Summer Holiday 2014-Day 6-Aonang Krabi, Thailand

DSCN8088

Baada ya kuwa Railay kwa siku tatu tuliondoka kwa njia ya boat kuelekea upande mwingine wa Krabi ambapo tulikaa usiku mmoja. Safari ya boat fupi sana ukilinganisha kama tungechukua boat kurudi Krabi town. Ilikua ni public transport so tulivyofika upande wa pili ilitakiwa tushuke na kubeba masaduku yetu wenyewe, sasa fikiria mama wa kiafrika tunavyojua kusafiri na vitu vingi wacha niangaike lol! Cha kuchekesha zaidi upande huo ulikua hauna taxi so ilibidi tuchukue usafiri wa pikipiki yenye miguu mitatu na masanduku yetu yalivyo makubwa si kubanana uko ilibidi tubebanane na mmoja kukaa juu ya sanduku huku mimi ilibidi nimbebe baba Amika ni vituko lakini tulifanikiwa kufika hotelini ambapo hapakuwa mbali ni kama dk 5 tu tatizo sehemu hii iko busy sana. Njiani tukawa kama kiburudisho cha watalii maana watu walikua wanashangaa tuliwezaje kutosha wote kwenye hiki kipikipike. Watoto wacha wafurahi maana familia hii kwa kupenda adventure :-) Now this is what we call an adventure!!!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *