Hii ni Christmas yangu ya tatu kusheherekea nikiwa mama and I love it. Inafurahisha sana kuona watoto wakifurahia kila kitu kuhusu hii holiday kuanzia Christmas tree, songs bila kusahau zawadi toka kwa santa hahahaaa…. Niliamua pia kuanzia utamaduni wangu wa kupiga picha ya familia siku ya Christmas day, huu inakuwa utamaduni wetu wa pili katika kipindi hiki cha holiday ambapo wa kwanza huwa tunaufanya kila tarehe 1 December kwa kusheherekea kwa kupamba mti wetu wa Christmas. Utamaduni huu nimeukuta kwenye familia ya mume wangu ambapo aliuanzisha. Ni utamaduni mzuri unatupa nafasi nzuri ya kuenjoy mti wetu wa Xmas kwa muda mrefu mpaka ifikapo 1st Jan.
This day tunasheherekea kwa kuanza kupamba mti wetu wa Xmas huku tukisikiliza nyimbo za Xmas. Pia kwenye mwezi huu huwa tunaangalia home movie videos, kusoma vitabu, pamoja na kuangalia movie zinazohusu holiday hii kwa kweli inapendeza sana.