Siku yetu ya pili hapa Aitutaki Island tuliitumia kwa kurelax kwenye beach, huku Amani na Malaika wakitumia ipatasavyo siku hii kwa kucheza na kuswim all day lol! Watoto wangu wanapenda sana outdoors ni kwamba walivyokua USA walikua kama wamefungiwa vile, tulivyotua tu Cook Islands walijiachia ipasavyo:) Beach za hapa ni nzuri sana, maji yake meupe pia yenye kina kifupi sana ambapo unaweza kutembea kwa umbali mkubwa bila kupata kina kirefu.