Category Archives: My diet

My Two Weeks Vegan Diet

Haya wapendwa baada ya kujiona nimeongezeka karibu 7kgs nikaamua ngoja niende extra mile na kufanya hii crush diet ambayo imenisaidia kutoa 4kgs just for 2weeks. Ingawa bado naendelea ambapo niko wiki ya tatu sasa, nataka kujaribu kwa mwezi ili nione kama nitafanikiwa kutoa kilo zote 7. Kwa kweli ni ngumu kidogo inabidi ukaze buti kisawa sawa ila mafanikio yake ni makubwa. Unachotakiwa ni kufanya diet kwa siku 5 za wiki mfululizo na siku mbili unakula chochote unachotaka wewe ili kubalance. Nilichofanya ni kubalance kidogo ambapo nimejitahidi sana kuweka vitu vyote muhimu vya mwili kwenye smoothie ambayo nakula kwenye mida ya saa 9 mpaka 10 jioni. Pia lazima ninywe maji lita 2 kwa siku ni muhimu sana.

Asubuhi:  Kama kwaida lazima ninywe maji nusu lita ya uvugu uvugu kuamsha tumbo baada ya hapo naenda mazoezi ya kutembea saa 1 na dk 15 then nafanya mazoezi ya kuruka kwa dk 15 na mazoezi ya tumbo na viungo dk 30. (Wewe kama utakua huna muda usijali sana unaweza fanya mazoezi yoyote kwa dk 30 na weekend ukajitahidi kufanya mazoezi zaidi)

Chakula cha asubuhi:  Nakula nuts kiganja cha mkono kimoja, mimi napendelea karanga au korosho wewe unaweza kula nuts zozote unazopenda ila almonds ni nzuri zaidi.

Mlo wangu wa siku ambao ni smoothie naula kwenye mida ya saa 9 mpaka saa 10 jioni, na mlo wangu wa mwisho usizidi saa 11 jioni ambapo baada ya hapo hakuna chochote nachokula zaidi ya maji mpaka kesho yake. Najitahidi kwenda kulala mapema ili niweze kulala masaa 8 kwa siku

My Smoothie:

Ni mchanganyiko wa 2 medium cucumber(matango), 1 medium mango(embe), 1 medium ovacado(parachichi), 1 cup soya milk(kama una soya milk unaweza tumia low fat milk or full fat mill) pia nachanganya tunda lolote lenye rangi nyekundu unalopenda pia unaweza kuweka nyanya, mimi naweka strawberries chache sana kama tatu hivi au Pomegranate kiganja kimoja.

Changanya mchanganyiko wote pamoja na upate smoothie ambayo iko nzito kama uji ambapo utaweza kula na kijiko, kama vile chakula cha mtoto mdogo vile.

Ok wapenzi jaribu hii uone mafanikio yake na ukifikia uzito unaotaka then unaweza kurudi kwenye diet yako nyingine ambayo iko balance au unaweza kufuata my six days diet.

Nimejitahidi kuchanganya virutubisho muhimu mwilini ili mwili usikose vitamins kadhaa, kwa mfano embe ni tunda, ovacado ni veg and tunda na linasaidia kupata mafuta mwilini sababu mwili unaweza kosa mafuta kabisa, cucumber ni vegetable ambayo ina umuhimu mzuri mwilini na kwenye upande wa calcium nimeweka soya milk kwa wanawake ni muhimu sana kupata calcium zaidi mwilini. Wewe unaweza kufuata mtiririko wangu na ukaweka matunda na vegetables unazopenda wewe ni sawa tu.

All the best wapendwa, Zawadi.

XOXO