Rome &Vatican City, Italy 2003

With my hubby, St. Peter Church Vatican City

 

My 1st European country to visit and nilikua very happy hasa ukizingatia nilikulia kwenye familia ya catholic nilifurahi sana kuvisit Vatican city na kutembelea St. Peter church na kupata nafasi ya kumuona papa John Paul II live. Tulifika hapa tukipitia Milan then Rome ambapo tulikaa for four days na kupata muda mzuri sana wa kutembelea Rome na Vatican city.

Tulivyofika Vatican City nilishangaa kwa uzuri wa hii, kulikua na watu wengi ambao walikuja kutembelea hapa wakiwemo wale waliokuja kwa ajili ya maombi. Siku ya kwanza tulipata bahati ya kumuona Pope John Paul II, ilikua ni siku ya kubariki na akaingia kanisani wakati huo tulikua ndani ya kanisa la St. Peter.

Kanisa la St. Peter ni kubwa na zuri sana, watu walikua wengi sana kanisani na alipomaliza kubariki aliondoka. Mara nyingi kanisa huwa linaachwa wazi kwa ajili ya watalii na tulipata bahati ya kulizunguka na kupiga picha pia kwenda kuona wanapozikiwa ma pope na mengineyo mengi tu.

Kitu kingine kilinifurahisha ni kwamba tuliweza panda kwenye Dome la kanisa la St. Peter na kushuhudia view ya Vatican City vizuri ambayo ilikua ni nzuri sana. Pia tukiwa juu tuliweza ona garden ya pope ambayo ilikua ya kuvutia sana. Ila kusema ukweli cha moto nilikiona maana hizo ngazi za kwenda huko juu zilikua nyingi sana si kuchoka huko ila baada ya kufika juu nilifurahi maana view yake ni kiboko. Kwa ujumla Vatican City ina uzuri wake wa kipekee ambao nadhani uko wa kitofauti naamini kila mtu ambaye amefika hapa anaweza kukubaliana nami. Nilipenda sana mavazi ya askari wa Vatican City yalikua yanapendeza kweli. Kutokana na kupenda sana tulirudi tena the next day ili tuweze kutembelea maeneo mengi zaidi. Hakika nilifurahi sana na ningependa kurudi tena.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *