Khao Sok Thailand, July 2011

Our Tree House

 

Tulitumia usafiri wa barabarani kufika hapa Khao Sok tukitokea Krabi, ilituchukua muda wa masaa 2 na nusu hivi. Tulifikia Baan Khao Sok Resort ambapo tuliamua kuwa na adventure kidogo na kufikia kwenye Tree House kama inavyoonekana kwenye picha. Hii ilikua special kwa Amani na Malaika maana wanapenda sana tree houses. Tulivyofika furaha iliyokuwa usoni mwao ili kuwa na dhamani kubwa. Walianza kuzunguka na kutupa story nyingi tu kuhusu Tree Houses ilikua kichekesho kweli nadhani shule zikifunguliwa itakuwa ndio habari mpya kwa rafiki zao.

Tulikaa hapa kwa siku 3 ila kwa bahati mbaya siku zetu zote tukiwa hapa kulikua na mvua za manyunyu ambazo zinakatika na kuanza. Tulisikitika sana maana plan zetu ilibidi zibadilike tulikua na mpango wa kwenda lake tour ambapo ni lake nzuri sana pamoja na jungle Elephant ride. Ila tuliweza kufanya River Tubing kwenye Sok River ambayo ilikua much fun. Kwa ujumla ilikua real adventure baada ya kulala kwenye Tree House for 3 days tulikumbuka real house maana hapa ilikua ni unyevu unyevu kwenda mbele kutokana na joto lililokua kali na mvua zisizoisha feni haikusaidia sana. Ila kwa upande mwingine tulikua happy kuona watoto wamefurahia sana maana sababu haswa ya kuja hapa ilikua ni kwa ajili yao. Hata baada ya holiday kuisha bado wanaendelea kuzungumzia hii experience. Kwa ujumla ni sehemu nzuri hasa kwa watoto, ila nadhani muda mzuri wa kwenda ni kipindi ambacho si cha mvua hahahaaaa…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *