Losing Weight After Holiday

Wow! OMG! This is really good nimefanikiwa kupunguza 3.3kg kwa siku sita happy happy me. Siku ya kwanza kabla sijaanza diet yangu hii nilipima na kukuta nina 74.4kg, fat 30 na water 49. Baada ya wiki moja nimepima na kukuta nina 71.1kg, fat 28 na water 47. Kwa diet yangu hii ya siku sita ambayo iko chini ya hii page kuanzia siku ya kwanza mpaka ya sita ndio imefanya mambo haya.

6 days diet

Kwa kweli inawezekana diet si lazima iwe ile ambayo unaweza kufanya njaa au iwe serious sana. Mimi wiki hii nimefanya kama vile si diet kwa kweli sikupanga kesho nitakula nini kila kitu nimejikuta nakifanya muda tu ambao nataka kula kitu. Cha msingi nimezingatia sheria ya diet zangu za mwanzo maana nimeshajua nini kibaya kwenye mwili wangu. Kwangu mimi ni wanga na carbs ndio tatizo kubwa kwangu maana nikila nakula kwa wingi sana na siwezi kujicontrol kwa hilo. So kwa siku sita nilichofanya kutokula vitu hivi, nadhani kila mtu anaweza kujipangia diet yake kwa kufuata mvumo anaona yeye unaomfaa na kuzingatia sheria chache ambazo ni mafanikio sana kwenye diet nyingi. Wewe unaweza angalia nini hasa ni ugonjwa wako kwa maswala ya chakula na usiguse vitu hivyo siku zako zote sita na kula vile ambavyo unaweza kucontrol wakati ukianza kuvila na kuongeza muda wa mazoezi na kujitahidi kumove a lot yaani tembea kila mara na jifanyie kazi ambazo utatumia nguvu kidogo hapa na pale nadhani kwa namna hii unaweza pata mafanikio makubwa katika maswala ya diet.

6 days diet

Siri yangu ya kupungua mimi nimeshaijua nadhani sasa kwa staili hii siwezi tena kuwa over weight nimeshajua ni wapi pa kuangalia. Good luck wapendwa hope nanyi mtapata mafanikio kwa diet ambayo una mpango wa kuanza soon maana huna sababu za kujiachia na kunenepa kwa kweli ni bora kuangalia kabla, kazi ya kutoa unene si rahisi kabisa bora kujiangalia kwa makini now and then. Tunasubiri maoni yako na kama umeanza na wewe tujulishane basi mwenzetu umefanya nini na mafanikio yako ni yapi ili kuwapa na wengine changamoto, siri yangu ni hii tunasubiri yako kama utafuata hii karibuni sana kama utatunga ya kwako pia karibu sana. Cheers!!!!!!!!

6 days diet

DAY SIX

Good news guys, nimefanikiwa kumaliza siku ya sita vizuri. Nimefanikiwa kufanya mazoezi kama kawaida ya kutembea na kuruka, kwa namna hiyo kwa siku zangu sita nimefanya mazoezi kwa siku nne. Si mbaya kabisa kama mtu unaweza fanya mazoezi angalau mara nne kwa wiki. Nimekunywa maji ya moto kama kawaida nusu lita na nimeona mafanikio makubwa sana upande wangu wa kiuno tumbo limepungua sana bila hata kufanya mazoezi ya tumbo, ila next week nitajitahidi kuongeza mazoezi ya tumbo ili nipate mafanikio makubwa kwa haraka.

Breakfast:

Asubuhi kabisa nimekula kipande cha Apple pamoja na nusu embe. Kwenye mida ya saa nne hivi nimekula kiganja kimoja cha roast almonds na Octivia laban 180ml.

Lunch:

Leo nimeamua kula roast chicken wings 5 ambazo nimetengeneza mwenyewe kwenye oven pamoja na salad ya majani ya lettuce, slice za hoho na tomato.

Dinner:

Kama kawaida nimekula dinner yangu kabla ya saa kumi na moja jioni ni muhimu sana kutokula chochote zaidi ya maji baada ya saa hii. Nimekula machungwa madogo mawili na 3 rambutan.

Diet yangu ya siku sita imeishia hapa kwa ujumla nimefurahi sana kuweza kufikisha siku zote maana wakati naanza nilikua sina hamu kabisa ya diet na nilijua nitaishia njiani. Ila nashukuru kwa muundo huu wa diet ambao umenisaidia kula kitu chochote nachotaka ila kuangalia mfumo wa low carbs na low calories diet pia kujitahidi kutokula kabla ya saa kumi na moja jioni. Pia wiki nzima nimejitahidi kujishughulisha na mazoezi mengine ya kawaida kama vile kufagia nyumba bila kutumia vaccum cleaner badala yake nimetumia mfagio mrefu peke yake inafanya utumie nguvu zaidi maana ni manual. Mara kwa mara nimejitahidi kujifanyisha kazi zaidi za nyumbani ili kujiweka busy kujishughulisha na kutembea na kazi za hapa na pale kuongeza chance ya kupunguza calories zaidi. Upimaji wa uzito unafanyika siku ya saba ambapo napima asubuhi sana nikiamka tu maana ndio niliopima muda huo siku ya kwanza ya diet. I hope nimefanya kazi nzuri na diet hii imefanya kazi nitawajulisha baada ya kupima. Cheers!

 

DAY FIVE

Mpaka sasa naendelea vizuri nimeweza kwenda mazoezi asubuhi kama kawaida kutembea saa moja pamoja na kuruka mara 400 bila kusahau mazoezi ya mikono. Nimekunywa maji ya moto nusu lita baada tu ya kuamka. Maendeleo yameshaanza kujionyesha maana naona sehemu nyingi zinaanza kusinyaa tena. Niko na furaha hope baada ya siku zangu sita diet yangu hii itatoa matokeo mazuri.

Breakfast:

Nimekula nusu embe pamoja na tunda damu moja dogo. Kwenye mida ya saa nne hivi nimekula mayai ya kuchemsha mawili.

Lunch:

Nimechemsha mix vegetables kama vile supu kidogo, nimekaanga sausage nne ambazo nimekatakata na kuchanganya pamoja kipindi nataka kula na hii supu yangu ya vegetables.

Dinner:

Hii huwa nakula mida tofauti toka saa tisa mpaka saa kumi na moja, nimekula 3 rambutan na ndizi mbivu ndogo 3, sijui kwa nini najua ndizi mbivu si nzuri kwenye diet yangu ila tangu nirudi toka Australia nimejikuta ghafla natamani ndizi sana tu, sijui kwa sababu nilikuta this time ndizi very expensive in Australia na kuamua kuzikomesha sasa. Kwa ujumla si nzuri kwenye low carbs diet ila nimeamua kuzila tu kwenye hii diet yangu mpya tutaona itakavyokuwa baada ya siku sita kama itafanya kazi au vipi.

Leo nimejitahidi kula vyakula vyote vya afya sijachanganya kitu ambacho si kuzuri kwa mwili pia nimefanya mazoezi kwa ujumla siku yangu ya leo ni nzuri lakini kazi ipo kwa kweli hapa nilipo nasikia njaa haswa ngoja nimalize hapa niendezangu kulala na kusubiri ya kesho ambayo ni siku yangu ya sita. Cheers!

 

DAY FOUR

Kama kawaida nimeamka mapema leo na kunywa maji yangu ya moto kama ya chai nusu lita. Nimekwenda for a walk kwa saa nzima pia nimeruka huku nikifanya mazoezi ya mikono mara 400. Kwa ujumla nimefanya mazoezi kwa muda wa saa moja na nusu hivi.

Breakfast:

Nimekula nusu embe kwanza harafu mida ya saa tano hivi nikala ndizi mbivu kubwa

Lunch:

Leo nimeamua kula sausage 3 na baada ya muda kidogo nikala dagaa za kukaa kiganja kimoja. Nilikua natengeneza dagaa ambazo nimeletwa jana na ndugu yangu toka Tanzania, nikaona ngoja nionje kidogo hahahaaaa…. Tatizo ambalo limejitokeza leo ambalo si zuri kwa diet ni kwamba nimekula hivi vitu vyote kwa lunch bila salad au mboga mboga kisa nimeona uvivu kutengeneza maana njaa ilikua nimenikamata hasa.

Dinner:

Nimeamua kutokula dinner kubwa leo, nimekula matunda 3 rambutan, ndizi kubwa 2, ovacado pamoja na Octivia 180ml hii ni muundo wa mtindi mwepesi. Nimeamua kula ovacado maana iko kwenye jamii ya mboga mboga pia itasaidia maana sikula mboga au salad mchana. Kumbuka vitu vyote hivi nimekula kati ya mchana mpaka ilipofika saa kumi na moja jioni baada ya hapo sijala chochote naendelea kunywa maji kama kawaida mpaka muda wa kufikia kwenda kulala niwe nimemaliza lita zangu 2 za siku.

Pamoja na kuwa diet hii haiko kwenye mpangilio au plan yoyote najiamulia kula nachoona kwa siku hiyo ila najitahidi kufuata mfumo wa low calories pamoja na kujitahidi niwezavyo kutokula vitu vya wanga kama vile ugali, wali, ndizi, viatu etc. Siku hii ya nne nimechaanza ona mafanikio yameanza kujitokeza eneo la tumboni, limeanza kupungua kwa kasi sana I hope mfumo huu unaweza nisaidia kutoa kilo ninazotaka ifikapo siku ya sita. Nina furaha nimeweza kwenda kufanya mazoezi leo maana mazoezi ni mazuri sana kama ukiweza kufanya hivyo, naomba kesho niamke si mvivu ili niendelee na hii kazi ya mazoezi. Cheers!

 

DAY THREE

Leo nimeamka mapema sana na kufanikiwa kwenda mazoezi. Nimeenda for a walk kwa muda wa saa nzima, nilivyorudi nimeruka pamoja na mazoezi ya mikono mara 400. Kama kawaida nilivyoamka tu nimekunywa maji ya moto kama ya chai nusu lita.

Breakfast:

Small ovacado pamoja na ndizi mbivu kubwa moja, baadae kwenye saa tano hivi nikajikuta nakula embe ambalo nilikua nimeletewa na ndugu yangu toka Dar yaani lilikua na harufu ya kuvutia kweli uzalendo ukanishinda. Naelewa siruhusiwi kula matunda yenye sukari nyingi  ila nimetamani na nimeona bora nile tu. Hope hii diet yangu mpya itafanya kazi nzuri na kupata mafanikio mazuri maana…

Lunch:

Mh! kazi ipo hapa, familia iliagiza KFC chicken zikaninukia vizuri sana nikaamua kula vipande 2 vikubwa na coleslaw pamoja na majani ya lettuce. Najua kuwa si kitu kizuri kwa diet nilijitahidi kula kama ilivyo bila wanga kama vile chips etc.

Dinner:

Kama kawaida nimekula kabla ya saa kumi na moja jioni. Ilipofika muda huo nimekua nimemaliza chakula changu kwa siku naendelea kunywa maji mpaka muda wa kwenda kulala kufika. Nimekula ndizi mbivu kubwa 2 na Octivia laban ambayo ni 180ml. Hii laban ni muundo wa youghurt nyepesi kama sijakosea.

Siku yangu imeisha kwa furaha kwa sababu nimeweza fanya mazoezi leo, ila kidogo nimesikitika kwa kula vitu vya sukari kama vile ndizi mbivu, embe pamoja na kuku za KFC ambazo si nzuri kwa diet. Ila nimejitahidi kula vyote hivyo kwa mpangilio bila kula calories nyingi kwa siku. Hope siku ya nne itakuwa ya mafanikio zaidi ili baada ya siku sita niwe nimepunguza kilo za kuridhisha. Cheers!

 

DAY TWO

Kama kawaida nimeamka na kunywa maji ya uvugu uvugu nusu lita. Mazoezi ambayo nimefanya leo ni ya kawaida tu kama vile kazi za nyumbani na kutembea kidogo kutoka na kwenda kwenye gari.

Breakfast:

Leo sikula chochote asubuhi si kwa sababu ya diet bali nilikua sina muda wa kufanya hivyo kutokana na kuchelewa kanisani. Ila kumbuka ni muhimu sana kula breakfast inasidia kukupa nguvu kuanza siku yako pia kufanya mwili wako ufanye vizuri kwenye maswala ya kukata calories.

Lunch:

Nimesteam mix ya vegetable kama vile zucchini, cauliflower, eggplant na majani ya lettuce kidogo. Nimekula vegetables zangu na 3 BBQ lamb chops.

Dinner:

Kiganja cha korosho zilizokaangwa, glass moja ya orange juice, one pear na 180ml Octivia nadhani ni muundo wa laban milk. Nimekula kwenye saa kumi hivi na kitu kabla ya saa kumi na moja. Kumbuka usile chochote baada ya saa kumi na moja jioni zaidi ya maji ya kunywa tu. Hapa nilipo nimeshaanza sikia njaa lakini nitajitahidi kwenda kulala mapema usizidi muda wa saa tatu usiku ili nisipate vishawishi vya kula chochote. Hii ndio siri yangu nikisikia njaa usiku nakwenda kulala mapema.

Guys, mazoezi ni muhimu sana kama unaweza jitahidi uwezavyo angalau hata kutembea. Mimi siku ya pili sasa nimekua mvivu kufanya mazoezi ila nitajitahidi sana siku zijazo kufanya maana yanasaidia kasi ya kupunguza uzito. Siku yangu ya pili nimeimalizia kwa kumalizia kunywa maji yangu lita mbili. Nashukuru siku yangu leo imeisha bila kupata kishawishi cha kula wrong food naomba kesho pia siku ya tatu iwe hivi. Cheers!

 

DAY ONE

Safari hii nimeamua kujaribu kitu tofauti kidogo na diet ambayo nimeizoea. Toka nimerudi holiday ya siku 22 imekua shida sana kurudi kwenye staili yangu ya diet na nimeona nikiendelea kusubiri kupata nguvu ya kuanza diet hali yangu itaendelea kuwa si nzuri nitaendelea kula bila mpangilio na kuongezeka nako hakutanisubiri. Kwa hiyo nimeamua kuanza kwa staili hii na nitaangalia baada ya siku sita kama nitakua nimefanikiwa kupungua basi nitaendelea nayo pia.

Baada tu ya kuamka:

Nimekunywa maji ya uvugu uvugu nusu lita. Nikaosha vyombo ambapo inaweza chukua nusu saa ukiwa umesimama ni moja wapo ya mazoezi.

Breakfast:

Nimekula mchanganyiko wa matunda ambapo ni kidogo tu. Siri hapa sikupanga kabisa nitakachokula, muda ulipofika na nikasikia njaa nikatengeneza mchanganyiko wa matunda nikala. Matunda yenyewe ni chenza, chungwa, jamii ya matunda damu pamoja na kiwi fruit.

Nilikwenda shopping ambapo siku zote najitahidi kupaki gari yangu mbali kidogo ili niweze tembea pia nikifika kwenye mall najitahidi kuzunguka kadri niwezavyo ili kupoteza muda hata kama nilikua nataka kununua kitu sehemu moja na kurudi. Hii inaweza nichukua karibu saa nzima au zaidi kwa namna hii naweza kujikuta nimetembea karibu saa nzima bila kutegemea. Najitahidi siku zote nikienda shopping kuvaa viatu ambavyo viko poa kwa mazoezi mimi napendelea Flip Flop ambazo ni nzuri sana kwa kutembea.

Lunch:

Nimekula BBQ lamb chop ndogo 4 pamoja na steam vegetable kama vile cauliflower, eggplant na zucchini.

Dinner:

Ambayo nimekula kwenye saa kumi jioni, nimejitahidi kama kawaida kutokula chochote baada ya saa kumi na moja jioni. Nilitamani sana Ice Cream nilishindwa kujizuia nilichofanya nikaenda Cold Stone na kula my favorite ice cream, hii ndio ilikua dinner yangu. Najua kua ni wrong ila roho ilikua inataka na sikuweza kuvumilia niliamua ngoja nijaribu staili hii nile kitu roho napenda ila kwa mpangilio huu.

Mazoezi yangu ya leo yalikua ya staili ya kawaida tu kama vile kwenda shopping, kazi za ndani pamoja na kupamba mti wa xmas maana ilikua ndio siku yetu ya kufanya hivyo. Nilijitahidi kunywa maji lita mbili pia nilijitahidi kulala mchana kama masaa mawili hivi. Inasemekana ni muhimu mwili kupumzika hasa kulala angalau masaa 8 kwa siku, mimi huwa kama sikulala masaa yote usiku basi nayalipa mchana hasa ikiwa ni siku ya weekend.

Hii ndio diet yangu ya siku ya kwanza, I hope baada ya siku 6 nitaona mabadiliko na kufanikiwa uzito hahahaaaa… I hope. Sawa guys nitaendelea kupost kila siku nilichofanya kwa maswala ya diet ili tuone kama itafanya kazi. Najitahidi kila siku kula kitu kimoja roho napenda hata kama si kizuri kwa diet yangu kwa staili hii inanipa moyo wa kuendelea. Hii ndio diet yangu ya siku ya kwanza.

 

KASHESHE YA KUPUNGUZA UZITO.

Jamani kusema ukweli tangu nirudi toka holiday wiki mbili na kitu sasa nimeshindwa kabisa kurudi kwenye mambo ya diet. Nimekua naanza ila baada ya siku moja mbili najikuta nasimama na kula kitu ambacho najua kabisa si kizuri kwangu. Ingawa nimekua najitahidi sana kwa mazoezi na ilinisaidia kupunguza kilo zangu nne kati ya saba nilizoongeza ila kama wiki sasa nimejikuta nakula vitu ambavyo ni vibaya kabisa kama vile chocolate, ice cream na cakes kwa wingi haswa naogopa kwa kweli nakoenda ni kubaya kweli. Sijaangalia uzito wangu sasa kwa siku kama nne hivi ila naogopa kujua nimeongeza ngapi kwa siku chache hizi maana nimekua mbaya kabisa kwenye maswala ya chakula.

Najua kuna wengi wako kama mimi ambao mnaangaika na suala hili tuungane basi pamoja na kuliongelea wewe mwenzetu ni kitu gani hasa kinakufanya ushindwe kabisa kila mara ukianza diet yako. Mimi tatizo langu kubwa ni chakula changu cha kitanzania nikikiona tu roho yote inanitoka inabidi nile tu na sio basi nakula kidogo nakula kingi haswa mpaka najisikia vibaya nikisema kuwa nile kidogo siwezi kabisa ni bora nisile kabisa. Cha kushangaza naweza kujizuia chakula kingine kama cha western ila cha kwetu nilichokulia nacho siwezi kuvumilia kabisa.

Wapendwa tuungane pamoja na kudiscuss suala hili kwenye page hii kama utapenda, usijali siwezi weka email ya mtu yeyote ambae atachangia pia kama hata utaki kuandika jina lako usijali pia tusaidiane kupeana mawazo kwenye suala hili la kupunguza huu uzito na ni kwanini watu wengi tunakwamba mara kwa mara na kurudia sehemu ambao tumejiahidi kuwa makini zaidi.

Nimejiwekea ahadi kuwa kesho kiwe kisiwe lazima nianze tena diet yangu iwe kwa heri au shari maana nisipoangalia nitajikuta narudia kule nilikotoka ngoja niamke mapema before too late. Nitakachofanya ni kupima uzito hapo kesho asubuhi na kuanza kwa kasi zote nitajitahidi sana kuwa mvumilivu na majaribu yote nitakayokumbana maana naelewa nikiweza kufanya hivyo angalau kwa siku tatu nne hivi basi nitakua tayari kuendelea maana mwanzo ni mgumu sana hasa baada ya holiday na kujiamulia kujilia chochote unachotaka. Kazi kwetu wapendwa tuanze pamoja na kama inawezekana tuachagie hoja zetu kwa suala hili, mimi nitajitahidi kila siku kuandika nilichokula siku hiyo na nimefanya mazoezi gani ili tuangalia baada ya siku sita nitakua nimefanikiwa kutoa kilo nazotaka? Swali linabaki pale pale, hope nitafanikiwa this week…cheers!

6 thoughts on “Losing Weight After Holiday”

  1. Dah safi dada zawadi nimependa issu yako kwa ujumla na mimi mwenyewe nlikuwa nakilo kama 84kg hivi june mwaka huu bt from pale nikaanza kujiangalia haswa nilivyoanza kufuatilia mambo ya afya coz watu walikuwa wanansema sana kibonge asie na hela,so kujua BMI which measure mass and weight bc nkasema ngoja nijicheki wapi pa kuanzia,zoezi mie mvivu na kazi zangu ni ngumu na gimu hakuna pande za Rukwa so food food!nkaacha soda, chipsy,kuku wa kisasa na vyakula vya sukari na mafut mengi halafu coz napenda maji usiku silagi ila mie kuanzia saa 12!nw nina kilo 71 which is better……but still is not good nataka nibakize 65 tuu…

    1. Hi Baraka,
      Nimefurahi sana kusikia kuwa nawe umejiandalia diet yako mwenyewe na umefanikiwa kupunza kilo zote hizo. Usijali utafika hizo kilo unazotaka cha msingi ni kutokata tamaa na kila kitu ni taratibu hapo ulipofikia pia umejitahidi sana nahakika utafika hizo kilo 65. Mi safari yangu ya kupungua nilianzia 96kg imenichukua miaka miwili na kitu hivi ila nimekua napungua na kuongezeka nilichofanya sikukata tamaa hapa nilipo niko kwenye uzito niliokua nataka ila nataka nipunguze kilo 3 za mwisho ili nianze maswala ya kucontrol ili nisiwe na ongezeka na kupungua mara kwa mara. Tuendelee kuwasiliana Baraka na all the best na kazi nzuri. Cheers!

  2. nmefurahi na diet yako kwa mm nami naanza hiyo diet kwa sababu napenda kulal mno ila chakul c mpenzi tumbo halipungui naombeni ushauri wako mdada nifanyaje I need to reduce my stomach and my weight what to do

    1. Hi Dinnah,
      Kitu ambacho kitakuwezesha kukata tumbo ni kuacha kula chakula cha wanga kama vile wali, ugali, ngano. Pia carrot, embe na ndizi. Pia usinywe chai yenye sukari unakata sukari ya aina yoyote kabisa hata juice. Jaribu kula zaidi protein kama vile samaki, mayai na jitahidi usile sana nyama ya ng’ombe jaribu kuku. Kula mboga za majani kwa wingi na salad. Nadhani ukijaribu hivi vitu utafanikiwa kukata tumbo kwa kasi sana.
      Good luck dear,
      xoxo

  3. Da Zawadi napenda kujua nyama ya kuku na samaki tunachemsha au tunaipikaje. Hata me tumbo linanisumbua sana kupungua.

    1. Dear Glory,
      Mimi huwa na steam fish au kuchemsha kwenye kuku nzuri ni ukichoma na jaribu kuchukua upande wa katikati(chicken breast) na toa ngozi. Ukifuata hii diet ya low carbs hakika tumbo litaisha kabisa.
      Zawadi
      XOXO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Safiri na Zawadi