My Siri Ya Kupungua Uzito

5 days a week naamka saa kumi na robo alfajiri naenda for a walk, nikirudi nafanya mazoezi ya mikono kwa dk 40 au zaidi maana mi na mikono minene, nikimaliza nafanya mazoezi ya tumbo sit ups kama 100. Pia naweza fanya kazi za ndani kidogo au kitu chochote kama kuandaa watoto kwa ajili ya kwenda shule kwa wale wenye watoto wadogo ili nalo ni zoezi, unaweza jikuta wakati mwingine unakimbizana nao karibu saa nzima mpaka mkute mmemaliza shughuli zote, ili pia limenisaidia.

Diet yangu kama kawaida sili vitu vyenye sukari kabisa kwa siku 5 za wiki kama vile wali, mkate, viazi, ugali, chapati, ndizi za kupika, pasta, sukari, etc. Badala yake nakula salad kwa wingi pamoja na samaki, nyama ya kuku, mayai, nyama ya ng’ombe ambayo nakula mara moja kwa wiki.

Matunda ambayo nakula aina mbili au tatu kwa siku ni kama vile Pears, Apple, Kiwi, Melon, Avocado ambayo nakula kama tunda au vegitable, Papaya na Machungwa.

Nakula nuts ambazo zinanisaidia mfuta mwilini ili nisipauke na kuzeeka pamoja na vitamins nyingine. Nuts nazopendelea kula ni Almonds ni nzuri sana pia zinasaidia kupunguza uzito maana zina calories ndogo sana mara nyingi huwa nazo kwenye pichi natembea nazo popote ili nikisikia njaa tu natafuna moja mbili tatu, pia napendelea sana karanga na korosho.

Kila nikiamka toka kitandani kabla sijapiga mswaki nakunywa maji nusu lita ambayo ni ya room temp ambayo ya kawaida tu sio baridi, ila kama unapenda ya moto ni mazuri zaidi mimi yamenishinda. Nahakikisha mpaka ifikapo usiku kabla sijaenda kitandani kulala nimeshakunywa maji yangu ya siku ambayo ni lita 2.

Kitu ambacho ni muhimu nafanya ni kwamba siwezi kula chochote zaidi ya maji ifikapo saa kumi na moja jioni kwa hizo siku tano za wiki. Mlo wangu wa siku lazima uwe saa kumi na moja jioni baada ya hapo naendelea kunywa maji tu hata kama nimemaliza lita 2 naendelea kunywa mengine zaidi maana maji ni mazuri kwa mwili hayana madhara.

Kitu ambacho niligundua ni kwamba napoenda kulala mapema napata nafasi ya kuamka mapema kwa ajili ya mazoezi pia inanisaidia kupata nafasi ya kulala masaa nane ambayo ni muhimu kwa binadamu. Endapo nitashindwa kulala masaa yote hayo usiku basi lazima nitafute muda kwenye day time nilale angalau kufidia muda ufikie angalau karibu na hayo masaa nane.

Kuna wakati mwingine nasikia njaa sana nachofanya ni kutafuta shughuli ya kufanya kama naangalia TV inabidi niache maana TV inaongeza njaa sana huwa najisikia kila mara nataka kutafuta kitu. Nachofanya naenda kusoma kitabu au naenda for a walk kama ni usiku basi naamua kwenda kulala hata kama ni saa mbili usiku kwangu mimi ni rahisi maana watoto wangu wanakua tayari kindani muda huo wanaenda lala kila siku saa moja na nusu usiku.

Pia najitahidi sana wakati nawapikia watoto au mume sionji kabisa chakula kama ikitokea kuonja basi simezi natema ili nisiweze haribu diet yangu. Kwa hizo siku 5 najitahidi kuepuka ndizi na maembe, Zina sukari nyingi na sio nzuri kwa diet yetu badala yake naamua kuzila siku zangu hizo mbili ambazo ni weekend ambapo naruhusiwa kula chochote nitakacho.

OK WAPENDWA HII NDIO SIRI YANGU NIMEWEZA KUSHIKAMANA NAYO KARIBU MIAKA MIWILI NA IMENIPA MAFANIKIO MAKUBWA MPAKA SASA NIMETOA KILO 28, NAWEZA KUSEMA KUWA NIMESHINDA UNENE SO FAR KAZI KWANGU ILIYOBAKI NI KU KEEP THIS WEIGHT NILIYONAYO NISIJE NIKARUDI TENA NILIKOTOKA. KUMBUKA KUNA KUPANDA NA KUSHUKA KATIKA SAFARI YA KUPUNGUA KITU MUHIMU NI KUTOKATA TAMAA, SIKUKATA TAMAA NDIO MAANA NIMEFIKA HAPA NILIPO INGAWA MARA NYINGI TU NIMEKUA NAPOTEA KIDOGO ILA THE NEXT DAY NAENDELEA MPAKA KUPATA HII FAIDA NILIYONAYO SASA.

ALL THE BEST GUYS AND CHEERS!

20 thoughts on “My Siri Ya Kupungua Uzito”

 1. wow asante sana kwa kushare nasi diet yako, nina tatizo lakupenda chapati na wali mpk nachanganyikiwa nimeanza fata diet yako hope nitapungua kwani nina 78kg nataka nipunguze mpk 68kg i hope nitaweza although huwa na cheat diet,pia mdada naomba unielekeze mazoezi ya mkono kwa kweli nina mkono cyo mchezo, lov u xoxo…………..

  1. Kuna aina km tatu hivi huwa natumia kwa mazoezi ya mkono, kwanza push up, kupiga ngumi hewani kama vile mia 2 kwa siku na pia huwa nina machine ya mazoezi ya mikono inaitwa TrimBike. Pia jitahidi kufanya mara kwa mara kazi za nyumbani kama vile kufagia au vaccum, kupiga deki, kuosha vyombo, gardening na kadhalika pia zinasaidia sana. Tuendelee wasiliana kama una swali lolote pia usihofu ukiona ume cheat usike tamaa next day endelea tu na diet.

 2. Hello,

  habari ya sahiz mimi naitwa ALLY labda tu dada yangu nilikuwa nataka tu nikuabarishe kuwa na matatizo ya tumbo yani na kitambi so utanisaidiaje ili nikipunguze

  asante sana

  1. Dear Ally,
   Habari, nachoweza kukusaidia kwa haraka ni kwamba kama unakunywa pombe inabidi uache pia kama unakula sana nyama nyekundu kama vile ng’ombe etc pia upunguze. Kitu kikubwa kabisa anza diet ya kukata kabisa vyakula vya wanga kama vile ugali, wali, chapati, maandazi, mihogo, viazi etc na badala yake kula sana samaki na mboga za majani na kama unaweza fanya za kuchemsha au kuchoma. Pia jitahidi angalau kila siku kwa dk 15 mpaka 30 kufanya zoezi la tumbo. Unaweza pia kuangalia my diet kwenye post zangu. Nakutakia all the best na karibu kama una swali lolote.
   Zawadi

 3. zawadi,
  nimefurahi sana,yaani mimi na angaika sana na weight yangu hii ila nimeanza kama wewe ila nilichojiona ni kwamba nakula sana ndizi ambayo nimeona nakosea sana alafu wakati napakulia baba na mwana uwa kwa kweli nakulaga kijiko kimoja kimoja ambayo nao naona ni kosa pia…vile vile nakula hata sambili ila ni matunda…nipe muongozo hapo ila kupungua nimepungua kidogo na mazoezi kwa kweli hata sifanya kwa kukosa muda…

  1. Dear Grace,
   Ndizi si nzuri kwa low carbs diet jaribu kupunguza kidogo kama kweli unazipenda. Mimi napenda sana maembe na kwa diet hii si nzuri but nakula mara moja moja. Jaribu kutodokoa chakula cha watoto au Mr. maana hata kama ni kidogo kidogo but inakupunguzia kasi ya kupungua. Ukishindwa kabisa kuacha kula saa kumi na moja fanya angalau kumi na mbili. Baada ya hapo usile kitu kabisa zaidi ya maji au green tea bila sukari. Kuhusu matunda jaribu kula asubuhi, jioni kwa diet hii vitu vya sukari havitakiwi kabisa.

   All the best dear, tuko pamoja.
   XOXO

  1. Dear Malaika,
   Mimi pia nasumbuliwa na mikono minene, jaribu wakati unatembea beba kilo moja kila mkono inasaidia. Pia fanya push up na unaweza kufanya mazoezi ya kupiga ngumi hewani.

   All the best dear
   XOXO

 4. habali yako dada mm ninamikono minene juu chini myembamba yaani hata kuvaa nguo iliyowazi nikifanya hili zoezi itapungua kweli maana
  ni shiiida

  1. Hi Fatuma,
   Pole sana maana nami pia nikinenepa mikono yangu nayo inanenepa sana. Nakubaliana nawe mikono minene inakosesha raha hasa ukitaka kuvaa nguo za kuachia mikono wazi. Mimi nafanya sana mazoezi ya mikono kama vile push up ingawa sipendi kabisa ila najilazimisha tu. Pia wakati natembea nabeba uzito wa kilo moja kila mkono pia inasaidia. Jitahidi pia kufanya zoezi la kupiga ngumi hata hewani tu huku umeshika kitu cha uzito angalau wa nusu kila na unaongeza kilo jinsi unavyojisikia. Pia kazi za ndani kama vile kufagia au kufua au kudeki kwa mikono nandhani pia inasaidia sana.
   Zawadi
   xoxo

  1. Hi Claudia,
   Diet bila mazoezi inawezekana ila sikushauri kufanya hivyo maana mazoezi yanasaidia mambo mengi, kuanzia afya pia kukaza mwili. Si lazima ufanya mazoezi magumu hata kutumbea tu inasidia. Kwa hiyo kama unatembea kwa kasi angalau dakika 45 mpaka saa moja hiyo inatosha.
   Zawadi
   xoxo

 5. Mambo Sis,
  Nimependa posti yako. Vilvile nimeishea katika Facebook. Na mimi nina kilo nyingi sana. Nifanyaje wakati daily kwa kazi. Nafanya mazoezi ya tumbo, naruka kamba, na mazoe mengine lakini naona sijapungua hata kilo moja. Chakula gani nile kuanzia asubuhi mpaka jioni?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Safiri na Zawadi