Musoma, Tanzania

Niko pembeni ya Lake Victoria, Musoma 2003

 

Nimefika hapa kwa mara ya kwanza 2000 ambapo niliamua kwenda kuangalia nilikotoka. Baba alirudi kwao the end of 90’s, na kuweka makazi yake. Naambiwa kuwa nilishaletwa hapa nikiwa na miaka miwili. Kwa sasa baba anaishi kijiji cha Burere, wilayani Rorya mkoani Mara. Kijiji kikiwa¬† karibu sana na Kenya yaani wanasema ukiwa hapa unaweza tembea tu kuingia nchi hii ya Kenya, kwa kweli ni mbali sana tena sana. Ukitaka kuja huku inabidi ujipange kisawa sawa. Tangu mwaka 2000 nimefanikiwa kurudi kama mara mbili hivi zaidi. Ila mara zote hizo sijafanikiwa sana kuzunguka kijijini kwa sababu ya kutokua na muda wa kutosha. Nimekua naingia jioni na kuondoka asubuhi, hata ndugu zangu wengine hapo hawanijui kabisa wananisikia tu. Ila nitapanga siku moja niende ili nipeleke watoto wangu wakapaone nina uhakika watapapenda sana kama baba yao alivyopapenda.

Mwaka huu 2003 tulikua tumetokea Mwanza ambapo tulifika kwa njia ya ndege na kuchukua basi ambalo lilitufikisha Musoma. Mume wangu alifurahi sana kuona mazingira ya barabarani na kupata nafasi ya kushangaa shangaa maisha ya maeneo haya.

Kwa kusema ukweli kijiji hiki ni kizuri sana, mume wangu alipofika hapa hiyo 2008 alishangaa sana uzuri wa kijiji hiki hasa view ya lake Victoria inapendeza kweli. Anasema kuwa kuna fresh air ya ajabu huku ambayo ni adimu sana kuipata. Nakubaliana nae hapa kweli si mchezo na uzuri wake ebu jionee mwenyewe jinsi panavyopendeza.

Mume wangu alipata nafasi ya kuzungukia kijiji na kupiga picha nyingi tu maana alikaa siku nne kwa hiyo alikua na muda wa kutosha kuenjoy fresh air. Kitu kingine kilichomfurahisha sana ni pale watoto walivyokua wakimfuata kila sehemu huku wakimuita mzungu, mzungu akikumbuka huwa anacheka sana. Alifurahi sana kwa kipindi chote alichokua hapa ila anasema kulikua hakuna shower eti alikua anatumia kikombe na ndoo kujimwagia maji anasema laiti kungekuwa na shower. Kweli mzungu aachi asili yake ila kila kitu kingine alipenda sana na alifurahi kweli nao wanakijiji walimfurahia sana kupata mgeni kama yeye.

Aug. mwaka huu nikiwa nimeongozana na ndugu zangu tulifika kijijini kwa njia ya gari ambapo tulidrive toka Dar. Uwezi amini kwenda na kurudi tulitumia zaidi ya kilomita 3000, hakika huku kwetu ni mbali haswa. Tulikuja kwa madhumuni ya kujenga kaburi la mdogo wetu Michael tunashukuru tuliweza kufanikisha hii shughuli kwa haraka na kuweza kurudi Mwanza siku hiyo hiyo. Hatukuwa na muda mrefu maana kaka yangu na wadogo zangu walitakiwa kurudi kazini pia mimi nilitakiwa kurudi kwa watoto wangu ambao walikua karibu ya kufungua shule.

Kwa ujumla nchi yetu Tanzania ni nzuri sana, kuna vijiji vingi ambavyo vina uzuri wa hali ya juu kama serikali yetu ingevitengeneza na kuweka mahitaji muhimu kama vile maji safi, hospitali, shule nzuri, umeme na mahitaji mengi muhimu watu wengi wangekuwa na moyo wa kurudi kuishi huko. Kwa mfano kijiji hiki ni kizuri sana kingeweza kuvutia watalii wengi kama kungekuwa na hayo mahitaji nadhani watu wangeweza hata kujenga nyumba za holiday watu wawe wanaenda pumzika huko maana kwa hii view watalii wangekuja tu.

4 thoughts on “Musoma, Tanzania”

  1. wow! . .this awesome. love everything bout u.
    ur pics have remind me of the luo land,home sweet home
    ber ainya nyako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *