Summer Holiday 2014-Day 3-Krabi, Thailand

Tuliondoka Bangkok siku ya tatu na kuelekea Krabi ni moja ya visiwa vilivyopo Thailand. Tumekua tukija hapa mara kwa mara toka mwaka 2003, imekua kama utamaduni wetu hatuwezi kuja Thailand bila kuja hapa angalau siku mbili tu. Sehemu hii imetulia sana na ina beach nzuri sana ambapo Railay beach ilishawahi kuwa one of the best beach in the world. Kufika hapa tulikuja kwa ndege mpaka Krabi Airport kutokea hapo tulipelekwa na gari mpaka sehemu ya kupandia boat. Usafiri uliopo kuelekea Railay ni wa maji tu hakuna usafiri mwingine wowote zaidi ya boat. Nashauri kama mtu ukipata nafasi ya kuja Thailand jaribu kutembelea kisiwa hiki nina uhakika uwezi kujilaumu :-)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *