Tag Archives: sana

Summer Holiday 2014-Day 10-Koh Nangyuan Island resort, Thailand

DSCN8437

Jioni familia iliamua kwenda kupanda kilima ili waweze pata view nzima ya visiwa vyote vitatu. View ya huko ni nzuri sana ila tatizo ni ngazi za kupanda kufikia huko so niliamua kuwaacha waende wenyewe. Kama picha zinavyoonyesha ni pazuri sana and the view is amazing! :)

 

Summer Holiday 2014-Day 4-Krabi, Thailand

Siku yetu ya nne tuliamkia bado Railay Krabi na tuliamua kuitumia kwa kushinda beach. Kama nilivyosema mwanzo beach hii imeshakua one of the best beach in the world. Kama inavyoonekana kwenye picha inapenda sana tena sana. Kitu kingine kinachofurahisha kwenye beach hii unaweza kukaa ukarelax na kupata massage toka kwa local people ambao unalipia pesa kidogo tu :-) Ila uwe tayari kukubaliana na michanga Lol! Amani na Malaika ni wapenzi sana wa beach msipo angalia wanaweza kuwakalisha huko siku nzima hawachoki kabisa, wanapenda sana maji.

Family weekend getaway at Alila Resort, Oman-July 2014

With my babies
With my babies

Weekend hii tuliamua kwenda countryside na kufikia kwenye hii hotel ambayo imefunguliwa mwaka huu huu. Ilituchukua masaa mawili na nusu kutokea Muscat kufika hapa. Hotel iko juu kabisa kwenye mountain na hali ya hewa ni nzuri sana hasa kipindi hiki ambacho Muscat ni 42 na huku juu ilikua only 23. Nasikia kipindi cha winter huku ni baridi sana inaweza fika mpaka 0. Tulivyofika tulifurahije sasa maana ni pazuri sana kama inavyoonyesha kwenye picha :)

Family at Turtle Beach, Oman. Jan, 2014

With my babies
With my babies

Hapa ilikua ni kipindi cha winter si baridi hiyo. Kupata nafasi ya kuona hawa Turtle inabidi muamke asubuhi sana kabla ya jua kutoka. So tulilala hotel ambayo iko karibu na eneo hili ambalo limetengwa na serikali kwa ajili hiyo. Tulifika kwanza usiku kuangalia wakiwa wanataga mayai na asubuhi ni pale watoto wanavyotoka na kuelekea baharini. Inashangaza sana inasemekana kuwa hawa watoto nao baada ya miaka mingi wakianza kutaga lazima waje sehemu waliyotokea kutaga na wao hata kama kukatiza dunia lol! Ni story inayoshangaza na kufurahisha na inapendezeza sana. Amani na Malaika walifurahi kupita kiasi.

One Week In Dar es Salaam, Tanzania. July 2013, Part II

 

@ Karambezi Sea Cliff hotel
@ Karambezi Sea Cliff hotel

 

Nilifurahi sana kukutana na marafiki zangu wapya Jessie & Irene ambao tumekua tunawasiliana muda mrefu atimae tulipata nafasi ya kukutana uso kwa uso nilifurahije sasa, asante sana lovely ladies. Pia nafurahi kupata muda angalau kukaa na wadogo zangu Celine, Tina, Scolar, Flora. Asanteni kwa muda wenu mlionipa pamoja na vicheko tulivyocheka…hahahaaa…mnakumbuka dada wa reverse pale kivukoni? lol! yaani hapa nacheka kweli bongo darisalama panapendenza lol. Uncle Festo asante sana kwa kuja kukutana nami yaani nilifurahije sasa uncle wangu, asante kwa kila kitu :)

Siku saba si nyingi kwa kweli kwa bongo yaani nilitamani niendelee kukaa zaidi kweli nyumbani ni nyumbani huwa siichoki Dar es Salaam yetu. Celine Victor mdogo wangu karibu sana maisafari <3  :)