Our around the world trip Nov-Dec, 2013-Venice, Italy-Day 1

 

With my baby girl
Nikiwa na binti yangu Malaika nje ya hoteli tuliyofikia, tayari kwa kuingia mtaani

 

Tuliwasili Venice Italy salama kwenye mji uliyojengwa juu ya maji kama unavyoitwa na watu wengi. Baada ya kucheck in kwa hotel tukaingia mitaani nasi kujumuika na watalii wenzetu kushangaa lol! Tulikua na bahati siku hii hali ya hewa ilikua nzuri jua lilikua linawaka vizuri na kufanya watalii kuwa wengi sana mitaani. Sasa sio kupigana vikumbo uko utafikiri tulikua sokoni lakini kwa jinsi mji ulivyo mzuri kila mtu alikua anaonekana na furaha. Venice ni moja kati miji mashuhuri duniani wenye historia kubwa.

 

DSCN3574
Nikiwa na familia yangu

 

DSCN3576
Venice, Italy

 

20131101_144639_5_bestshot
Venice, Italy

 

20131101_141249_3_bestshot
Pizza za hapa ni kiboko

 

P1050523
Pizza time with my family

 

DSCN3589
Mjini Venice, Italy with my kids Amani and Malaika

 

DSCN3593
Mama Amika mwenyewe ndani ya Venice, Italy

 

Mara yangu ya kwanza kuja kwenye mji huu ilikua ni 2002 wacha mtanzania mimi nishangae maana kila kitu nikiangalia kwangu kilikua ni kigeni lol! Unaweza angalia kwenye post ya VENICE, ITALY 2002 kwenye post za nyuma. Nakumbuka vizuri jinsi nilivyoupenda mji huu nikasema lazima nirudi tena, furaha iliyoje nimeweza rudi tena ingawa imechukua miaka kumi lol! Ningependa kurudi tena ila safari hii nataka iwe summer maana vipindi vyote hivi viwili tumekuja wakati wa winter, inasemekana summer kunapendeza zaidi ila kwa wale wasiopenda kubanana summer si nzuri kwao inasemekana watalii wanakua wengi sana kulinganisha na kipindi cha winter. Tutakuwepo hapa kwa siku mbili then tunachukua cruise ship kutokea hapa Venice to Miami Florida, yaani tunasubiri kwa hamu kweli kukatiza Atlantic ocean to America kama Titanic vileĀ  :)