Musoma, Tanzania

Niko pembeni ya Lake Victoria, Musoma 2003

 

Nimefika hapa kwa mara ya kwanza 2000 ambapo niliamua kwenda kuangalia nilikotoka. Baba alirudi kwao the end of 90’s, na kuweka makazi yake. Naambiwa kuwa nilishaletwa hapa nikiwa na miaka miwili. Kwa sasa baba anaishi kijiji cha Burere, wilayani Rorya mkoani Mara. Kijiji kikiwa  karibu sana na Kenya yaani wanasema ukiwa hapa unaweza tembea tu kuingia nchi hii ya Kenya, kwa kweli ni mbali sana tena sana. Ukitaka kuja huku inabidi ujipange kisawa sawa. Tangu mwaka 2000 nimefanikiwa kurudi kama mara mbili hivi zaidi. Ila mara zote hizo sijafanikiwa sana kuzunguka kijijini kwa sababu ya kutokua na muda wa kutosha. Nimekua naingia jioni na kuondoka asubuhi, hata ndugu zangu wengine hapo hawanijui kabisa wananisikia tu. Ila nitapanga siku moja niende ili nipeleke watoto wangu wakapaone nina uhakika watapapenda sana kama baba yao alivyopapenda.

Mwaka huu 2003 tulikua tumetokea Mwanza ambapo tulifika kwa njia ya ndege na kuchukua basi ambalo lilitufikisha Musoma. Mume wangu alifurahi sana kuona mazingira ya barabarani na kupata nafasi ya kushangaa shangaa maisha ya maeneo haya.

Kwa kusema ukweli kijiji hiki ni kizuri sana, mume wangu alipofika hapa hiyo 2008 alishangaa sana uzuri wa kijiji hiki hasa view ya lake Victoria inapendeza kweli. Anasema kuwa kuna fresh air ya ajabu huku ambayo ni adimu sana kuipata. Nakubaliana nae hapa kweli si mchezo na uzuri wake ebu jionee mwenyewe jinsi panavyopendeza.

Mume wangu alipata nafasi ya kuzungukia kijiji na kupiga picha nyingi tu maana alikaa siku nne kwa hiyo alikua na muda wa kutosha kuenjoy fresh air. Kitu kingine kilichomfurahisha sana ni pale watoto walivyokua wakimfuata kila sehemu huku wakimuita mzungu, mzungu akikumbuka huwa anacheka sana. Alifurahi sana kwa kipindi chote alichokua hapa ila anasema kulikua hakuna shower eti alikua anatumia kikombe na ndoo kujimwagia maji anasema laiti kungekuwa na shower. Kweli mzungu aachi asili yake ila kila kitu kingine alipenda sana na alifurahi kweli nao wanakijiji walimfurahia sana kupata mgeni kama yeye.

Aug. mwaka huu nikiwa nimeongozana na ndugu zangu tulifika kijijini kwa njia ya gari ambapo tulidrive toka Dar. Uwezi amini kwenda na kurudi tulitumia zaidi ya kilomita 3000, hakika huku kwetu ni mbali haswa. Tulikuja kwa madhumuni ya kujenga kaburi la mdogo wetu Michael tunashukuru tuliweza kufanikisha hii shughuli kwa haraka na kuweza kurudi Mwanza siku hiyo hiyo. Hatukuwa na muda mrefu maana kaka yangu na wadogo zangu walitakiwa kurudi kazini pia mimi nilitakiwa kurudi kwa watoto wangu ambao walikua karibu ya kufungua shule.

Kwa ujumla nchi yetu Tanzania ni nzuri sana, kuna vijiji vingi ambavyo vina uzuri wa hali ya juu kama serikali yetu ingevitengeneza na kuweka mahitaji muhimu kama vile maji safi, hospitali, shule nzuri, umeme na mahitaji mengi muhimu watu wengi wangekuwa na moyo wa kurudi kuishi huko. Kwa mfano kijiji hiki ni kizuri sana kingeweza kuvutia watalii wengi kama kungekuwa na hayo mahitaji nadhani watu wangeweza hata kujenga nyumba za holiday watu wawe wanaenda pumzika huko maana kwa hii view watalii wangekuja tu.

Mwanza Trip. Aug, 2011

Love u guys, mwaah!

 

Safari hii ilikua ni mara yangu ya tatu kuja kwenye jiji hili, tofauti ni kwamba safari zote mbili za mwanzo nilikuja kwa njia ya anga na sio barabara. Hii ilikua ni adventure nzuri sana kwangu na wote ambao tulikua kwenye safari hii, tulianzia safari yetu Dar kupitia Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga then Mwanza. Ni safari ndefu sana ambayo ilikua inatupeleka kijiji cha Burere, wilaya ya Rorya huko Musoma. Tulijumlasha kilomita zote na kupata zaidi ya kilomita 3,000 tulitumia kwenda na kurudi Dar. Safari hii ilituchukua siku nne ambapo tuliweza maliza kilomita zote hizo, tunamshukuru mungu tulisafiri salama na kurudi salama na safari ilikua ya mafanikio makubwa ingawa tulichoka sana.

Madhumuni ya safari hii ilikua ni kwenda kujenga kaburi la mdogo wetu ambaye alifariki karibu miaka 10 iliyopita. Safari hii ilitujumuisha watoto wote wa Fatuma yaani marehemu mama akiwepo kaka yetu mkubwa Hassan, mimi, mdogo wangu aliyenifuata Obuya ambaye tulimpitia Mwanza ndipo anapoishi na mdogo wetu wa mwisho Tina. Pia tulikua na ndugu yetu  Flora pamoja na Hamis ambaye alitusaidia sana kwenye maswala ya gari pamoja na udereva, ambapo walikua wanasaidiana na Hassan.

Tulianza safari yetu kutokea Dar saa kumi na mbili asubuhi na tuliwasili Moro mida ya saa 3 asubuhi hivi. Ila tulichelewa kutoka Moro kuelekea Dodoma kwa sababu ya tatizo dogo la gari ambapo ilituweka mpaka mchana ndipo tulianza safari yetu ya kuelekea Dodoma. Tuliwasili Dodoma kwenye mida ya saa tisa jioni hivi baada ya kujisaidia na kupata lunch tulianza safari yetu ya kuelekea Singida. Tuliwasili Singida kwenye mida ya saa kumi na mbili jioni hivi hapa hatukukaa kabisa baada ya kucheki gari na kujisaidia tuliendelea na safari yetu ya Shinyanga. Tuliwasili Shinyanga usiku kwenye mida ya saa nne hivi pia hatukupoteza muda baada ya kucheki gari na kujaza mafuta tulianza safari yetu ya Mwanza, tuliingia kwenye jiji hili kwenye mida ya saa saba usiku tukiwa hoi, choka kabisa na kuamua kulala hapa.

Asubuhi ya saa kumi na mbili tulianza safari yetu ya kuelekea Musoma ambapo tulipitiliza moja kwa moja kuelekea kijijini bila kuingia Musoma mjini. Tuliwasili kijijini kwenye mida ya saa sita hivi na kufanya shughuli iliyotupeleka na kumaliza kwenye saa kumi na mbili jioni na kuanza safari yetu ya kurudi Mwanza, tuliingia Mwanza kwenye saa nne usiku hivi baada ya kutafuta msosi na kula maana tulikua na njaa sana toka tule asubuhi ya siku hiyo hatukula chochote tulielekea hotelini na kulala. Kesho yake asubuhi tulianza safari yetu ila kabla ya kutoka mjini gari lilileta matatizo kidogo ikabidi tulipeleke garage, ilituchukua mpaka mida ya mchana hivi kabla ya kuanza safari yetu ya kuelekea Shinyanga.

Tulianza safari yetu ya kuelekea Dar kupitia Shinyanga, Tabora lakini si mjini, Singida, Dodoma, Moro then Dar. Safari hii tuliamua kulala Dodoma ambapo tulifika hapa kwenye saa mbili au tatu usiku hivi. Tulipata nafasi kwenye Veta hotel ambayo kwa ujumla ilikua nzuri. Kesho yake asubuhi tulielekea kwenye makaburi ya Kizota kwenda kutizama kaburi la mama ambapo alizikwa karibu miaka 21 iliyopita. Baada ya hapo tulipata breakfast na kuanza safari yetu ya kuelekea Dar mnamo karibu saa tano hivi.

Tuliwasili Dar kwenye mida ya saa kumi jioni hivi ila kutokana na foleni ilitufanya kuwasili home kwenye saa kumi na moja jioni. Kwa kweli safari hii ilikua ya mafanikio makubwa, ilikua ni adventure nzuri sana ambapo wote tuliokuwa kwenye msafara huu tunakubaliana nalo sote tulifurahi sana. Nina plan ya kurudia tena hii safari in the future ila this time nataka nisiwe na haraka ili nipate muda wa kulala kwenye mikoa yoyote hii ili nipata muda mzuri wa kuitembelea sio kama hii safari ambapo tuliingia na kupita tu. What an adventure, I love it!

 

 

Sydney Australia, 2004

Nikiwa Old Sydney Holiday Inn Hotel ambapo tulifikia.

 

Nilijikuta nime fall in love kwenye jiji mara tu nilipotua hapa, kimoyo moyo nikaanza plan ya my wedding here. Yap, this year ndoto yangu ikatimia atimaye 1st July 2004 kwenye very old church karibu kabisa na Sydney Harbor ndipo nilipofungia ndoa. Ilikua ni furaha tele hasa pale rafiki yangu mpendwa Stella alipokuja kwa ajili ya harusi akitokea Nairobi  pia baba ambaye alifika siku hiyo hiyo asubuhi akitokea kijijini Burere wilayani Rorya Musoma pamoja kuwa alikua amechoka sana baada ya kuwa angani zaidi ya masaa 24  ila alikua na furaha tele  pale aliponisindikiza na kunikabidhi. Ninafuraha sana kuona ndoto yangu ilikua kweli na kufanikisha kufunga ndoa kwenye jiji hili.

Mipango ya harusi haikuwa rahisi sana kutokana na kuishi sehemu tofauti na mji huu ila tulifanikiwa kumpata wedding planner ambaye alitufanikishia kila kitu na mambo yote ya harusi yalienda safi kabisa. Ila kitu cha kuchekesha ni kwamba mimi ndio kidogo nichemshe na kuchelewa kwenye wedding kisa eti nilikua natafuta sehemu ya kutengeneza kucha kwa style nayotaka. Tukaingia mitaani na rafiki yangu Stella wote tukiwa wageni na sehemu hii tulitafuta mpaka tukapata sehemu na kufanikiwa kutengeneza hizo kucha sasa kasheshe ilikua kurudi hotelini. Wakati tunaenda tulikua tuko busy bila kujali kuangalia tunakokwenda kumbe tulienda mbali sana wacha tupotee kichekesho kweli tukikumbuka. Ila baadae ilibidi tuchukue taxi kama nakumbuka vizuri ya kutufikisha hotelini ambapo nakuta mtu wa make up alishafika siku nyingi na hakuna time ya kufanya hivyo tena, la sivyo tutachelewa kabisa kanisani lol! Ikabidi nioge haraka haraka na kuvaa my dress na kupakwa vitu vidogo tu na kukimbilia kwenye gari na safari ya harusini ilianza yaani ilikua mchaka mchaka kweli, ila nashukuru mungu siku ilienda vizuri na kufanikisha harusi yangu. Kweli hatuachagi asili ya kuchelewa :))))

Tulikua na siku mbili hivi kabla hatujaanza safari yetu ya kuelekea kwenye honeymoon na kutumia muda huo kumtembeza baba around. Kitu kikubwa baba alikua anataka kufanya kabla ajaondoka ni kuwaona Kangaroo hivyo ikabidi tumpeleke Tarongo Park Zoo ambapo aliweza kuwaona na hata kuwashika hao Kangaroo alifurahi sana. Pia tulimpeleka Sydney Tower ambapo aliweza kuona Australia kwenye one room, ndani ya chumba kuna screen kubwa ya tv ambayo inaonyesha helicopter inayozunguka sehemu mbali mbali za utalii wa Australia. Tukiwa tumekaa kwenye viti ambavyo viko kama vya kwenye ndege huku head phone zikiwa masikioni kwetu kwa ajili ya kusikiliza. Wakati hiyo helicopter inakata kona au inachuka kidogo viti vyetu navyo vinafata basi utafikiri nasi tupo pamoja tunaizunguka nchi. Baada ya kumaliza na kutoka baba ndio akatutolea kali tulicheka sana anasema yaani kwa muda mfupi huu tumeweza kuzungukia Australia yote na kurudi kweli hawa wenzetu wametupita mbali sana, alifikiria kuwa katika safari hii nasi tulikua pamoja kwenye hii helicopter, mbavu zetu zilitaka kupasuka kwa kucheka ndio tulimuelewesha nae wacha acheke sana na kuamini kuwa hawa wenzetu ni hatari. Mpaka leo tukimkumbusha huwa anacheka sana

Niliahidi siku nyingi kuwa siku moja nikifanikiwa kwenda kwenye nchi za wenzetu lazima nimpeleke baba nae akapaone hii ilikua ni nafasi nzuri sana ya kumuonyesha dunia ya kwanza wanavyoishi. Baba alifurahi sana tena sana alikua anashangaa kila kitu alivyofika tu toka Airport anauliza  mbona hakuna watu barabarani, kesho yake asubuhi alishangaa sana kuona watu wengi kweli wakivuka barabara wakielekea makazini hapo akasema ok kumbe kuna watu barabarani yaani alikua anatufanya tucheke kila mara hiyo ilikua ni furaha yangu kubwa sana. Alifurahia kila kitu kuanzia usafi wa mji kila akitembea hakuona hata karatasi au vumbi maana Sydney ni moja ya mji msafi duniani ni kusafi sana.

Kwa upande wangu ulikua mwaka wa furaha sana niliweza kufunga ndoa kwenye jiji la my dream, pia kumuona baba yangu akiwa na furaha baada ya kuona nchi za wenzetu wa dunia ya kwanza walivyoendelea, kwangu mimi hiyo ni furaha kubwa sana.

 

 

Dar es Salaam, Aug.2011

With my brother Hassan and baby sis Tina at the Airport. Love this guys kupindukia

 

Safari hii ilikua ya mafanikio sana ambayo ilinipeleka mpaka kijijini Musoma. Nilikaa Dar kwa kipindi kifupi tu ila nilifurahi sana hasa kwa kupokelewa vizuri na wifi na kaka yangu, asanteni sana guys! Pia kitu kikubwa ambacho kilinifurahisha kuliko ni kuweza kufanikisha kilichonileta na pia kukutana na watoto wate wa Fatuma, I hope mama huko aliko alismile kwa furaha. Ni muda mrefu sana tangu sote tuwe pamoja karibu miaka 15 hivi na kuweza kufanikisha kitu muhimu kwetu sote. Kitu kingine ambacho this time nilienjoy sana ni misosi wifi yangu ni mtaalam kwa mambo haya basi si kupika, wacha tule, I wonder why niliongeza more than 3kg kwa chini ya siku 10 tu. Kwa ujumla this trip ni ya furaha kubwa..

 

 

Greenery Resort Hotel Khao Yai Thailand, July 2011

Greenery Resort

 

Pande hii ya Thailand hatujawahi kuufiki hii ilikua ni mara yetu ya kwanza. Tulikuja special kwa ajili ya Greenery Resort ambayo iko famous sana kwa ajili ya watoto na familia nzima kwa ujumla. Kuanzia makaribisho mpaka huduma yote ilikua nzuri sana. Amani & Malaika walifurahia sana hii ilikua special kwa ajili yao. Kitu cha kwanza walichoona tulivyofika tu ilikua ni hotel pool ambayo ilikua amazing. Pia walipata nafasi ya kutembelea The life park ambayo iko chini ya hotel ambayo ina michezo mingi sana ya watoto. Bila kusahau Elephant(Tembo) ride adventure ambayo ilikua awesome.

Hotel ina aina tofauti za room zikianzia za chini kabisa mpaka za juu, sisi tulichukua this time standard room. Muda wetu mwingi tulitumia nje kwenye michezo ya watoto hatukuona haja ya kuchukua room nzuri sana maana hatutaitumia sana zaidi ya kulala tu. Tulikaa hapa for 3 nights watoto walifurahi sana wanasema kuwa ni one of their favourite hotel this summer holiday.

Dar es Salaam, Feb.2011

Double Tree Hilton Hotel

 

Safari hii niliamua kwenda kupumzika kidogo peke yangu. Nilipata nafasi nzuri ya kukaa na mdogo wangu this time pia nilipata nafasi ya kumpeleka mdogo wangu wa mwisho kwenda kuangalia kaburi la mama huko Dodoma, kitu ambacho najivunia sana maana baada ya kufika na kuliona roho yangu ilisuhuzika mno nadhani huko aliko anasmile.

 

Dar es Salaam, 2010

With Kay & baby sis Tina at Golden Tulip Salsa night

 

Malaika alifurahia sana Tanzania maana this time alikua amekua kidogo anaelewa karibu kila kitu. Neno alilochukua sana ni Jambo, basi yeye kila mtu mweusi anamuita from Jambo maana anamuita mama yake ametokea Jambo eti ndio Tanzania, watoto bwana wanachekesha sana, basi akiitamka hiyo jambo yake sasa inaleta raha kweli.

 

Dar es Salaam, 2009

At Giraffe Hotel, Mange’s kitchen party

 

Kwa kusema ukweli pamoja na kusafiri nchi mbali mbali duniani siku ambayo najijua nakwenda Dar es Salaam huwa nakuwa na furaha tele maana kuna kitu ambacho huwa najisikia ambacho si cha kawaida ni furaha ilioje pale napoanza kutua kwenye kiwanja cha ndege cha Mwalimu Julius Nyerere huwa napata raha ya ajabu kuwa I’m home now. Kweli naamini usemi usemao nenda West or East Nyumbani ni Nyumbani.

 

Dar es Salaam, 2008 & 2009

Kempinski Hotel

 

Holiday ya kipindi hiki pekee ndio nilipata nafasi ya kukaa kwa muda mrefu nyumbani karibu miezi miwili hivi. Nakumbuka tangu niondoke Dar mwanzo wa mwaka 2002 sijawahi kurudi nyumbani na kukaa zaidi ya wiki 2, kipindi hiki kilikua so special kwangu niliweza fanya mambo mengi ambayo niko proud nayo. Pia niliweza kuwaleta Amani na Malaika kuja kuwatembelea ndugu zao wa huku na familia yangu kupata nafasi ya kuwaona watoto wao. Kitu kingine cha kupendeza ni dada zake Amani & Malaika walipata nafasi ya kuja tembelea Tanzania kwa mara ya kwanza wakitokea Australia. Kila mtu alikua happy kwa kweli….

 

 

Labua State Tower Hotel, Bangkok. July, 2011

The view of Bangkok from 63 bar

 

Awww…Lebua, hapa kila kitu 1st class kuanzia unavyoingia mpaka unavyotoka. Tulikaa Lebua State Tower Hotel for 3 days nilitamani zisiishe mapema. Our summer holiday inaendelea tumeingia hapa  tukitokea Phuket. Naweza sema I love everything about this hotel, huduma yake ni ya kukata na shoka. Unapoingia tu unasikia harufu ya upendo moja kwa moja kwanza hotel staff anakuja kukupokea kwa upendo wa hali ya juu na kukukaribisha kukaa na huku akiwa na file lako la kucheck inn,  ina maana alikua anawasubiri nyinyi specially na akimaliza kupata data zote anawasindikiza kwenye room yenu huku akiwapa maelezo muhimu kuhusu hotel with big smile.  Wamefanikiwa kumfanya  kila mteja kujisikia ni most important kwao nadhani hii  ni huduma ya 1st class kwa kweli. Kwa wale mtakaojikuta Bangkok please jaribu hii hotel nadhani utakubaliana nami. Very happy indeed until next time Labua State Tower Hotel, cheers!!!

Safiri na Zawadi