Paris, France 2008

On top of the Eiffel Tower

 

This is not my first time in Paris lakini mara ya kwanza nilielekea moja kwa moja hospital. Kwa bahati mbaya muda ambao natakiwa kuelekea train station London nilidondoka kwenye ngazi ya sehemu tuliokua tumefikia niliangukia mkono vibaya. Kasheshe ya maumivu nilianza kuisikia nikiwa ndani ya train na ilizidi kupita kiasi ndipo nilipofika tu Paris ilibidi moja kwa moja nielekee hospital, kwa ujumla ni story ndefu sana ngoja niachie hapa.  This time nilikua mzima wa afya tele na kupata muda mzuri wa kuitembelea Paris na kuifurahia vizuri. Tulikaa hapa kwa siku 3 ambapo tulipata nafasi ya kutembelea sehemu mbali mbali including The Eiffel Tower and of course shopping, kama unavyojua shopping in Paris ni lazima.

Tuliamua kutembelea The Eiffel Tower muda wa usiku maana huwa kunapendeza sana, baada ya kupanda mpaka juu tulifurahishwa sana na view ambayo tulikumbana nayo huko juu. Kama kawaida watu walikua wengi sana baada ya kumaliza kushangaa shangaa tulielekea kwenye dinner, my favourite food in Paris is dessert yaani acha tu ukilinganisha na unene niliokua nao ilikua hatari tu.

Pia tulipata nafasi ya kutembelea Ossuary, ambapo kuna mifupa mingi ya binadamu imehifadhiwa. Wanasema kuwa kuna karibu ya mifupa ya watu millioni sita hivi ambapo imehifadhiwa hapa.

Kipindi chote tulichokua hapa tulikua na kaka wa mume wangu na familia yake. Siku zetu zilivyoisha ulikuwa muda wa kuondoka wakati sisi tunaelekea Geneva wao walikua wanaelekea London then back to Australia. Kwa ujumla Paris ni pazuri nitapenda kurudi tena but only for holiday hahahaaaa…Cheers Paris until next time!

2 thoughts on “Paris, France 2008”

  1. You deserve the most of it and I do real pray for you that this happiness will last till the end of time.
    Remember better is not good enough the best is yet to come

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *