Family Holiday Krabi, Thailand. 2009

My baby Malaika at Railay beach

 

We love Railay Krabi, tunazidi kurudi hapa karibu kila mwaka, mambo yanabadilika kwa kasi sana. Maendeleo yanaongezeka mara ya kwanza tulipokuja 2003 kulikua na hoteli chache sana, sasa hivi zimeongezeka maradufu na kufanya kuwepo na choice nyingi ya wapi upate lunch au dinner.

Kitu ambacho bado hakijabadilika ni ukarimu wa watu  nadhani ndio sababu kubwa ambayo inatufanya tuendelee kurudi. Ni sehemu ya kila mtu uwe single, couple au ukiwa na watoto kila mtu atafurahia holiday yake.Sisi bado tunafikia the same hotel kila mara tukiwa Railay Krabi Sunrise Hotel kwa kweli hatuna cha kucomplain kabisa kuhusu hotel hii. Huduma zao ni nzuri sana na wafanyakazi wake ni wakarimu kweli pia bei yao ni ya kuridhisha.

 

 

The Family Krabi, Thailand. 2007

Amani with his brother & sisters

 

This year sikuweza kwenda holiday nilikua niko hoi na ujauzito wa Malaika. Amani and daddy walienda peke yao bila mimi. Huko Thailand walijumuika na our family iliyokua imetokea Australia. My Amani alikua ana mwaka na miezi mitano tu, ila kwa sababu ameshazoea kusafiri hakusumbua kabisa.

Krabi Thailand, 2003

Panapendeza kwa kweli 2003

 

 

Mara yetu ya kwanza kwenda Krabi ilikua ni 2003, moja kwa moja tuka fall in love with this place. Tulifikia Sunrise Resort Hotel kwa kweli hatuna cha kulalamika kabisa huduma zilikua nzuri sana na wafanyakazi wake ni wanaupendo kweli. Hatukukaa sana kama nakumbuka vizuri tulikaa kama siku nne hivi na tuliahidi kuwa tutarudi na tumefanya hivyo karibu kila mwaka.

Hizi ni baadhi za picha tulizopiga mwaka huo 2003 nadhani utaendelea kuziona picha za Krabi mara mara kwenye MaiSafari. Picha hazionekani vizuri sana nimefanya kuscan.

Los Angeles, USA. July 2004

Universal Studio Hollywood

 

This was part of my honeymoon. Ni safari yangu ya kwanza kwenda US. Tulisafiri kutokea Sydney mnamo tarehe 4th July 2004 kuelekea Los Angeles. Tulikatiza kwenye ‘International Date Line’ was kind of adventure na nilipenda sana. Ndege yetu ilituchukua 14hours but we arrived in US the same day 4th July. Tuliwasili Los Angeles airport and palikua pako kimya kidogo kutokana na kuwa ni Public holiday 4th July. We stayed at Radisson Hotel Los Angeles and baada ya kupumzika tuliweza tembelea mitaa ya karibu. The next day we tulitembelea mitaa ya Hollywood na kufanya shopping kidogo. Siku inayofuata tulienda Universal Studio for tour,kwa wale wapenda movie kama mimi hii ni sehemu yake, was wonderful.

The next day tulihamia Holiday Inn Disneyland ili tuwe karibu na park ambapo tulikaa hapa for 3days na kupata nafasi nzuri sana ya kutembelea park. The park ilikua busy sana thanks for our  fast line ticket, tuliweza tembelea ride nyingi bila kushinda kwenye foleni. My favourite ride was Hollywood Tower Hotel was scary but good scary. Kitu kingine ambacho kilinipendeza sana hapa ilikua ni maswala ya misosi yaani kila sehemu ilikua na chakula kitamu sana my favourite was Classic Nachos ambayo nilikula Rainforest Cafe, my goodness was delicious pamoja na kwamba nimeshawahi kula classic Nacho before but this one was yummy!  Kwa ujumla nime enjoy sana muda wote niliokuwa Los Angeles lazima nirudi tena sikumoja. Honeymoon ilianza vizuri sana me nilikua happy kupindukia. Cheers!!!!:)))

Amsterdam, Holland. June, 2011

Ibis Airport Hotel Amsterdam

 

Too bad we didn’t have much time to spend in Amsterdam, we had only one day. Lakini tuliweza tumia muda wetu vizuri.  We stayed at Ibis Hotel Airport. Tulipata muda wa kuzunguka kwenye neighbourhood.  Angalua kupata picha kidogo ya maisha ya wadutch. Panapendeza ila tungependa kuona nchi zaidi, tutapenda kurudi tena safari hii kukaa zaidi ili tuweze tembelea sehemu mbali mbali. The hotel na service zake zilikua nzuri sana tulifurahi kwa kweli. Amani aliweza kufanya shopping aliyokua anasubiria kwa hamu sana, kununua KLM plane toy ili aweze kuwaonyesha rafiki zake back home, he was so happy to get it.

Family Holiday Spain. June, 2011

Madrid

 

 

Safiri na Zawadi