Category Archives: Cambodia

Siem Reap, Cambodia 2003

One of the temple

 

Nikiwa ni mmoja wa watu wanaopenda historia ya mambo ya kale. Ndio kisa hasa kilichotuleta hapa Siem Reap kuja kuangalia temples za Angkor Wat. Zikiwa na nyingi na zimejengwa karibu eneo moja inasemekana kuwa enzi hizo pande hii ulikua moja kati ya miji mikubwa. Tulifika hapa tukitokea Bangkok na tulikaa kwa siku tatu ambazo zote tulizimalizia kuzungukia temples. Inasemekana kuwa kwa miaka mingi temples hizi zilikua zimefunikwa kabisa na msitu mkubwa sana hata watu waliokua wanaishi karibu na eneo hili walikua hawajui karibu yao kuna kitu kama hiki.

Ndipo ilipokuja kugundulika na mwana research wa vipepeo ambaye alikua katikaka harakati zake za kutafuta vipepeo ndipo alipokutana na kitu kama hiki.

Kwa wale wapenda movie kama umewahi ona sinema aliyo act Angelina Jolie ya kwanza Tomb Raider sehemu nyingine ya movie walichukulia hapa kwenye hii temple ambayo imeotea miti juu yake, inapendeza kwa kweli.

Hatukupata nafasi zaidi ya kutembelea mji huu wa Siem Reap. Ila hotel tuliyofikia ilikua ni nzuri tu ambayo iko mjini kabisa. Bahati mbaya sikumbuki jina la hoteli yenyewe ni miaka mingi imepita sasa.

Tulipata nafasi ya kuzunguka na Balloon na kupata view nzuri sana ya Angkor Wat, ukiangalia kutokea juu inapendeza sana kuona mpangilio walio tumia hawa watu wazani yaani walikua wazuri. Kwa ujumla nilifurahi kuwa part ya hii historia na nilifurahi sana.