Our Honeymoon, 2004

The formal night party on board the ship

Love my honeymoon, my hubby alichukua my dream na kuifanya ikawa reality. Honeymoon yetu ilikua karibu 2months ndani yake kila siku ilikua ni siku ya furaha kubwa kwangu. Honeymoon yetu ilikua in USA, Mexico and Caribbean Islands. Tulianzia Los Angelous ambapo tulikatiza International Date Line tulisafiri the same day tukitokea Sydney na kufika Los Angelous America the same day amazing. Tukiwa USA tuliweza tembelea kama 5 states California, Arizona, Utah, Nevada & Florida. Tukiwa Mexico tuliweza tembelea Mexico City, Cancun & Conzumel. Tuliweza tembelea sehemu nyingi na kuona mengi, Hollywood, Universal Studio, Disneyland, Grand Canyon, Meteor Crater, Las Vegas and Everglade kuona Alligator. In Mexico tulitembelea Teotihuacan Pyramids & Chichen Itza Pyramid in Tulum.

Tukiwa Florida nilidhani ndio holiday yetu imeisha kumbe kuna ya mwisho hiyo ambayo ni kali haswa. Nilichoambiwa ni funga mizigo tunaondoka naona tunaelekea port badala ya Airport, tulielekea Fort Lauderdale na kukumbana na Cruise Ship nyingi zimepark. Moyo ukanipasuka maana nakumbuka our 1st date aliniuliza what’s my dream wacha nijieleze so far honeymoon yote imetoka uko. Moja ya dream kubwa kwangu ilikua kusafiri kwenye Ship kubwa kama Titanic, siku ya kwanza nilivyoona movie hii nikawa na wish one day nami niwe katika maisha yaliyokua ndani ya meli ukitoa ajali hahaaaa…

Welcome aboard pic

Mbele yangu ilikua imesimama dream yangu wow! Ilikua ni CARIBBEAN PRINCESS CRUISE moja ya meli kubwa ambayo inachukua karibu watu 3000 hivi. Tulikaribishwa kwa kupiga picha ya kumbukumbu ambapo abiria wote lazima wafanye hivyo. Tulivyoingia ndani wacha macho yanitoke niliona kama vile niko ndotoni lakini ilikua si ndoto, nashindwa hata kujieleza jinsi gani nilijisikia nachoweza sema nilikua na furaha kupita kiasi. Safari yetu itachukua siku 7 kuelekea Princess Cays Bahamas, Montego Bay, Grand Cayman and Conzumel. Tulipelekwa moja kwa moja kwenye chumba chetu ambapo kitakuwa ndio nyumbani kwetu for 7days amazing.

Our room Riviera 707 Deck 14
At Fort Laurderdale on our balcony

Tulikua Riviera Deck 14 room 707 tulikua juu sana meli ina deck 16, the view ilikua amazing. Room ilikua nzuri na kubwa sikutegemea kulikua na double bed, tv, sofa, fridge, wardrobe, bathroom na tulikua na balcony. Room ilikua na mtu special ambaye kazi yake ni kuhudumia wakati wowote nadhani wana vyumba kadhaa na walikua wanafanya kazi nzuri sana maana ukitoka tu kidogo unakuta chumba kimesafishwa na kupangwa vizuri sana hata kukunja nguo na kupanga kabatini, Kazi hii iliendelea siku zote tulipokua onboard.

On board Princess Cruise
On board Princess Cruise Ship

Ndani ya meli kuna mambo mengi yanayoendelea ukiwa ni mtu wa kuparty basi utapati mpaka asubuhi kuna ukumbi mwingine hawafungi mpaka asubuhi. Pia kulikua na intertainment nyingi sana kuanzia swimming pool ambazo zilikua kama tatu ikiwepo moja kubwa sana, usiku mmoja walitumia kama movie theater ambapo tuliangalia movie under star katikati ya bahari with blacket and popcon so romantic. Chakula ndio kilikua chenyewe jamani nilikula kupita kiasi na kilikua kitamu sana nilivyotoka baada ya hizo siku saba nilikua nimeongezeka sana maa chakula ni 24/7 ukisikia njaa muda wowote wewe kimbilia restaurant na ukizingatia ni bure kabisa. Kulikua na restaurant kama 7 hivi kama nakumbuka vizuri 2 zilikua ni buffet hizo ndizo zilikua na chakula muda wowote wakifunga hii wanafungua nyingine basi kazi tu. Pia kulikua na nyingine ambazo zilikua more traditional dinner setting ambako ulikua unatakiwa kulipa uko, kuna moja ilikua ina serve mpaka serve 7 course meal. Vinjwaji ulikua unalipia ukitoa soda.

Smart Casual Night Party
Formal Night Party

Tukiwa katikati ya sea kulikua na party ambapo usiku mmoja ulikua special kwa Casual Night Party na mwingine ulikua ni Formal Night Party ambapo kila mtu kwenye meli lazima avae according kama huna unaweza kuazima kwenye boutique iliyopo melini. siku ya Formal ilikua muhimu sana lazima kila mtu auwashe kisawa sawa mpaka watoto kama huna na utaki usijitokeze katikati ya meli ilikua wonderful kwa kweli unajihisi kama vile super star vile. Siku hiyo kila mtu ni star kwa nafasi yake huko unapata kinywaji champain ambayo inapitishwa na wahudumu waliovalia maridadi kabisa huku tukiwa tunapigwa picha kama vile tupo red carpet vile. Kwenye formal lazima wanaume wote wavae suti utake usitake ilikua ni kitu kingine kwa kweli mi nilipenda sana nilisahau kama vile nimetokea kwenye shida wakati huo.

Behind me is our cruise ship in Bahamas
Our cruise ship in Bahamas
Cayman Island, Stingrays Fish

Siku ya kwanza tulitia nanga Bahamas, iliyofuata tulitia nanga Cayman Island na kupata siku nzima ya kuzunguka mji au kwenda tour yoyote unayotaka nyingi zilikua zinaandaliwa melini si tuliamua kwenda kuswim kwenye sand bar na stingrays fish. Kulikua ni katikati ya bahari upande wote ni maji yenye kina kirefu sana then unakutana na sehemu hii ambapo ukisimama maji yanakufikia magotini na ukienda kidogo mbele unakutana na kina kirefu sana ilikua amazing.

Montego Bay Jamaica

Montego bay, Jamaica tuliamua kwenda city tour kufanya some shopping then tulienda Horse riding. Nakumbuka wakati tunaelekea mjini tulimchukua taxi driver mmoja alikua anaongea utafikiri anaimba inapendeza kwa kweli. Kwenye horse riding mjamaica alifurahi kuona mtu ametokea Africa ukilinganisha katika kundi lote ni mimi tu mwenye ngozi nyeusi na yeye basi aliniuliza maswali mengi sana na kuanza kulaumu utumwa ulioenda kuwaacha kwenye land ambayo hata nyoka hakuna eti anatamani kurudi kwenye land yenye simba na kadhalika angejua kuna watu ambao wanakimbia hiyo Africa anayoitaka yeye, anaonyesha ni mtu mzuri sana.

Conzumel Mexico, on my left is our ship The Caribbean Princess
Conzumel Mexico

Tulivyofika Conzumel Mexico tuliaenda city tour pia kufanya kishopping kidogo. Nilishangaa sana muda wote ambao tulikua kwenye visiwa hivi watu wanathamini sana jiwe la Tanzanite maana kote wanaitangaza sana. Pia bei yake ilikua kubwa na watu wanaipenda na kuinunua kwa wingi hapo ndipo nikafungua macho kuhusu Tanzanite maana enzi hizo wakati nilikuwa Tanzania nilikua naisikia tu kwa mara ya kwanza kuiona nimeiona kwenye visiwa vya Caribbean aibu kwa kweli eti nami najidai nimetoka Tanzania. Kitu cha kwanza nilipopata nafasi ya kurudi home nilienda madukani na kuanza kuifuatilia na kuuliza maswali mengi kuhusu jiwe ili. Conzumel ndio ilikua stop yetu ya mwisho kabla ya kuanza sail back to Fort Laurderdale Florida US.

On board Conzumel Mexico
Our last day on board, nimeongeza kilo chakula kilikua si mchezo
Our last night on board

Safari yetu ilifikia kikomo usiku wa kuamkia our last destination ndipo wanapoleta bill zote kwa ajili ya malipo maana muda wote tukiwa onboard utakiwi kulipia kitu chochote na pesa unachofanya unalipia kwa card ambayo ni ufunguo wako wa room yako. Sasa hiyo kasheshe ya bill ndipo watu wanapochoka kuona pesa ngapi wamespend ndani ya meli ni balaa maana ndani ya meli kuna kila kitu kuanzia vinywaji vya kukata na shoka kwa wale wanaopenda cocktail maana hapa ndio kwenyewe na wale wanaopenda boutique kama mimi, kulikua na maduka ya jewels za kila aina na zenye thamani kubwa sana sasa walioamua kushop kama hawana akili nzuri siku ya mwisho bill inavyokuja unalia.

Flamingo garden, Florida
Flamingo Garden, Florida

Tulivyotia nanga tuliamua kwenda tour Everglade kutizama Alligator ilikua so much fun kuzunguka na flying boat. Jioni ilivyofika tulienda zetu Airport na kuelekea Los Angelous Airport ready to board our flight back to down under Sydney. Baada ya this experience kwa kweli nilitua manyanga na nikawa sina mchachato wa iana yoyote nikaona kuwa kila kitu kwenye hii dunia kinawezekana usiwe na papara muombe mungu atakusaidia na pigania maisha yako usikate tamaa.

The formal night party on board the ship

Thanks hubby that was the best honeymoon any bride could ask. Was Awesome! love u big xox

 

2 thoughts on “Our Honeymoon, 2004”

Leave a Reply to KENNETH kOLOWA Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Safiri na Zawadi