Hubby & Malaika in Thai Airways from Phuket to Bangkok
Ciem Paragon Mall
Awww…Lebua, hapa kila kitu 1st class kuanzia unavyoingia mpaka unavyotoka. Tulikaa Lebua State Tower Hotel for 3 days nilitamani zisiishe mapema. Our summer holiday inaendelea tumeingia hapa tukitokea Phuket. Naweza sema I love everything about this hotel, huduma yake ni ya kukata na shoka. Unapoingia tu unasikia harufu ya upendo moja kwa moja kwanza hotel staff anakuja kukupokea kwa upendo wa hali ya juu na kukukaribisha kukaa na huku akiwa na file lako la kucheck inn, ina maana alikua anawasubiri nyinyi specially na akimaliza kupata data zote anawasindikiza kwenye room yenu huku akiwapa maelezo muhimu kuhusu hotel with big smile. Wamefanikiwa kumfanya kila mteja kujisikia ni most important kwao nadhani hii ni huduma ya 1st class kwa kweli. Kwa wale mtakaojikuta Bangkok please jaribu hii hotel nadhani utakubaliana nami. Very happy indeed until next time Labua State Tower Hotel, cheers!!!
Tulitumia usafiri wa barabarani kufika hapa Khao Sok tukitokea Krabi, ilituchukua muda wa masaa 2 na nusu hivi. Tulifikia Baan Khao Sok Resort ambapo tuliamua kuwa na adventure kidogo na kufikia kwenye Tree House kama inavyoonekana kwenye picha. Hii ilikua special kwa Amani na Malaika maana wanapenda sana tree houses. Tulivyofika furaha iliyokuwa usoni mwao ili kuwa na dhamani kubwa. Walianza kuzunguka na kutupa story nyingi tu kuhusu Tree Houses ilikua kichekesho kweli nadhani shule zikifunguliwa itakuwa ndio habari mpya kwa rafiki zao.
Tulikaa hapa kwa siku 3 ila kwa bahati mbaya siku zetu zote tukiwa hapa kulikua na mvua za manyunyu ambazo zinakatika na kuanza. Tulisikitika sana maana plan zetu ilibidi zibadilike tulikua na mpango wa kwenda lake tour ambapo ni lake nzuri sana pamoja na jungle Elephant ride. Ila tuliweza kufanya River Tubing kwenye Sok River ambayo ilikua much fun. Kwa ujumla ilikua real adventure baada ya kulala kwenye Tree House for 3 days tulikumbuka real house maana hapa ilikua ni unyevu unyevu kwenda mbele kutokana na joto lililokua kali na mvua zisizoisha feni haikusaidia sana. Ila kwa upande mwingine tulikua happy kuona watoto wamefurahia sana maana sababu haswa ya kuja hapa ilikua ni kwa ajili yao. Hata baada ya holiday kuisha bado wanaendelea kuzungumzia hii experience. Kwa ujumla ni sehemu nzuri hasa kwa watoto, ila nadhani muda mzuri wa kwenda ni kipindi ambacho si cha mvua hahahaaaa…
For sure these two love water, this day they stay in the water more than 3hrs
Amani & Malaika
Mama wawili
Mama Amika
Having fun at Phra Nang Beach
Malaika with her sis Skye having a drink at Railay Beach
Amani at Railay Beach
Amani's having fun at Railay Beach
Amani & Malaika at Phra Nang Beach
Ilikua furaha kwetu kurudi tena Krabi and enjoy one of the best beach in the world Phra Nang. Kama kawaida tulifikia Sunrise Beach Resort tumekua tunafikia hapa since 2003. Uzuri wa Railay kumetulia sana hakuna mambo ya haraka haraka hapa just relax and enjoy if you want to go for a swim, spa or just have a lazy day yote poa tu. Jioni mambo huwa yanachangamka sana hasa Railay beach, I like to sit kwenye mkeka and have a drink huku uki enjoy sunset. That’s way I like it, cheers!!!
Over 2000 years old wall painting. Pompeii City, 2003
Majiko yao yalikua namna hii
Masalio yaliyokutwa Pompeii City
Wall painting
Sanamu za miaka hiyo
Wanyama nao walikutwa hivi
Maskini mtu wa watu yeye alikutwa hivi
Inside Pompeii City
Poor guy, kweli volcano si mchezo
Pompeii City
Pompeii City
Mabaki ya watu inasikitisha kwa kweli
Pompeii Sauna
Pompeii street
Over 2000 years old wall painting, The lost city Pompeii 2003
Wall painting, uwezi amini picha hii imechorwa thousands yrs ago
Wall painting
Volcano mountain
The lion door, Pompeii Stadium
Pompeii Stadium
Pompeii Stadium
Pompeii Stadium
Garden in Pompeii
Naples
Hubby inside Pompeii
The Pompeii entry
The entry to Pompeii
Tulikuja mji huu special kwa ajili ya kutembelea mji wa Pompeiiambao ulifunikwa na volcano miaka ya 79AD. Ilikua furaha kubwa kwangu kuweza kupata chance ya kutembea kwenye street ambazo watu wa miaka mingi sana walikua wakitumia. Pompeii’s ruins, a jump back to the Roman era in a town destroyed by the Vesuvio eruption in the 79 ad and preserve in a status unique in its kind.
Tulifika Naples by Train tukitokea Venice tulikaa hapa siku 2. Mjini Naples sikukupenda sana ulikua uko just okey sidhani kama ningependa kurudi tena ila kitu ambacho nilifurahi sana ni kutembelea huu mji wa Pompeii.
Historia ya mji huu inasikitisha sana hasa ukipata nafasi ya kuangalia masalio ya watu na wanyama ambao wamekauka kabisa na moto wa volcano. Inasemekana hakukuwa na taarifa yoyote walichoona ni mwanga kama vile wa jua kumbe ulikua moto mkali sana.
Walivyoufukua mji huu walikuta kila kitu kipo kama kilivyokua kabla ya Volcano ambapo maisha yalikua yanaendelea kama kawaida waliokutwa wakitembea, kulala hata wale waliokua shughulini walikutwa wamekauka hivyo hivyo. Ikanifanya nikumbuke mambo ya biblia kuwa siku ya mwisho hata taarifa haitakuwepo utakapo kuwa ni huko huko. Masalio mengi ya vitu vilivyokutwa kwenye mji huu yameifadhiwa kwenye Museum ya Naples. Kwa upande wangu ilikua funzo kubwa maana kabla ya hapo nilikua sijui kama kitu kama hiki kipo.