Tag Archives: krabi

Family Holiday Krabi, Thailand. 2010

At Sunrise resort Krabi with my kids

 

Siamini mara ya kwanza nilikuaja hapa miaka saba iliyopita, hii ni mara yangu ya nne. Kitu cha kuchekesha na kizuri ni kwamba kila tukirudi wanatupa the same room ambayo tulikaa 2003 how sweet. Sunrise Resort and Railay never disappointed us and again we had an awasome time. No adventure this time just relax and enjoy until next time cheers!!!!

Family Holiday Krabi, Thailand. 2009

My baby Malaika at Railay beach

 

We love Railay Krabi, tunazidi kurudi hapa karibu kila mwaka, mambo yanabadilika kwa kasi sana. Maendeleo yanaongezeka mara ya kwanza tulipokuja 2003 kulikua na hoteli chache sana, sasa hivi zimeongezeka maradufu na kufanya kuwepo na choice nyingi ya wapi upate lunch au dinner.

Kitu ambacho bado hakijabadilika ni ukarimu wa watu  nadhani ndio sababu kubwa ambayo inatufanya tuendelee kurudi. Ni sehemu ya kila mtu uwe single, couple au ukiwa na watoto kila mtu atafurahia holiday yake.Sisi bado tunafikia the same hotel kila mara tukiwa Railay Krabi Sunrise Hotel kwa kweli hatuna cha kucomplain kabisa kuhusu hotel hii. Huduma zao ni nzuri sana na wafanyakazi wake ni wakarimu kweli pia bei yao ni ya kuridhisha.

 

 

The Family Krabi, Thailand. 2007

Amani with his brother & sisters

 

This year sikuweza kwenda holiday nilikua niko hoi na ujauzito wa Malaika. Amani and daddy walienda peke yao bila mimi. Huko Thailand walijumuika na our family iliyokua imetokea Australia. My Amani alikua ana mwaka na miezi mitano tu, ila kwa sababu ameshazoea kusafiri hakusumbua kabisa.

Krabi Thailand, 2003

Panapendeza kwa kweli 2003

 

 

Mara yetu ya kwanza kwenda Krabi ilikua ni 2003, moja kwa moja tuka fall in love with this place. Tulifikia Sunrise Resort Hotel kwa kweli hatuna cha kulalamika kabisa huduma zilikua nzuri sana na wafanyakazi wake ni wanaupendo kweli. Hatukukaa sana kama nakumbuka vizuri tulikaa kama siku nne hivi na tuliahidi kuwa tutarudi na tumefanya hivyo karibu kila mwaka.

Hizi ni baadhi za picha tulizopiga mwaka huo 2003 nadhani utaendelea kuziona picha za Krabi mara mara kwenye MaiSafari. Picha hazionekani vizuri sana nimefanya kuscan.