Wednesday diet

Asubuhi

Maji nusu lita baada tu ya kutoka kitandani.

Tembea kwa dk 45. Kama asubuhi si muda mzuri kwako chagua muda wako mwingine.

Smoothie ya ovacado na passion fruit glass moja kubwa ila isiwe kubwa sana.

Mchana

Nyama choma yoyote utakayo pamoja na salad ya kutosha unaweza changanya ya aina yoyote ile isiwe na carrot. Kiwango cha salad unaweza kula kiasi chochote unachoweza wewe ila jitahidi isiwe kidogo. Dressing chukua kijiko cha olive oil changanya na nusu ndimu.

Kabla ya saa kumi na moja

Tunda lolote unalotaka kiasi kidogo kinachotosha pamoja na kiganja cha korosho au karanga au nuts ya aina yoyote unayotaka, mi napendelea almonds.

Kumbuka

Usisahau kunywa maji lita 2, mpaka ifikapo muda wa kwenda kulala. Pia usisahau kutembea au kufanya mazoezi yoyote angalau kwa saa moja au zaidi. Lala masaa 8 kila siku, jaribu kwenda kulala mapema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Safiri na Zawadi