You can’t believe this is Tanzania, yes ni Lushoto hiyo. Hii waterfall utaiona kwa mbali ukishaanza ingia tu kwenye mji wa Lushoto, sisi tuliamua kupatembelea siku yetu ya mwisho ambayo tulikua ndio tumeanza safari yetu ya kurudi Bongo. Kinachosikitisha ni kwamba eneo hili ni nzuri sana ila sijui serikali imelisahau maana wangepatengeneza vizuri na kuvutia watalii wengi tu na kuweza kuongezea kipato. Kwenye sehemu ya kuingilia eneo hili ambapo ndio unalipia shs. 2,000 kuweza kutelemka chini hali yake ni mbaya sana nilijaribu kwenda chooni kujisaidia mbona niliishia mlango ni pachafu ujawahi kuona. Inaonyesha ilikua ni hotel zamani sasa hivi pamekua kama gofu tu na linatumika kama vile sehemu ya kufundishia au sijui nini. Jamani eneo hili ni zuri sana kama wangeweza kujenga hotel nzuri tu au restaurant nzuri wangewavutia watalii wengi sana. Nikilinganisha na nchi nyingine nyingi ambazo nimepitia, kuna tofauti kubwa sana maana wenzetu wametupita sana na maswala ya utalii. Huku tukiwa na sehemu nzuri na nyingi ambazo zinavutia, nchi yetu inatakiwa kuamka na kuendeleza sehemu kama hizi na kukuza sekta hii ya utalii maana hakika nchi yetu ni nzuri na ya kuvutia.
Next day tuliamua kufanya tour kidogo around Lushoto na kujionea uzuri wa wilaya hii kunapendeza sana. Tulipata nafasi ya kutembelea Lushoto view hotel ambayo iko sehemu nzuri ila nilisikitika jinsi walivyoijenga na kuziba view ambayo ndio ingependezesha sana eneo hilo ambayo ni ya aina yake. Walitakiwa kuacha eneo kubwa wazi hata mtu akikaa restaurant aweze kuenjoy beautiful view lakini ukiwa ndani uwezi ona chochote kutokana na ujenzi walioufanya. Nilifurahia uamazi niliyofanya wa sisi kukaa Swiss Farm cottage ambapo kuna character ya aina yake ya kipekee ambapo kwangu mimi ni sifa kubwa sana kwa kuifanya sehemu kuwa nzuri zaidi.
Raha nyingine ya hii sehemu ni kuamka asubuhi na kufurahia sunrise ambayo inashine kwenye maua yenye unyevu unyevu uliotokana na baridi ya usiku ambapo ni baridi sana. Kama unavyoona picha ambazo nilipiga, asubuhi kunapendeza sana, I love this place kwa kweli. Nawashauri wanaokaa mijini ukitaka kupumzisha kichwa jaribu kwenda sehemu kama hizi ambapo utatuliza kichwa na utaenjoy ukimya na uzuri wake, huku ukijisoema vitabu. I love life like this ni za kipekee :))))))))