazi itupate ya kupanda hizo ngazi ilikua shughuli kweli, watu wengine walikua wanapanda kwa matako ilikua inachekesha kweli. Ngazi zilikua nyingi sana na zilikua zinaenda juu kwa kasi ilibidi wakati mwingine ushikirie kamba ambayo imewekwa kwa ajili hiyo la sivyo unaweza kupata kizungu zungu na kudondoka. Uzuri unakuja pale ukishafika juu, view unayokumbana nayo ni ya hatari, panafurahisha kwa kweli. Unaanza kujiuliza ni jinsi gani hawa watu waliweza kupima na kuweka kitu cha namna hii, it’s amazing.

Baada ya kuzunguka na kutosheka tulienda kula lunch kwenye hotel ya karibu kwa bahati nzuri siku hiyo na Traditional Mexican dancing ilikua poa sana kuona hiyo show wanasema dancing ya namna hii imeanzwa kuchezwa tangu enzi hizo za Pyramids.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *