Soya Milk & Pears Porridge

Wapendwa nimetengeneza hii kitu leo kwa breakfast yaani ni kitamu sana. Nimeamua kujitungia tu ila imetoka safi sana.

Recipe

1. Chukua kikombe kimoja cha soya milk ambayo aina sukari.

2. Pears 2 zenye size ya kawaida, menya toa maganda then katakata vipande.

3. Tangawizi fresh ndogo sana, toa maganda na katakata vipande vidogo. Inategemea kama unapenda tangawizi unaweza zidisha kidogo ila inatakiwa kidogo tu.

Changanya vyote pamoja kwenye blender mpaka vyote vilainike, weka kwenye kikombe tayari kwa kula unaweza kunywa au kutumia kijiko kama uji. Inashibisha sana na itakusaidia kukusukuma mpaka muda wa lunch na ina ladha nzuri sana. Pia ina virutubisho vingi mwilini na unapata fibre nyingi kutoka kwenye pear ambayo ni nzuri kwa kujenga mwili. Mimi nimetengeneza kwa breakfast ila unaweza kula kabla ya saa kumi na moja jioni kama dinner yako pia inafaa sana tu. Unaweza pia hata kuwa unawatengenezea watoto maana ni kitu chenye afya.

Muhimu, kumbuka kuinywa mara tu unapoitengeneza isikae muda mrefu inakua si nzuri.

Enjoy and Cheers!

4 thoughts on “Soya Milk & Pears Porridge”

    1. Jaribu low fat milk nadhani itakua poa. Labda kwenye radha tu inaweza kuwa tofauti kidogo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Safiri na Zawadi