Zawadi’s Diet

Baada ya watu wengi  kuniuliza nimefanya diet gani kupunguza kilo zangu nyingi nilizokuwa nazo nimeamua kushare nanyi siri ya mafanikio yangu. Kusema kweli mi ni kati ya watu wengi ambao wanaangaika na hii kitu kinachoitwa weight. Nikiwa nimeshajaribu diet za aina tofauti kwa miaka kadhaa na kusoma vitabu vingi vya kuhusu diet pamoja na kujaribu pia nimejikuta mara kwa mara naishia njiani au kushindwa kabisa kutokana na ugumu wa hizo diet au kutokana na utofauti wa maisha. Pia utofauti wa chakula ambacho pia tumekulia nikawa najikuta badala ya kuenjoy nakua najitesa tu na mwisho wake ni kuamua kuacha kabisa kufuatilia hizo diet. Mpaka siku moja niliposoma kitabu kimoja ambacho kilinigusa sana ambacho chenyewe kinaelezea diet ya emotional na sio chakula hapo ikanigusa haswa.

Kitabu kinaelezea tatizo kubwa la watu ambao ni over weight ukiangalia kiundani si kuwa ni chakula tu kuna mengi. Kitabu kinatuhita watu kama sisi ni ‘Emotional Eater’ kwa kweli nilijiona kama wananiongelea mimi maana kwangu mimi kila kitu kinazunguka na chakula napenda sana kula na kila mara nikila si kwa sababu nina njaa la nakula nikiwa na furaha, huzuni, mawazo, hasira or just bored.

Uamuzi wangu ulifikia kuwa sitaki kumaliza mwaka wangu wa 35 nikiwa naangaika na hii habari ya weight. Ikabidi nilikafanya uamuzi mzito kuwa kwa hali yoyote lazima nitoe huu unene ambao unanikosesha raha kwa muda mrefu sasa na sio tu sipendezi pia nika naanza kuchoka choka sana na kuwa mtu ambae napenda kulala lala sana nikaona kuwa mwili wangu unalia kuwa nahitaji kuchange situation napoelekea ni kubaya kabisa. Pia kitu kingine kilichoniamsha ni picha za mwanangu Amani kwenye 2nd birthday yake nilijiangalia na kutojitambua kuwa ni mimi maana muda wote nilikua najipa moyo kuwa niko mnene ila si sana.

Nilisikitika kufikia kiwango hicho na nisipoangalia naelekea pabaya sana, najua sikuwa hivyo kabla sijazaa na maswala ya uzito kwangu ni kitu cha kawaida nimekuwa naongezeka na kupungua ila sijawahi fikia kiwango hicho. Nikaamua kuchukua diary na kuanza kuandika chini sababu iliyonifanya kufikia hapo nilipo. Kwanza kabisa wazo la uzazi likanijia maana within 3yrs nimeweza kuwa na watoto wawili yaani kabla sijamaliza toa uzito wa mtoto wa kwanza nikabeba mimba ya mtoto wa pili, nilipojifungua huyo wa pili mambo ya kupungua yakazidi kuwa magumu zaidi. Nilikua 2 choice watoto au mwili wangu nikiwa mama kama mama wengine nikachagua watoto kwanza. Uamuzi huo ulinipeleka kwenye uamuzi wa kunyonyesha maziwa ya mama wanangu kwa miezi yao sita ya mwanzo bila kitu kingine hata maji, na uamuzi huo ulikua unanilazimu kula chakula kingi hasa watoto walipokua wanafikisha miezi minne maana muda huo wanakua kwa kasi na wanahitaji chakula zaidi. Kwa sababu hiyo wanangu walikua wanapata chakula chao chote toka kwangu ikabidi niongeze kula zaidi ili niweze kupata maziwa mengi maana walikua wananyonya kila wakati na nisipokula kulikua hakuna maziwa ya kutosha so nikawa nakula zaidi.

Kwa upande mwingine siwezi kulaumu uzazi kwenye issue yangu ya unene kwani mimba zangu zote sikuongezeka sana na nilipojifungua tu kilo nyingi zilitoka baada ya  miezi kadhaa ya mwanzo mwili wangu ulianza kurudia hali ya zamani kabla ya ujauzito. Nadhani nilichokosea ni pale walipoacha kunyonya ilitakiwa nami kupunguza kiwango cha chakula nilichokuwa nakula kwa siku yaani nilitakiwa nikate nusu nzima na sikufanya hivyo badala yake niliendelea kuenjoy chakula kama kawa ukilinganisha napenda msosi basi ilikua balaa. Mwili ulianza kupasuka kwa kasi na kuendelea kuongezeka kila siku mpaka kufikia kiwango ambacho sikuwa na furaha nacho kabisa.

Nikaamua kuutolea uvivu unene, nikachukua karatasi na kuanza kuandika kila kitu nachokula kwa siku ilipofika wiki nikaangalia nilishangaa kiwango cha chakula nachokula mtu mmoja kilikua ni kingi sana na hakikuwa chenye afya wala hakiko balance diet kabisa. Nikaamini kuwa kumbe wanaosema kuwa sehemu kubwa ya unene inatokana na  kula chakula kingi kupita uwezo wa mwili wako. Sehemu kuwa ya chakula changu ilikuwa wangu kama sijakosea nadhani ndio vyakula vyenye carbs nyingi, napenda sana wali nakula sahani kubwa sana na sijali hata kama nitakula wali siku nzima mi niko happy, pia vitu vya unga kama chapati nami kwa chapati unitoe kabisa naweza kula chapati mpaka 10. Nafanya hivi only kwa chakula nachopenda ila kama chakula sikipendi basi huwa sigusi kabisa.

Nimejaribu diet nyingi sana zingine zinakupa mafanikio kwa muda mfupi then hali inarudia vile vile kama una bahati la sivyo unaweza ukaongeza zaidi. Ndipo nilipofikia kutengeneza diet ambayo inanifaa mimi na ambayo nitaweza kuifuatilia kwa kipindi kirefu bila kuchoka, nikajaribu kuunganisha kutoka kwenye diet ya low carbs na kujaribu kuandaa ambayo itanifurahisha mimi na nitaweza kuifanya ndipo nikaja na hii diet ya six days a week na unajipongeza siku moja ya wiki kwa kula chochote unachotaka. Pia nikaangalia zaidi kwenye upande wa nutrition zaidi maana sikupenda kupunguza unene na kuonekana kama vile mgonjwa au hata kuanza kupata matatizo mengine ya kiafya. Kwahiyo nikaona diet ya kupunguza kilo moja kwa wingi ni nzuri zaidi maana nimesoma kwenye vitabu vingi wanasema kuwa ndio njia ya afya kupunguza kilo kwa wiki maana hiyo kilo inatoka kwenye fat zaidi.

Kwa diet hii imenichukua karibu miaka 2 kufikia weight loss niliyokuwa nataka maana nilikua natakiwa kutoa 25kg. Na tatizo lilikua kwamba nilikua naongezeka na kupungua kutokana na kusafiri mara kwa mara kwenda holiday na sikuweza kustay away from delicious food na matokeo yake ilikua ni kuongezeka kilo kadhaa. Nachoshukuru mungu nimeweza kuzitoa kilo zote 25 na kufikia kiwango nilichotaka, sikutaka kufikia uzito niliokua nao wakati naolewa maana mambo mengi yamepita umri nao umekwenda na kujumlisha watoto wawili juu yake nilitaka nifikie kiwango ambacho nitakuwa niko healthy na pia najisikia kuwa niko mrembo. Kwa urefu wangu weight inayotakiwa ni between 71 to 73kg ndio nayotaka niwe nacheza nayo, nashukuru nimefikia hiyo 71 ingawa shepu ya mwili wangu imebadilika kuna sehemu zingine siwezi kuzirudisha kama nilivyokua kabla ya kuzaa, nachoshukuru niko happy na weight niliyonayo sasa. Najua nitakua naongezeka na kupungua mara kwa mara maana ndio maumbile yangu yalivyo ila nitajitahidi niwe nacheza hapo sana 71-73kg.

Kilo zote hizo nimezipunguza kwa maangaiko kweli na kazi kubwa inachotakiwa ni moyo wako kuwa umekubaliana na hali kuwa lazima utoe huo uzito kwa heri au shari then nadhani mafanikio utayaona. Mwanzo siku zote huwa mgumu mimi nilianzia  GYM ambayo ilinisaidia kutoa kilo 10 zangu za mwanzo lakini muda ulivyokuwa unaendelea nikaanza kuona uvivu kwenda. Nikaamua kununua vifaa tofauti vya mazoezi ambapo ningeweza fanya mwenyewe home cha kuchekesha baada ya mwezi nakua tena situmii kifaa hicho na kinaanza kupigwa vumbi tu na nimefanya hivyo kwa kununua vifaa vingi tofauti na kupoteza pesa nyingi  vyote vimeishia kupigwa vumbi mpaka leo.

Ndipo nikaja na plan yangu mwenyewe ya mazoezi ambayo nitaweza kuifuatilia. Pia hata kama nikicheat now and then sitojisikia vibaya wala kukata tamaa ya kuendelea. Kila asubuhi sana naamka saa moja na nusu kabla familia yangu haijaamka na kwenda for a walk, then jumping in kids trampoline ni kubwa hata watu wazima wanaweza tumia. Pia nikaanza kumove more yaani kila mara naamua kufanya kitu ambacho natumia nguvu kidogo kama house work niliamua kumsimamisha full time house maid na kuweka wa part time so siku ambazo haji mi ndio nafanya kazi za nyumba.

Nilivyoweza mambo ya mazoezi pia nikaweza mambo ya diet, vyote hivyo vinatakiwa kwenda sambamba. Nikajiwekea kuwa nitakula chakula cha kwetu yaani TZ food mara moja kwa wiki nikachagua Thursday maana hapa tunapoishi ni weekend. Niliona Thur ni siku nzuri maana ni siku ambayo familia tuko pamoja na ndio siku ambayo natengeneza chakula cha kutoka home TZ ndio msosi pekee ambao roho inanitoka nikiuona, napenda sana chakula cha kitanzania. Siku hii pia ndio naweza kujiachia kwa kula vyakula kama  rice, ugali, bread, pasta, chapati, maandazi, ndizi, carrot, maembe, viazi, chips any food ambayo ina carbs ambavyo siruhusiwi kula siku za diet. Pia siku hii ndio napima uzito wangu kuangalia mafanikio niliyoyafanya wiki nzima ya diet. Napita uzito the same time pia navaa nguo zile zile nilizovaa mara ya mwisho nilipopima hiyo inasaidia kujua kwa uhakika umepungua kiasi gani. Wanashauri kupima uzito mara moja kwa wiki hiyo inasaidia kujua kwa uhakika weight ambayo umepunguza kwa kupima uzito pia inakupa moyo wa kuendelea baada ya kuona mafanikio yake, usikate tamaa kama ukupunguza uzito wiki hiyo maana wakati mwingine mwili unakua na tabia ya kustop.

Kwa hiyo wapendwa ningependa kuungana nanyi katika haya mapambano ya kupunguza uzito naamini kuwa kuna watu wengi wanaangaika kama mimi katika hii issue. Diet yangu si ngumu mtu yoyote anaweza kuifanya cha msingi ni kuwa na moyo kuwa utaweza na kuwa na nia mafanikio yake ni makubwa na utafurahi mwenyewe. Ukishafanikiwa kupungua zaidi au umefikia kiwango unachotaka unaweza kubadili na kuanza kula unachotaka 2days a week.  Kwa sasa mimi nimefikia weight nayotaka nafanya diet yangu 5days a week na kula nachotaka on weekends pia napumzika na mazoezi. Ila siku ya kwanza ya wiki biashara inaendelea pia napumzika kidogo kidogo nikiwa holiday inategemea ni holiday ya siku ngapi.

Wapendwa narudia tena diet hii ni rahisi na ya kumfanya kila mtu ajisikie vizuri at the same time una enjoy maisha. Nitapost 1 week diet ambayo imenisaidia sana ila wewe unaweza kuwa creative na kubadilisha chakula cha kula maadam kiwe low carbs na kufuata mfumo wangu au unaweza kubadilisha kidogo na ukiona kwenye wiki imefanya kazi basi unaweza endelea nayo safari yote hii ni kumfanya mtu ajisikie vizuri kufanya hiyo diet na kutokata tamaa na kupata mafanikio ya kupungua. Kwa wale ambao mko creative pls msisahau kushare nasi ili sote tupate kufaidika. Hii web ni ya wote so pls usisite kushare pamoja nasi idea uliyonayo ambayo inamafanikio katika maswala ya loss weight. Nadhani tunaweza saidia wengi kwa mfumo huu karibuni sana and all the best. Cheers!

13 thoughts on “Zawadi’s Diet”

      1. Judith, mbona iko tayari angalia kwenye 6days diet then angalika mon-sat diet. Tizama ipi inakufaa ni rahisi nina hakika utaiweza tu. All the best, Cheers!

  1. maneno nimengi sana, nimesoma baadhi….lakn diet yenyewe cjaiona, plZ naomba unitumie io diet

    1. Hi brenda,
      Cha msingi jitahidi kula chakula ambacho hakina wangu kama vile ugali, chapati, wali, mihongo, viazi na kadhalika. Jaribu kula kwa wingi mboga za majani pamoja na samaki au kuku. Matunda jitahidi kula mara moja kwa siku ila usile ndizi za kuiva au maembe. Pia kwenye salad usile carrot maana zina sukari nyingi. Jaribu kutokula vitu vya sukari kama soda au juice za madukani. Kunywa maji lita mbili kwa siku pia kunywa madafu yanasaidia. Usinywe chai na sukari kabisa maana diet hii haitakiwa sukari kabisa.

      Nakutakia mafanikio mema, ukiamua utaweza na utafanikiwa kabisa.
      XOXO
      Zawadi

  2. hi dada zawadi , mie nataka kupungua mchana najitahidi kula matunda tu ila napendelea kula tikiti maji ni vizuri au na km sio nzuri matunda gani nile yasiyokuwa na shida?

    1. Hi dear, ndio matunda ni mazuri pia tikiti Ni zuri sana. Ila jitahidi kutokula usiku na ule mchana na asubuhi. Jioni jitahidi kula salad tu.

  3. hellow!!!!
    asante nimefurahi kwa kushare nasi diet yako na pia kutupa moyo kwetu sisi ambao ndo kwanza tuko kwenye changamoto hii ya kupunguza uzito.Pia napenda kufahamu kama avacado ni zuri kwani me huwa napenda kuchanganya na tango nakula kama kama salad.
    Nakutakia siku njema*

    1. Hellow Victoria,
      Karibu, ndio dear ovacado ni zuri sana tena lina faida kubwa sana mwilini. Hata mimi ni mpenzi sana wa ovacado.
      Zawadi
      XOXO

Leave a Reply to Anonymous Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Safiri na Zawadi