Niagara Falls Buffalo, USA-Our around the world trip Nov-Dec 2013

Niagara Falls
Niagara Falls

What an experience we had here lol! Kwa sasa nacheka ila kusema ukweli mbona cha moto tulikiona. Tulikua na bahati mbaya sana kwa safari yetu ya Niagara Falls, kwanza flights zetu zilikua zinabadilishwa kila mara wakati tukiwa tunatokea Orlando kuja hapa ndege yetu ilichelewa kidogo so tulichelewa kufika Atlanta Airport ambapo tulikua tunatakiwa kuunganisha ndege ambayo ingetuleta hapa Buffalo. So tulipangiwa kuchukua ndege ya jioni na hapo sasa ndio tatizo lilipoanza kutokea.

Niagara Falls by night
Niagara Falls by night, snow ikimwagika

 

Niagara Falls by Night
Niagara Falls by Night

Kutokana na ratiba yetu ya mwanzo tulitakiwa kuwa hapa Buffalo si zaidi ya masaa 24 so tungewasili mchana ambapo tungepata nafasi ya kutembelea water falls na kesho yake asubuhi pia kabla ya kuanza safari ya kuelekea Airport. Hoteli tuliyofikia ni Holiday Inn ambayo iko karibu sana na waterfalls ni mwendo mdogo tu kufika hapo so plan yetu ya mwanzo ilikua iko poa sana. Ila sasa baada ya kuchelewa ndege yetu na kufika hapa usiku wa saa mbili hatukuwa na jinsi ilibidi tu twende kutizama usiku huo huku pia tukiwa na mpango kesho yake asubuhi kama kawaida pia tutaenda tena.

Niagara falls by night
Niagara falls by night

Sasa tukapata tatizo lingine yaani toka winter ianze hapa kulikua hakuna snow ilikua haijaanza rasmi siku ambayo tumeingia wakati tunatokea Airport kulikua kuko shwari ingawa kulikua na baridi na upepo. Baada ya kuweka mabegi yetu tulianza safari ya kuelekea kwenye waterfalls ile kutoka nje tu snow ikaanza kumwagika kama manyunyu ya mvua haikuwa mbaya sana tuliweza tembea mpaka sehemu yenyewe na kupata nafasi ya kupiga picha ingawa kulikua na baridi lakini si lile la sana sana. Ila kutokana na kutokua na nguo ambazo ni za baridi kwa sisi tuliumia na hili baridi, maskini Malaika alilichukia kweli eneo.

View from our hotel at Niagara Falls
View from our hotel at Niagara Falls

 

Amani trying to keep warm at Niagara Falls
Amani trying to keep warm at Niagara Falls

 

Niagara Falls
Niagara Falls

Snow iliendelea usiku kucha mpaka asubuhi na eneo lote lilikua jeupe limefunikwa na snow na hii ikawa bahati yetu mbaya nyingine maana tulitakiwa asubuhi hii kwenda tena kutembelea haya maporomoko ya maji na hii baridi ukiunganisha hatuna kabisa nguo za baridi au viatu vya snow na tulitakiwa kutembea kwa mita kadhaa ili kulifikia eneo hili basi we ilikua si fun kabisa na nilimuonea sana huruma Malaika maana ya jana usiku alilalamika sana wakati ndio kwanza snow ilikua inaanza kudondoka na barabara zote zilikua ziko okey bila snow sasa leo hii asubuhi na hii snow imefunika kila kitu sijui hali itakuaje. But after breakfast tukaanza safari ya kuelekea kwenye waterfalls wewe acha tu snow huku inamwagika upepo ndio usiseme miguu inafunikwa na baridi, huku viatu vyetu vinateleza maana si vya snow but at the end tulifanikiwa kufika eneo lenyewe ila kwa shida kweli.

Niagara Falls
Niagara Falls

 

mama Amika
mama Amika

 

Baridi kweli kweli
Baridi kweli kweli

Baada ya picha tulianza safari ya kurudi kwa kasi ila ilitushinda ilibidi tuishie kwenye one of the public washroom maana kulikua na heater tupate joto kidogo na kupasha miguu na mikono kabla ya kuanza safari ya kutembea kuelekea hotelini. Niagara Falls ni pazuri sana ila nadhani panapendeza zaidi kipindi cha summer ambapo hakuna baridi, tunampango wa kurudi siku ingine kipindi cha summer. Ila kwa yote tulifurahia maana ni moja ya adventure nyingine tumeweka kwenye maisha yetu ingawa ilikua ya kipekee ambapo pia imeleta umuhimu zaidi wa kuikumbuka sehemu hii :)

4 thoughts on “Niagara Falls Buffalo, USA-Our around the world trip Nov-Dec 2013”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *