Tag Archives: drive

@Phoenix Arizona, Utah & Las Vegas, USA. July 2004

 

Stratophere Top of the World Restaurant, Las Vegas

 

Hii ilikua part ya honeymoon yetu. Nachopenda kuhusu hii safari ni kwamba tulidrive all the way to Las Vegas, tulitumia muda wa wiki moja kufika Las Vegas kwa sababu tuliamua kusimama na kulala sehemu mbali mbali on the way.  Pia tulitembelea Meteor Crater pamoja na Grand Canyon ambapo tulilala usiku mmoja. Kwa kusema ukweli safari hii ni moja ya safari ambazo nilizipenda sana mpaka leo imeshapita miaka karibu saba bado naikumbuka kama jana vile, ningependa tena kufanya safari kama hii sehemu nyingine duniani. Hii ilituwezesha kutembelea na kuona maisha ya real Amarican people maana tulikua tunasimama kwenye small town na kulala kwenye small motels.

Wakati tukiwa njiani tulisimama kwenye mji mmoja kuweka mafuta pamoja na kununua drinks. Kwa nini nimekumbuka huu mji ni kwamba ulikua wa kushangaza sana ulikua tofauti sana na miji yote ambayo tumepita, this small town watu wake walikua wako very strange yaani jinsi wanavyovaa ni kama watu wa miaka mingi sana nguo ndefu na ambazo zina staili moja pia wanafuga nywele ndefu kwa wanawake na kufunga kama mabutu mawili au moja. Wanawake wote walivaa staili zinazofanana pia wanaume. Gari letu lilivyokaribia tu kwenye mji huu tuliona watu wanatuchungulia toka majumbani tulivyofika Petrol Station mambo yalikua yale yale. Tukadhani labda upande huu ni ule upande wanaoishi wale wabaguzi wa rangi ukilinganisha mimi ni African tukaona bora mimi nibaki kwenye gari Mr. yeye aingie dukani kwa ajili ya kulipia mafuta na kununua drink.  Aliporudi hata yeye alishangaa sana akasema kwa kweli mji huu uko tofauti bora tundoke mara moja hatukuweza jua kisa na mkasa wa huu mji.

Baada ya mwaka mmoja kupita siku moja naangalia Oprah Winfrey Show then hapo ndipo nilipata jibu. Kumbe mji unaitwa Colorado City ambao uko Arizona, watu wanaoishi hapa wanadini yao ya tofauti inayoamini maisha ya wake wengi pia ni ruska kwa wasichana wadogo kulewa na watu wazima ambao wamewazidi miaka mingi sana. Kitu cha kushangaza ni kwamba watu wengi hawakuwa wanajua kitu kama hiki kiko kwenye nchi iliyoendelea kama America. Wamarekani wenyewe walishangaa na kusikitishwa kuwa kitu kama hiki kipo na kinaendelea nchini kwao. Pia tukajifunza kuwa kuna mengi ambayo yanaendelea kwenye mji huu ambao kwa ujumla ni vya kushangaza pia hawataki wageni kwenye mji wao ndio sababu kubwa ya wao kutuchungulia na kukimbilia ndani. Baada ya kumaliza kuangalia na kuelewa kwa undani nilibaki mdogo wazi na kusema wow!

Baada ya kutoka Colorado City Arizona tuliendelea na safari yetu kama kawaida. Mji mwingine ambao ulinifurahisha sana ni small town call Zion. Iko katikati ya desert ambao umezungukwa na milima mikavu katikati yake ndio kuna huo mji. Tulilala Zion Park Lodge  na kupata nafasi ya kuzungukia mji kidogo nilipapenda kwa kweli ni pazuri sana.

Tulipoanza kuingia Las Vegas mambo yakaanza kubadilika ghafla mambo yakawa ni kufurahisha tu. Tulivyofika tu Stratophere Hotel nilibaki mdogo wazi kama vile nilikua naangalia movie kumbe si movie ni hali halisi hiyo. Tuliposimamisha gari tu wafanyakazi wakaja kwa kasi na kutufungualia milango ya gari huku wengine wakitoa mizigo kwenye gari na kutuomba ufungua wa gari kabla hata sijamaliza kushangaa naona gari letu hilo linaondoka na kwenda sijui wapi yaani lilipotea machoni mwetu ghafla ndio nikakumbuka zile movie nilizokua naona zamani kuwa watu wachukuliwa magari kwenda kupaki mmh! eti leo hii ni mimi nilibaki kutabasabu kabla hayo hayajaisha Mr. ananishika ananishika mkono na tunaelekea hotelini wow! kuelekea reception unahitaji kupitia Casino baadae nagundua kuwa ndio staili ya Las Vegas hiyo karibu hotel zote ziko hivyo.

Tulivyocheck in ikabidi tuzunguke zunguke hotelini hii ni Vegas uwezi kukaa sehemu moja au kulala kila sehemu ni fun tu. Baada ya kuzunguka tukaamua kwenda Casino na nikaamua kucheza Slot Machine ambapo nilikua na kidola changu 20 uwezi amini muda mfupi baadae najikuta nina 200 wacha ninogewe na kuendelea kucheza big mistake baada ya muda kidogo najikuta nimeliwa pesa zote nina ziro mkononi nilichukia huyo, hapo hapo hubby yeye kashinda $120 si nisianze kubembeleza angalau anipe $10 nikiwa na imani kuwa nikicheza nitashinda tena angalau kurudisha pesa zangu. Alichofanya alicheka maana yeye kacheza mara moja kashinda na kaacha kucheza si asinikatalie nilichukia sana nilimnunia karibu siku nzima hata sikuweza kwenda kwenye Stratophere Rides ambapo tulikua na mpango wa kwenda kisa nimeliwa kwenye kamali lol sasa nikikumbuka naishia kucheka si aibu ilioje. Ila ukweli ni kwamba mpaka leo nataka siku nikienda tena Vegas lazima nicheze nilirudisha $200 zangu hahahaaa…

Uzuri sikuacha mambo ya kamali yaniharibie honeymoon na mwisho wake tuliishia kuipenda Las Vegas kupita kiasi, tuliweza tembelea sehemu mbali mbali na kuweza kuenjoy fun za Vegas. Kama kawaida yangu siwezi kwenda sehemu bila kuwa na food favourite, nilipenda sana Strawberry pancakes from  I-Hope, sikuwa peke yangu inaonyesha ni sehemu mashuhuri sana kwa pancakes maana foleni ya kuingia si mchezo ila ukishaingia tu utajua ni kwanini.

Tulikaa Vegas kama siku nne, one night tuliweza kwenda romantic dinner at Stratophere Restaurant Top of the World, ilikua fun maana ukikaa huko juu unaona kama vile jengo linazunguka wacha tubishane na hubby mi nikisema kuwa madirisha yanazunguka yeye anasema hapana ni sisi tunazunguka mpaka tulipomuuliza waiter na kutuambia kuwa ni sisi tunazunguka mh! nikaona hii kali nikaona makubwa ya ulimwengu kwa ujumla tulienjoy sana. Pia tulitembelea Star Trek, hoteli mbali mbali, restaurant na bar tofauti na kila moja ina mvuto wake ni kweli mambo ya Vegas yaache Vegas kwa kweli. Muda wetu wa kukaa hapa ulionekana mdogo sana siku nne hazikutosha kwa kweli lazima turudi tena.