Our around the world trip Nov-Dec, 2013-Venice, Italy-Day 2

 

Mitaani Venice
Tukiwa njiani kuelekea St. Mark’s square hii ni mitaa ya Venice

 

Siku yetu ya pili tulianza kwa kutembelea St. Mark’s square hili liko mashuhuri sana kwa watalii pia watengenezaji sinema maana limekua likionyeshwa sana. Kwa mtalii yoyote uwezi kufika Venice bila kuja kushangaa hapa nami nikiwa mmoja wapo lol! Hii ikiwa ni mara yangu ya pili mara ya kwanza ilikua 2002 unaweza cheki post yangu ya nyuma VENICE, ITALY 2002.

 

Amani in Venice
Amani in Venice

 

Hali ya hewa haikua nzuri sana siku hii, kulikua na mawingu pamoja na baridiĀ  ukilinganisha na jana yake ambapo kulikua na jua zuri leo hakuna jua kabisa.

 

St. Marco Square
St. Mark’s Square

 

St. Mark’s Square kipindi cha winter eneo hili huwa linakua na maji ndio huwa wanaweka hizo meza kama vile daraja ili watalii waweze kupita na kupata nafasi ya kushangaa eneo hili. Kipindi cha summer hapa huwa panapendeza sana.

 

At St. Mark's Square
At St. Mark’s Square

 

With my kids at St. Marco Square
With my kids at St. Marco Square

 

With hubby and Malaika
With hubby and Malaika

 

With my baby girl
With my baby girl

 

Hubby and kids
Hubby and kids

 

Baada ya kushangaa St. Mark’s Square moja kwa moja tukaanza safari ya kutafuta msosi ambapo chaguo la watoto lilikua ni pizza si pengine zaidi ya sehemu tuliyokula jana yake lol! Kusema kweli pizza ya hapo ni balaa, tamuje sasa

 

Tukisubiri daddy alete pizza
Tukisubiri daddy alete pizza

 

Tukisubiri lunch
Tukisubiri lunch

 

Ta taaa..pizza imefika, the best pizza ever, tulikulaje sasa
Ta taaa..pizza imefika, the best pizza ever, tulikulaje sasa

 

Baada ya lunch moja kwa moja tulielekea hotelini na kucheck out ili kuanza safari ya kuelekea port ambapo tunaanza safari yetu ya meli ya siku 19 kuelekea Miami, Florida.

2 thoughts on “Our around the world trip Nov-Dec, 2013-Venice, Italy-Day 2”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *