Dar es Salaam Feb, 2012

Breakpoint Posta with Blandina na kaka zake Festo and Gabu

Ilikua ni vizuri kukutana na Blandina, Festo na Gabu Langibori na kupata lunch pale Break Point Posta, ukiunganisha na story za miaka mingi pamoja na chakula kitamu basi mchana wetu ulienda vizuri sana. Walikua ni jirani zetu kipindi tunaishi Dodoma na nikaja kukutana nao kipindiĀ  nafanyia kazi Kigoma. Nakumbuka vizuri sana siku ambayo tumempoteza mama Blandina ndio alikuja kunipa taarifa kuwa mama yangu ametutoka. Utoto bwana nakumbuka alinipa news black & white kuwa mama yako amefariki wacha nikimbilie home huku nikiomba kuwa habari hii iwe si kweli lakini ndio hivyo ilikua imetokea. Kwa kweli tumetokea mbali sana, siku hii tuliongea mengi kweli. Baadae niliungana na mdogo wangu Tina na kwenda kuenjoy view pale Karambezi Sea Cliff Hotel na siku yangu ya kwanza bongo iliishia hapo. Hahahahaaaa…Bongo kuzuri bwana lol!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *