Category Archives: Thailand

Chiang Mai, Thailand

Celebrating Thai New Year in style

 

Ilikua furaha kwetu kuja hapa Chiang Mai kipindi hiki cha Thai New Year celebration.  Kila mwaka huwa wanakua na festival kubwa kusheherekea mwaka mpya kwa fire works, balloons, lanterns  and lantons kwa kweli kunapendeza sana. Tulifikia kwenye heritage B&B ambayo ilikua karibu sana na mto ambao unatumiwa katika sherehe. Tulikaa hapa kwa siku nne na kupata picha halisi ya sherehe hizi ambapo kila usiku anga lote linapendeza na lanterns na mto unapendeza na lantons zenye candle za kupendeza.

Amani na Malaika walifurahi sana kushiriki kwenye sherehe hizo pamoja na wenyeji ambapo nao waliweza kuweka lantons zao kwenye mto na kumake a wish. Hali ya hewa in Chiang Mai kuna kibaridi kidogo sio kama sehemu nyingi za Thailand. Pia kama kawaida ya Thailand nilipata nafasi ya kutembelea Spa ambapo safari hii nilikwenda kwenye spa na kupata Thai massage ya aina yake ilikua iko poa sana ingawa nimeshapata Thai massage sehemu nyingi Thailand hii ilikua kiboko wanasema ni modern Thai massage, pesa yangu niliyolipa ilikua ya halali kabisa. Kipindi hiki ni cha low season ila tourist wengi wanakuja kwa ajili ya hizi sherehe na hakika zinapendeza sana.

Greenery Resort Hotel Khao Yai Thailand, July 2011

Greenery Resort

 

Pande hii ya Thailand hatujawahi kuufiki hii ilikua ni mara yetu ya kwanza. Tulikuja special kwa ajili ya Greenery Resort ambayo iko famous sana kwa ajili ya watoto na familia nzima kwa ujumla. Kuanzia makaribisho mpaka huduma yote ilikua nzuri sana. Amani & Malaika walifurahia sana hii ilikua special kwa ajili yao. Kitu cha kwanza walichoona tulivyofika tu ilikua ni hotel pool ambayo ilikua amazing. Pia walipata nafasi ya kutembelea The life park ambayo iko chini ya hotel ambayo ina michezo mingi sana ya watoto. Bila kusahau Elephant(Tembo) ride adventure ambayo ilikua awesome.

Hotel ina aina tofauti za room zikianzia za chini kabisa mpaka za juu, sisi tulichukua this time standard room. Muda wetu mwingi tulitumia nje kwenye michezo ya watoto hatukuona haja ya kuchukua room nzuri sana maana hatutaitumia sana zaidi ya kulala tu. Tulikaa hapa for 3 nights watoto walifurahi sana wanasema kuwa ni one of their favourite hotel this summer holiday.

Labua State Tower Hotel, Bangkok. July, 2011

The view of Bangkok from 63 bar

 

Awww…Lebua, hapa kila kitu 1st class kuanzia unavyoingia mpaka unavyotoka. Tulikaa Lebua State Tower Hotel for 3 days nilitamani zisiishe mapema. Our summer holiday inaendelea tumeingia hapa  tukitokea Phuket. Naweza sema I love everything about this hotel, huduma yake ni ya kukata na shoka. Unapoingia tu unasikia harufu ya upendo moja kwa moja kwanza hotel staff anakuja kukupokea kwa upendo wa hali ya juu na kukukaribisha kukaa na huku akiwa na file lako la kucheck inn,  ina maana alikua anawasubiri nyinyi specially na akimaliza kupata data zote anawasindikiza kwenye room yenu huku akiwapa maelezo muhimu kuhusu hotel with big smile.  Wamefanikiwa kumfanya  kila mteja kujisikia ni most important kwao nadhani hii  ni huduma ya 1st class kwa kweli. Kwa wale mtakaojikuta Bangkok please jaribu hii hotel nadhani utakubaliana nami. Very happy indeed until next time Labua State Tower Hotel, cheers!!!

Khao Sok Thailand, July 2011

Our Tree House

 

Tulitumia usafiri wa barabarani kufika hapa Khao Sok tukitokea Krabi, ilituchukua muda wa masaa 2 na nusu hivi. Tulifikia Baan Khao Sok Resort ambapo tuliamua kuwa na adventure kidogo na kufikia kwenye Tree House kama inavyoonekana kwenye picha. Hii ilikua special kwa Amani na Malaika maana wanapenda sana tree houses. Tulivyofika furaha iliyokuwa usoni mwao ili kuwa na dhamani kubwa. Walianza kuzunguka na kutupa story nyingi tu kuhusu Tree Houses ilikua kichekesho kweli nadhani shule zikifunguliwa itakuwa ndio habari mpya kwa rafiki zao.

Tulikaa hapa kwa siku 3 ila kwa bahati mbaya siku zetu zote tukiwa hapa kulikua na mvua za manyunyu ambazo zinakatika na kuanza. Tulisikitika sana maana plan zetu ilibidi zibadilike tulikua na mpango wa kwenda lake tour ambapo ni lake nzuri sana pamoja na jungle Elephant ride. Ila tuliweza kufanya River Tubing kwenye Sok River ambayo ilikua much fun. Kwa ujumla ilikua real adventure baada ya kulala kwenye Tree House for 3 days tulikumbuka real house maana hapa ilikua ni unyevu unyevu kwenda mbele kutokana na joto lililokua kali na mvua zisizoisha feni haikusaidia sana. Ila kwa upande mwingine tulikua happy kuona watoto wamefurahia sana maana sababu haswa ya kuja hapa ilikua ni kwa ajili yao. Hata baada ya holiday kuisha bado wanaendelea kuzungumzia hii experience. Kwa ujumla ni sehemu nzuri hasa kwa watoto, ila nadhani muda mzuri wa kwenda ni kipindi ambacho si cha mvua hahahaaaa…

Krabi Thailand, July 2011

Amani & Malaika at Phra Nang Beach

 

Ilikua furaha kwetu kurudi tena Krabi and enjoy one of the best beach in the world Phra Nang. Kama kawaida tulifikia Sunrise Beach Resort  tumekua tunafikia hapa since 2003. Uzuri wa Railay kumetulia sana hakuna mambo ya haraka haraka hapa just relax and enjoy if you want to go for a swim, spa or just have a lazy day yote poa tu. Jioni mambo huwa yanachangamka sana hasa Railay beach, I like to sit kwenye mkeka and have a drink huku uki enjoy sunset. That’s way I like it, cheers!!!

@Banyan Tree Hotel Bangkok, Thailand. July 2010

The roof top restaurant, Banyan Tree Hotel Bangkok.

 

Safari hii tulikaa Banyan Tree Hotel Bangkok  baada ya kucheck in tulielekea kwenye room yetu OMG room yetu ilikua wow! Tulichukua Club Suite ambayo ilikua ni breath taking. Baada ya kupumzika kidogo nilimuachia hubby watoto and mum alielekea shopping maana Bangkok na shopping ndio kwenyewe. Usiku hubby treated me a dinner at the roof top restaurant ambayo ilikua amazing and the food was delicous bila kusahau the view is to die for. Kids tuliwaacha na babysitter ambapo Hubby alikua amesha arrange, haya ndio mambo ya Thailand bwana :))))))

The Family Holiday in Koh Ngai, Thailand. 2010

Thanya beach resort

 

Another beautiful Island, was a low season so we had all beach for ourself and that we call fun. We stayed at Koh Ngai Thanya Resort kwenye kisiwa kuna only 5 hotel maana ni kisiwa kidogo tu. Nimeondoka na kumbukumbu ya aina yake toka kisiwani  hapa wacha nidondoke toka kwenye boat siku yetu ya kwanza tu tulivyofika. Bahari kidogo ilikua haijatulia mrembo mimi naanza telemka toka kwenye boat somehow mahesabu yangu yakakataa kutokana na boat kucheza cheza nilichojistukia niko chini mzima mzima na vitu vyangu vyote ndani ya maji kwa kweli ilichekesha sana ila nilichukia kweli pale nilipoona watu wote wanacheka. Maskini simu yangu mpya wacha ilowe na maji ya chumvi ndio ikawa mwisho wake but anyway sikutaka holiday yangu iende vibaya muda mchache ikabidi nichangamke na kuanza kuenjoy and that’s way I like it. Cheers!!!!!

Family Holiday in Khao Kheeo, Thailand. 2010

Flight of the gibbon

 

What an adventure!  Baada ya kuenjoy Pattaya tukaenda Khao Kheeo kupata adventure ya Flight of the Gibbon ni sehemu maalum imetengwa kwa ajili ya national park. Tulifikia Estete ni Tents hotel ina mandhari ya kuvutia sana. Pia nilifurahishwa sana na design ya bathroom zake ambazo zilikua zina usafi wa hali ya juu. Kipindi hiki kilikua ni cha mvua kidogo ambapo kwa upande wangu nilifurahia sana kulala kwenye tents huku mvua inanyesha ilinikumbusha mbali sana enzi hizo nilipokua nafanya kazi Red Cross Kasulu Kigoma Tanzania.

Was nice kuona upande mwingine wa Thailand ambapo huku ni mainland. Na kupata adventure ya kutembelea Zoo mida ya usiku ambapo tuliweza kumsogelea Tiger kwa karibu zaidi and of course without forget Flight of the Gibbon oh dear another new adventure in my life, that’s way I like it. Cheers!!!!

Family Holiday Krabi, Thailand. 2010

At Sunrise resort Krabi with my kids

 

Siamini mara ya kwanza nilikuaja hapa miaka saba iliyopita, hii ni mara yangu ya nne. Kitu cha kuchekesha na kizuri ni kwamba kila tukirudi wanatupa the same room ambayo tulikaa 2003 how sweet. Sunrise Resort and Railay never disappointed us and again we had an awasome time. No adventure this time just relax and enjoy until next time cheers!!!!

Family Holiday Krabi, Thailand. 2009

My baby Malaika at Railay beach

 

We love Railay Krabi, tunazidi kurudi hapa karibu kila mwaka, mambo yanabadilika kwa kasi sana. Maendeleo yanaongezeka mara ya kwanza tulipokuja 2003 kulikua na hoteli chache sana, sasa hivi zimeongezeka maradufu na kufanya kuwepo na choice nyingi ya wapi upate lunch au dinner.

Kitu ambacho bado hakijabadilika ni ukarimu wa watu  nadhani ndio sababu kubwa ambayo inatufanya tuendelee kurudi. Ni sehemu ya kila mtu uwe single, couple au ukiwa na watoto kila mtu atafurahia holiday yake.Sisi bado tunafikia the same hotel kila mara tukiwa Railay Krabi Sunrise Hotel kwa kweli hatuna cha kucomplain kabisa kuhusu hotel hii. Huduma zao ni nzuri sana na wafanyakazi wake ni wakarimu kweli pia bei yao ni ya kuridhisha.