You can’t believe this is Tanzania, yes ni Lushoto hiyo. Hii waterfall utaiona kwa mbali ukishaanza ingia tu kwenye mji wa Lushoto, sisi tuliamua kupatembelea siku yetu ya mwisho ambayo tulikua ndio tumeanza safari yetu ya kurudi Bongo. Kinachosikitisha ni kwamba eneo hili ni nzuri sana ila sijui serikali imelisahau maana wangepatengeneza vizuri na kuvutia watalii wengi tu na kuweza kuongezea kipato. Kwenye sehemu ya kuingilia eneo hili ambapo ndio unalipia shs. 2,000 kuweza kutelemka chini hali yake ni mbaya sana nilijaribu kwenda chooni kujisaidia mbona niliishia mlango ni pachafu ujawahi kuona. Inaonyesha ilikua ni hotel zamani sasa hivi pamekua kama gofu tu na linatumika kama vile sehemu ya kufundishia au sijui nini. Jamani eneo hili ni zuri sana kama wangeweza kujenga hotel nzuri tu au restaurant nzuri wangewavutia watalii wengi sana. Nikilinganisha na nchi nyingine nyingi ambazo nimepitia, kuna tofauti kubwa sana maana wenzetu wametupita sana na maswala ya utalii. Huku tukiwa na sehemu nzuri na nyingi ambazo zinavutia, nchi yetu inatakiwa kuamka na kuendeleza sehemu kama hizi na kukuza sekta hii ya utalii maana hakika nchi yetu ni nzuri na ya kuvutia.