Tuliwasili Venice Italy salama kwenye mji uliyojengwa juu ya maji kama unavyoitwa na watu wengi. Baada ya kucheck in kwa hotel tukaingia mitaani nasi kujumuika na watalii wenzetu kushangaa lol! Tulikua na bahati siku hii hali ya hewa ilikua nzuri jua lilikua linawaka vizuri na kufanya watalii kuwa wengi sana mitaani. Sasa sio kupigana vikumbo uko utafikiri tulikua sokoni lakini kwa jinsi mji ulivyo mzuri kila mtu alikua anaonekana na furaha. Venice ni moja kati miji mashuhuri duniani wenye historia kubwa.
Mara yangu ya kwanza kuja kwenye mji huu ilikua ni 2002 wacha mtanzania mimi nishangae maana kila kitu nikiangalia kwangu kilikua ni kigeni lol! Unaweza angalia kwenye post ya VENICE, ITALY 2002 kwenye post za nyuma. Nakumbuka vizuri jinsi nilivyoupenda mji huu nikasema lazima nirudi tena, furaha iliyoje nimeweza rudi tena ingawa imechukua miaka kumi lol! Ningependa kurudi tena ila safari hii nataka iwe summer maana vipindi vyote hivi viwili tumekuja wakati wa winter, inasemekana summer kunapendeza zaidi ila kwa wale wasiopenda kubanana summer si nzuri kwao inasemekana watalii wanakua wengi sana kulinganisha na kipindi cha winter. Tutakuwepo hapa kwa siku mbili then tunachukua cruise ship kutokea hapa Venice to Miami Florida, yaani tunasubiri kwa hamu kweli kukatiza Atlantic ocean to America kama Titanic vileĀ :)