Mwanza Trip. Aug, 2011

Love u guys, mwaah!

 

Safari hii ilikua ni mara yangu ya tatu kuja kwenye jiji hili, tofauti ni kwamba safari zote mbili za mwanzo nilikuja kwa njia ya anga na sio barabara. Hii ilikua ni adventure nzuri sana kwangu na wote ambao tulikua kwenye safari hii, tulianzia safari yetu Dar kupitia Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga then Mwanza. Ni safari ndefu sana ambayo ilikua inatupeleka kijiji cha Burere, wilaya ya Rorya huko Musoma. Tulijumlasha kilomita zote na kupata zaidi ya kilomita 3,000 tulitumia kwenda na kurudi Dar. Safari hii ilituchukua siku nne ambapo tuliweza maliza kilomita zote hizo, tunamshukuru mungu tulisafiri salama na kurudi salama na safari ilikua ya mafanikio makubwa ingawa tulichoka sana.

Madhumuni ya safari hii ilikua ni kwenda kujenga kaburi la mdogo wetu ambaye alifariki karibu miaka 10 iliyopita. Safari hii ilitujumuisha watoto wote wa Fatuma yaani marehemu mama akiwepo kaka yetu mkubwa Hassan, mimi, mdogo wangu aliyenifuata Obuya ambaye tulimpitia Mwanza ndipo anapoishi na mdogo wetu wa mwisho Tina. Pia tulikua na ndugu yetu  Flora pamoja na Hamis ambaye alitusaidia sana kwenye maswala ya gari pamoja na udereva, ambapo walikua wanasaidiana na Hassan.

Tulianza safari yetu kutokea Dar saa kumi na mbili asubuhi na tuliwasili Moro mida ya saa 3 asubuhi hivi. Ila tulichelewa kutoka Moro kuelekea Dodoma kwa sababu ya tatizo dogo la gari ambapo ilituweka mpaka mchana ndipo tulianza safari yetu ya kuelekea Dodoma. Tuliwasili Dodoma kwenye mida ya saa tisa jioni hivi baada ya kujisaidia na kupata lunch tulianza safari yetu ya kuelekea Singida. Tuliwasili Singida kwenye mida ya saa kumi na mbili jioni hivi hapa hatukukaa kabisa baada ya kucheki gari na kujisaidia tuliendelea na safari yetu ya Shinyanga. Tuliwasili Shinyanga usiku kwenye mida ya saa nne hivi pia hatukupoteza muda baada ya kucheki gari na kujaza mafuta tulianza safari yetu ya Mwanza, tuliingia kwenye jiji hili kwenye mida ya saa saba usiku tukiwa hoi, choka kabisa na kuamua kulala hapa.

Asubuhi ya saa kumi na mbili tulianza safari yetu ya kuelekea Musoma ambapo tulipitiliza moja kwa moja kuelekea kijijini bila kuingia Musoma mjini. Tuliwasili kijijini kwenye mida ya saa sita hivi na kufanya shughuli iliyotupeleka na kumaliza kwenye saa kumi na mbili jioni na kuanza safari yetu ya kurudi Mwanza, tuliingia Mwanza kwenye saa nne usiku hivi baada ya kutafuta msosi na kula maana tulikua na njaa sana toka tule asubuhi ya siku hiyo hatukula chochote tulielekea hotelini na kulala. Kesho yake asubuhi tulianza safari yetu ila kabla ya kutoka mjini gari lilileta matatizo kidogo ikabidi tulipeleke garage, ilituchukua mpaka mida ya mchana hivi kabla ya kuanza safari yetu ya kuelekea Shinyanga.

Tulianza safari yetu ya kuelekea Dar kupitia Shinyanga, Tabora lakini si mjini, Singida, Dodoma, Moro then Dar. Safari hii tuliamua kulala Dodoma ambapo tulifika hapa kwenye saa mbili au tatu usiku hivi. Tulipata nafasi kwenye Veta hotel ambayo kwa ujumla ilikua nzuri. Kesho yake asubuhi tulielekea kwenye makaburi ya Kizota kwenda kutizama kaburi la mama ambapo alizikwa karibu miaka 21 iliyopita. Baada ya hapo tulipata breakfast na kuanza safari yetu ya kuelekea Dar mnamo karibu saa tano hivi.

Tuliwasili Dar kwenye mida ya saa kumi jioni hivi ila kutokana na foleni ilitufanya kuwasili home kwenye saa kumi na moja jioni. Kwa kweli safari hii ilikua ya mafanikio makubwa, ilikua ni adventure nzuri sana ambapo wote tuliokuwa kwenye msafara huu tunakubaliana nalo sote tulifurahi sana. Nina plan ya kurudia tena hii safari in the future ila this time nataka nisiwe na haraka ili nipate muda wa kulala kwenye mikoa yoyote hii ili nipata muda mzuri wa kuitembelea sio kama hii safari ambapo tuliingia na kupita tu. What an adventure, I love it!

 

 

5 thoughts on “Mwanza Trip. Aug, 2011”

  1. wow malaika na amani uliwaacha wapi jamani? Next tyme wabebe nao waone kwa barabara ila watahoi

Leave a Reply to mtagey Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *