Category Archives: Mexico

Our Honeymoon Sydney, Los Angeles, Hollywood, California, Phoenix, Utah, Arizona, Las Vegas, Mexico City, Cancun, Tulum, Miami Florida, Bahamas, Grand Cayman, Montego Bay Jamaica and Cozumel Mexico.

Happy Valentine’s Day People Cheers!!!!

Our honeymoon 2004 full of beautiful memories with wonderful feelings. Very Interesting and amazing places wow! love it! :)))))

 

 

Cancun Mexico 2004

With hubby in Carlos & Charles Restaurant

 

What an amazing place, wow! Hii holiday ni part ya our 2 months honeymoon. Kufika hapa tumetokea  Mexico City. Cancun ni one of my favourite place in the world, I love this place too much. wakati tukiwa on the way to our hotel tulikatiza hotel nyingi sana ambazo nyingi ziko pembezoni mwa bahari, ukiangalia zote ni nzuri sana panapendeza kwa kweli. Sisi tulifikia Intercontinental Hotel Cancun ambayo nayo ni nzuri sana.

Ilikuwa ni kipindi cha summer kulikua na watu wengi sana. Cancun ni holiday destination ya watu wengi wanaoishi US. Kitu unachoona kwanza ukiingia tu hapa ni kiasi gani watu wana furahi maisha kuanzia wanaokatiza barabara mapaka waliokaa pembeni, unachoweza ona usoni kwao ni furaha ya holiday. Party everywhere ukiwa Cancun. Kitu kingine kilichonifurahisha ni kuona watu wanakatiza tu barabarani huku wamevaa nguo zao za kuogelea na kushika mataulo mikononi huku wakiwa peku peku, panatia raha sana.

Usiku sasa ndio kunawaka moto kuna night club nyingi sana. Kwa wale wasiopenda club sana kama mimi pia hamkuachwa nyuma karibu kila restaurant ilikua na viburudisho vyake. Kila uendapo kulikua kuna kukuhakishia good time, kazi ilikua kwako tu. Kwenye night club kulikua na foleni kubwa ya kuingia ndani unaweza shangaa watu wote hao wanatokea wapi lakini hiyo ndio Cancun in summer. Tumepapenda sana hapa kila dk tuliyotumia hapa ilikua ya furaha kubwa.

Nilifurahishwa sana na Carlos & Charles Restaurant in Cancun nadhani ndio my favourite. Kuanzia huduma yao ilikua hiko fast na wahudumu wake walikua much fun. Hapo sijaongelea msosi ambao ulikua uko super. Karibu kila siku nikiwa Cancun lazima nije hapa kula. Pia nilifurahi kuona my favourite Rainforest Cafe in Cancun. Mara yangu ya kwanza kula hapa ilikua ni Los Angelous moja kwa moja nikapenda sana chakula chao kizuri.

OMG! The beaches is to die for. The ocean has such amazing colour and the sand so white. Maji masafi sana na beach ziko so clean. Ukiangalia kwenye bahari unaweza kudhani maji yana rangi tatu ya kwanza ni light blue, blue & dark blue just amazing. Nadhani watu wengi pia wanakuja kwa ajili ya hizi beach maana ni nzuri sana. Pia bila kusahau mji wenyewe ulivyochangamka watu wanajua kuparty bwana.

Pia tulipata nafasi ya kwenda Tulum kutembelea  Chichen Itza Pyramid. Tulifikia Club Med Villas Chichen Itza ambayo ilikua nzuri pia. Kufika huko tulitumia njia ya barabara tulidrive wenyewe na gari ya kukodi. Tulichelewa kufika na kuamua kulala kesho yake ndio tulielekea kwenye Pyramid ilikua ni walking distance. Kama kawaida yangu napenda sana historia hasa mambo ya kale sana. Chichen Itza Pyramid inasemekana ilijengwa na watu wa Maya ambao wanasemekana ni watu wa siku nyingi sana huko. Karibu na pyramid kulikua na underground river ambapo kisima chake kinasemekana kilikua kinatumika kama sehemu ya human sacrifice to their god, mmh..sad.

Tulivyomaliza kushangaa shangaa tulianza safari yetu ya kurudi Cancun ila kutokana na kuchelewa kutoka Chichen Itza tuliamua kutafuata hotel Tulum na kulala then kesho yake tuanze safari ya kurudi Cancun. Tulipata Los Lirios Cabanas Hotel ambayo nayo ilikua nzuri iko pembeni ya bahari na ina beach nzuri san. Kesho yake tulianza safari yatu ya kuelekea Cancun njiani nakumbuka tuliamua kusimama na kupata lunch nilioda Classic Nachos ila sikuzipenda sana. Kwa kipindi nikiwa Mexico niligundua kua real Mexican food ndani ya Mexico akinogi sana kama unapokula Mexican food nje ya Mexico. Siri yake nikagundua kuwa most of Mexican food outside Mexico ni American Mexican food wanaweka vikorombwezo vyao vinavyofanya kinoge haswa. Maana kipindi hicho chote nikiwa huko kila nikiagiza Mexican food nakua sijakipenda sijui ni mimi tu au la.

Kwa ujumla naweza kusema, what an experience, love this place, for sure lazima turudi tena Cancun is one of my favourite place in the world.

 

Mexico City, Mexico 2004

The view from the Pyramid of the Sun

 

Holiday hii ilikua part ya our 2months honeymoon. Tulifika hapa tukitokea Las Vegas ambapo ndio tulipanda ndege yetu ya kuja hapa. Tulikuja mji huu kwa ajili ya kwenda kutembelea Teotihuacan Pyramids. Tulikua na siku 2 tu hapa Mexico City ambapo siku ya kwanza tuliitumia kuuzunguka mji na siku ya pili tuliimalizia kwenye pyramids.

Siku ya pili ilivyofika tulianzia moja kwa moja kuelekea kwenye pyramids ambapo kuna umbali kama kilometres 40. Tunaambiwa Teotihuacan Pyramids zimekuwepo about 2,000yrs ago. Pia inasemekana kuwa huu mji ulikua ni kati ya miji mikubwa duniani enzi hizo, ilikua na watu kama 200,000.

Tulivyofika tulishangaa kuona the beauty of this place yaani ilikua inapendeza sana. Ukikaa na kufikiria watu miaka hiyo waliwezaje jenga sehemu nzuri na kubwa kama hii bila kuwa na urahisi wa vitendea kazi. It’s real amazing.

Tulivyokua kwenye pyramids wacha kazi itupate ya kupanda hizo ngazi ilikua shughuli kweli, watu wengine walikua wanapanda kwa matako ilikua inachekesha kweli. Ngazi zilikua nyingi sana na zilikua zinaenda juu kwa kasi ilibidi wakati mwingine ushikirie kamba ambayo imewekwa kwa ajili hiyo la sivyo unaweza kupata kizungu zungu na kudondoka. Uzuri unakuja pale ukishafika juu, view unayokumbana nayo ni ya hatari, panafurahisha kwa kweli. Unaanza kujiuliza ni jinsi gani hawa watu waliweza kupima na kuweka kitu cha namna hii, it’s amazing.

Baada ya kuzunguka na kutosheka tulienda kula lunch kwenye hotel ya karibu kwa bahati nzuri siku hiyo na Traditional Mexican dancing ilikua poa sana kuona hiyo show wanasema dancing ya namna hii imeanzwa kuchezwa tangu enzi hizo za Pyramids.