Nilifurahi sana kukutana na marafiki zangu wapya Jessie & Irene ambao tumekua tunawasiliana muda mrefu atimae tulipata nafasi ya kukutana uso kwa uso nilifurahije sasa, asante sana lovely ladies. Pia nafurahi kupata muda angalau kukaa na wadogo zangu Celine, Tina, Scolar, Flora. Asanteni kwa muda wenu mlionipa pamoja na vicheko tulivyocheka…hahahaaa…mnakumbuka dada wa reverse pale kivukoni? lol! yaani hapa nacheka kweli bongo darisalama panapendenza lol. Uncle Festo asante sana kwa kuja kukutana nami yaani nilifurahije sasa uncle wangu, asante kwa kila kitu :)
Siku saba si nyingi kwa kweli kwa bongo yaani nilitamani niendelee kukaa zaidi kweli nyumbani ni nyumbani huwa siichoki Dar es Salaam yetu. Celine Victor mdogo wangu karibu sana maisafari <3 :)
Jamani nyumbani ni nyumbani kwa kweli, kila mara nikijikuta napanda ndege ya kuelekea Dar nakua na furaha ya ajabu. Nashukuru sana kukutana na rafiki yangu Jessie pamoja na mrembo wake Sasha ambao nao walikua Bongo kwa ajili ya holiday pia kukutana na mrembo wangu mwingine Thanya, nilifurahije sasa :)
Bila kusahau wadogo zangu Scola, Christina na Flora asanteni sana kwa kunitafuta ingawa muda niliokua nao ulikua ni mdogo sana lakini nilifurahi sana. Nawapenda sana wadogo zangu, xoxo. Scola karibu sana Maisafari lol!