Hot Spring Beach Resort Phang Nga, Thailand. July 2011

Beach Pier at the hotel

 

Tulifika hapa kwa njia ya barabara tukiwa tumetokea Khao Sok. Safari yetu ilituchukua karibu 2.30hrs mpaka kufika Hot Spring Beach Resort tulikaa hapa kwa 2nights. Tulikuja kipindi cha low season kwa hiyo kulikua kimya kidogo, hotel ni kubwa na nzuri sana. Room yetu ilikua kuwa kubwa ambapo ni chini na juu na ilikua na view nzuri sana, rooms zote za hii hotel zina view ya ocean. Tulifurahishwa karibu na kila kitu kuanzia chakula ambacho kilikua kitamu sana, huduma yao ambayo ni ya kukata na shoka, two swimming pool one ya natural water ambayo ni hot spring water pamoja na pool ya kawaida. Hot spring pool ilikua ya aina yake ambayo ndio haswa iliyotuleta hapa. Pia nilifurahia GYM yao ambayo ilikua imejengwa pembeni ya man made huku ikiwa imezungukwa na lovely garden. Kids Amani na Malaika walifurahia sana kufeed fish ambao walikua kwenye man made lake iliyokua inatoa maji yake toka kwenye ocean, walikua samaki wakubwa kweli.

I like to be in the place like this maana unajifunza vitu vipya kwa mfano inasemekana kuwa haya maji yanatokea chini sana, yanachukua thousands years kwenda chini na kurudi. Just amazing!!! Wengi wanakuja hapa kwa maswala ya medical wanasema kuwa maji haya yanafaida kiafya na yanatibu magonjwa kadhaa. Pia yanahadhari zake ukiwa kwenye pool uruhusiwi kuweka uso wako ndani ya maji, yakiingia kwenye pua yanaweza kuleta matatizo kwenye ubongo. Kitendo cha kuingia tu kwenye pool mwili wako wote unajisikia vizuri sana pia maji yake yako so warm, good temperature. Kwa ujumla hoteli imetufurahisha sana na tulisikitika kukaa kwa siku 2 tu. Tumepanga kurudi tena na safari hii tutachagua kipindi si cha mvua nadhani tutaenjoy zaidi :)))))) xoxo

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *