Six Senses Resort & Spa, Zighy Bay Oman

Zighy Bay Six Senses Resort & Spa Hotel

 

What an experience! Kulala hapa kwa usiku mmoja inaanzia dola 1,000 na kuendelea. Zighy Bay ambayo ni Six Senses Resort & Spa Hotels iko Musandam, Oman. Kufika kwetu hapa ilituchukua karibu 7hrs tukitokea Muscat baada ya kukatiza boarder mbili za UAE. Eneo hili liko chini ya Oman ila likiwa limezungukwa na UAE pande zote so ukitaka kufika hapa lazima ukatize Fujairah or Sharjah. Ila ukitokea Dubai Airport ni masaa mawili tu. Bahati barabara ni nzuri sana kwenye nchi zote hizi mbili ni kipengele kidogo tu ambacho ni cha kuvuka milima mkubwa ndipo uweze kuingia Zighy Bay ambapo lazima uwe na 4WD ila kama huna kuna sehemu unapaki gari lako na hotel inakuja kukufuata.

Tulivyowasili tu tulipokelewa kwa ukarimu wa hali ya juu yaani wafanyakazi wote ni wakarimu sana pia kuna amani ya aina fulani unapata pindi tu ukiwasili hapa ni ya ajabu sana. Resort imejengwa kwa staili ya kizamani ya watu wa Oman ambapo villa zote zimejengwa kwa mawe huku wakichanganya na modern style kama vile private pool, etc.

The resort kwa ujumla ni very expensive kila kitu ukigusa ni pesa tu. Ila cha kushangaza ukiangalia jinsi hoteli ilivyojaa utadhani ni pesa ndogo tu kumbe bila usd 1,000 na kuendelea ujalala hapa. Ilikua bahati kweli kwetu maana our 2nights zilikua ni za bure tulishinda, tulichotakiwa kulipa ni chakula na mambo mengine tukitaka. Pia tulipewa 25% ya kila kitu lakini hata hivyo mambo yalikua expensive sana uwezi amini kwa hizo siku mbili pesa tuliyolipa inasikitisha. Wakati hapo kuna watu wako na familia nzima mpaka watoto ambapo ukipiga mahesabu mtoto mmoja si chini la dola 300 kwa siku bado chakula na mambo mengine, jamani kuna watu wana hela.

Huduma yake ilikua iko kwenye standard ya juu sana kila villa ilikua na mhudumu special ambaye yuko 24hrs kwa ajili yenu ukitaka chochote we piga simu tu dk chache tayari kafika. Chumba kinasafishwa karibu kila wakati mkitoka tu mtu keshafika na kusafisha mkirudi kunanukia acha tu, kweli hii ni 1st class service.

Wacha nami nijidai kama vile nina hela vile hahahaaa… maana watu waliopo hapa ni wenye pesa zao nami nikaonekana kuwa nami ninazo wangejua Lol! Ilikua ni experience mpya kwangu kuzungukwa na watu wa pesa tu wanavyozitumia utafikiri hakuna shida kabisa. Hii kwangu ilikua ni mpya ingawa nimeshazunguka sehemu mbali mbali na yenye watu wa aina tofauti ila hapa kwangu ilikua ni kali maana ni watu wa aina moja tu wenye pesa na si vinginevyo hata atmosphere yake ilikua tofauti kabisa. Si nisijifanye naangalia bei za spa mbona nilifunga kitabu haraka sana maana hizo bei weweeeee…yalinishinda. Nikiwa ni mpenzi wa spa na Six Senses Resort ni maarufu sana kwa spa nikasema ngoja nami nijitahidi mbona yalinishinda maana dah! zina wenyewe labda siku moja nitajaribu lakini si sasa.

Pamoja kuwa tulienjoy na kufurahia amani iliyopo hapa na sehemu yenyewe ila kama ingekuwa kulipa sidhani kama tungelipa pesa zote hizi kwa ajili ya kukaa hapa, tunaamini kuna sehemu nyingi ambazo ni nzuri zaidi ya hapa ambapo unaweza kukaa kwa bei rahisi zaidi. Ila tulifurahia kupata another new experience ingawa zilitutoka kidogo hasa kwenye dinner.

Kitu ambacho kikubwa nime notice hapa ni amani, kwa kweli ukiwa na stress au umechoka unahitaji mapumziko hapa ni mahali pake kuna amani ya ajabu sana. Ufikapo tu hapa moja kwa moja unaanza kujihisi tofauti kwa hilo nawapa hongera zao sana. I’m happy nilikwenda maana nimepata experience nyingine ambayo naweza kuadd kwenye my travel experience. Naweza sema was very interesting. Cheers!!!!