Life in Oman

Grand Hyatt Hotel Muscat

 

Maisha ya Muscat, Oman kwa ujumla ni mazuri, kitu kikubwa kilichopo hapa ni amani iliyopo ni nzuri sana. Kitu cha kushangaza baada ya kufika hapa mwaka mmoja ukazaa wa pili, watatu na bado tupo. Mimi huwa napenda kuishi sehemu ambazo zimetulia sana kama vile nje ya miji, huwa sipendi kukaa sehemu ambazo ziko busy sana, kwa namna hiyo hapa nimefika maana kumetulia sana. Ila kwa wale ambao wanapenda sana kutoka mara kwa mara hapa wanaweza kidogo kuchoka ila kwa wale kama sisi ambao tunapenda sehemu iliyotulia nadhani hapa ndio penyewe.  Hakuna wizi hapa hata kama ukilala mlango wazi, utashangaa ukiamka unakuta kila kitu kiko vile vile. Nimetokea kukupenda zaidi  baada ya kupata watoto ni sehemu nzuri kwa kulea, ukiangalia kama nchi nyingi kila wakati unakua na wasiwasi na usalama wa watoto wako. Pia bila kusahau wenyeji wa hapa ni watu wazuri kuna tofauti kubwa na nchi nyingine za ukanda huu. Kama wataendelea kutupa kazi nadhani tutaendelea kuwepo hapa kwa muda…