Tag Archives: kama

Summer Holiday 2014-Day 6-Aonang Krabi, Thailand

DSCN8088

Baada ya kuwa Railay kwa siku tatu tuliondoka kwa njia ya boat kuelekea upande mwingine wa Krabi ambapo tulikaa usiku mmoja. Safari ya boat fupi sana ukilinganisha kama tungechukua boat kurudi Krabi town. Ilikua ni public transport so tulivyofika upande wa pili ilitakiwa tushuke na kubeba masaduku yetu wenyewe, sasa fikiria mama wa kiafrika tunavyojua kusafiri na vitu vingi wacha niangaike lol! Cha kuchekesha zaidi upande huo ulikua hauna taxi so ilibidi tuchukue usafiri wa pikipiki yenye miguu mitatu na masanduku yetu yalivyo makubwa si kubanana uko ilibidi tubebanane na mmoja kukaa juu ya sanduku huku mimi ilibidi nimbebe baba Amika ni vituko lakini tulifanikiwa kufika hotelini ambapo hapakuwa mbali ni kama dk 5 tu tatizo sehemu hii iko busy sana. Njiani tukawa kama kiburudisho cha watalii maana watu walikua wanashangaa tuliwezaje kutosha wote kwenye hiki kipikipike. Watoto wacha wafurahi maana familia hii kwa kupenda adventure :-) Now this is what we call an adventure!!!

 

Summer Holiday 2014-Day 4-Krabi, Thailand

Siku yetu ya nne tuliamkia bado Railay Krabi na tuliamua kuitumia kwa kushinda beach. Kama nilivyosema mwanzo beach hii imeshakua one of the best beach in the world. Kama inavyoonekana kwenye picha inapenda sana tena sana. Kitu kingine kinachofurahisha kwenye beach hii unaweza kukaa ukarelax na kupata massage toka kwa local people ambao unalipia pesa kidogo tu :-) Ila uwe tayari kukubaliana na michanga Lol! Amani na Malaika ni wapenzi sana wa beach msipo angalia wanaweza kuwakalisha huko siku nzima hawachoki kabisa, wanapenda sana maji.

Family at Alila Resort, Oman-Weekend getaway 2014

Mr. Amani
Mr. Amani

Maji ya pool yalikua baridi ila kama unavyoona watoto hawataki toka kwenye maji mpaka giza linaingia kama inavyoonekana kwenye picha lol!

Dinner at Al Mahala Restaurant, Burj Al Arab hotel Dubai 2014

With hubby
With hubby

Our anniversary dinner tulikula hapa na kusema ukweli ni pazuri sana. Kama wanavyosema wenyewe ni 7 Star hotel ambapo iko pekee duniani sijui ni kweli au la, ila nachoweza sema sijaona hotel kama hii na huduma yao ni super. Restaurant ikiwa imezungukwa na aquarium kubwa yenye samaki wa kila aina inapendeza sana. Tuliweza kumuona Mr. George ambaye amekuwepo hapa toka hoteli ilivyofunguliwa. By the way Mr. George ni samaki lol! Ukiangalia kwenye picha yuko mkubwa hivi ambae ana sura ya tofauti. Baada ya dinner walitupa another cake ya kutuwish ikiwa ni cake ya pili toka tuwasili kwenye hii hotel and was supper yummy :)

 

Family at Bimah Sinkhole, near Tiwi, Oman 2013

 

mama Amika
mama Amika

Haya maji ni ya chemchem uwezi amini yapo jangwani. Pia ina ruhusiwa kuogelea kama ukitaka ila kipindi hiki kulikua ni baridi sana ni wakati wa winter so hatukuweza kuogelea.