I do love this hotel nikipata nafasi ya kurudi tena Las Vegas nitajitahidi lazima nikae tena hapa lol! Nadhani siko peke yangu kwenye hili maana Amani na Malaika waliataka kukesha kwenye dirisha so waone dancing water ambayo kuanzia saa mbili usiku, shoo ilikua kila baada ya dk 15. Ilibidi tufunge mapazia na kuzima TV ili tusione au kusikia music tuweze lala la sivyo nadhani tungekesha :) I did well kwa kweli nilichagua hotel nzuri maana ilikua muda wa mama kuchagua hotel anayopenda :)
I do love Vegas kwa kweli, hapa kila mtu yuko kwa ajili ya kuhave fun na ndio raha yake yenyewe. Hii ni mara yangu ya pili kuja hapa mara ya kwanza ilikua kwenye honeymoon yangu 2004. Baada ya kuamka na kuchange kwenye mummy’s hotel choice tulielekea Ihoop pancake house yaani siwezi kuja Marekani bila kuvisit pancake house lol! Kama kawaida utalii muhimu ilibidi tusimame kwenye bango la Las Vegas kwa ajili ya picha ya kumbukumbu :) Oh dear, siku hizi America kila kitu ni foleni yaani kuna watu wengi kila sehemu, fikiria mpaka hapa kwenye bango kuna foleni ya kupiga picha. Baba Amika akajionea isiwe tabu cha muhimu ni kupata picha inayoonyesha bango akasema mke wangu simama hapo pembeni tujipigie picha haraka tujiondokee, ingawa picha hazikuwa nzuri sana maana kuna watu wanaonekana nyuma yetu but tulipata picha ya bango la Las Vegas lol!
Was so nice to meet Mange na familia yake in Las Vegas nao walikua hapa kwa ajili ya holiday. Siku zote huwa napenda wazazi ambao wanapata nafasi ya kusafiri na watoto wao na kupata experience hii kwa pamoja inapendeza sana. Huwa nampenda sana Mange so nilifurahi sana kuwaona hapa, namuombea aendelee kubarikiwa siku zote yeye na familia yake.
Yaani ilikua kama bahati vile siku hiyo hiyo nilipata nafasi ya kuonana na my fb friend Kathleen Kuntz akiwa na mumewe na wifi yake, nao walikua Las Vegas kwa ajili ya weekend. Was very nice to meet you Kathleen :)