Sawasdee Village Resort, Phuket Thailand. July 2011

Around the garden

 

OMG! I don’t know where to start, one word  ‘Awesome’ Tulifika Sawasdee Village Resort tukitokea Phang Nga ambapo ilituchukua 1.30hr kwa usafiri wa barabara. Street ambayo hotel iko pako kawaida sana ni kazi kuamini kuwa kuna hoteli kama hii  mpaka utakapopata nafasi ya kuingia ndani ndipo macho yatakapokutoka ya kutoamini unachoona. Na kumbuka mimi na Amani tuliuliza sasa hiyo hoteli iko wapi? maana street tuliyokuwepo kulikua hakuelekei kama kuna hoteli yoyote. Tulipokaribishwa na kuingia macho yalitutoka na kusema wow!

Kuna watu wabunifu jamani, nikiwa mpenzi wa ubunifu hapa ni kiboko. Baada ya kucheck inn tulikabidhiwa personal assistant , kila ina personal assistant wake. Hapa kila kitu wanachofanya wanataka kumfanya mteja ajisikie vizuri kweli mteja ni mfalme. Personal assistant yuko kwa ajili yenu 24hrs, ukitaka msaada wowote unamtafuta yeye.

Kwa wale wapenda Spa hapa ndio penyewe Baray Spa ni one of the best Spa in Thailand. Napenda Spa haswa. This time niliamua kupata treat ya 3.30hrs nilichagua ‘Baray made in haven’ ndani ya masaa hayo unapata huduma kama Herbal Tea during treatment, Foot Bath, Kesa Massage, Vichy Shower, Choice of body massage, Reflexology foot massage & Choice of facial. After 3.30hrs nilijisikia mtu mpya maana ilikua kitu ingine. Magnificent!

Usiku mmoja tuliamua kwenda kutembelea Bangla road, mchana ni barabara usiku kunafungwa na kugeuzwa shopping. Hakika kuko busy ukiwa hapa unajua kumbe huko Phuket ndani ya Sawasdee Village Resort unasahau kabisa uko wapi.

Kwa ujumla Baray Villa ni kiboko, tulikaa for 3days lakini hazikutosha tulitamani kukaa hapo forever. Tumependa kila kitu kuanzia huduma, Baray Villa yenyewe, chakula na mengineyo mengi tu. Hakika lazima turudi hii ni kitu kingine kabisa iko tayari kwa kila mtu kuanzia familia, wapenzi na wenye honeymoon wote lazima mfurahi mkiwa hapa. Cheers Sawasdee Village Resort until next time :)) It was awesome!

One thought on “Sawasdee Village Resort, Phuket Thailand. July 2011”

  1. MY DEAR NTAOMBA HIZI PICHA NPATE DIZAIN YA NYUMBA YANGU NKIANZA KUJENGA ESPECIALLY INTERIOR DIZAINI HAHAHAHAHA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *