Venice Italy, 2003

Venice City

 

Nachoweza sema ni wow! na ushamba wangu wote hapa uliisha. Venice City ni ya kipekee kwa kweli yaani kila kitu kinapendeza yaani design ya mji inafurahisha sana. Mitaa yake ni maji ni vidaraja tu ndio unakatiza kufikia mtaa mwingine usafiri wake ni boat au baiskeli nadhani hata pikipiki.

Ingawa tulikua tunajua mji uko juu ya maji lakini tulikua tunafikiria kuwa labda kuna usafiri wa barabara endapo kidogo. Tulipata kichekesho baada ya kutelemka toka kwenye train tukitokea Rome tukajifanya tunatafuta taxi na kuonyeshwa taxi zenyewe kumbe ni boat. Sasa kasheshe ilikua ni sanduku langu ambalo lilikua limejaa zito hilo ikabidi tuingie kwenye boat taxi hahahaa..tulivyofika sehemu tuliyotakiwa kushuka ikawa ni upande wa pili wa maji tunatakiwa kuvuka daraja kubwa kuelekea upande mwingine. Maskini hubby mbona shughuli ilimpata ya kubeba sanduku langu.

Tulipofika upande wa pili pia ikawa kasheshe nyingine maana atujui hoteli yetu iko wapi na ukizingatia hakuna usafiri wa bara bara ni vichochoro kuitafuta hiyo hotel ilikua mbinde. Ikabidi mi nibaki nyuma na mizigo so hubby aende kutafuta hotel kwanza na akipata ndio aje nichukua kwa bahati nzuri alipapata. Si kuchoka huko ila tulifurahia hotel maana ilikuwa bado mpya na nzuri.

Tulikaa Venice kwa siku nne na katika siku hizo tulienjoy kutembelea sehemu tofauti na kufanya kijishopping kidogo. Chakula kama unavyojua Italy kilikua kitamu kweli my favourite iliku pizza jamani nimekula pizza tamu sana kipindi chote nikiwa Italy. Moja ya pizza ambayo siwezi kusahau nilikula Vatican City ilikua ndogo na expensive ila hiyo Hawaian pizza ilikua kiboko. Kwa jinsi tulivyopapenda tulisema tutarudi tena ila cha kushangaza mpaka sasa bado tunapanga hahaaaa…ila lazima turudi tena na this time tungependa kwenda wakati wa summer maana si tulienda kipindi cha winter so kulikua na kibaridi.

 

2 thoughts on “Venice Italy, 2003”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *