Lushoto, Tanzania Mar 2012. Part 1

Lushoto mountains

 

OMG! Sijui niseme nini I just love Lushoto, nilikua nakusikia tu toka kwa friends waliotokea huku kuwa ni kuzuri sana this time nikaamua nami niende. Ilichekesha sana some of friends waliniambia kuwa sitoweza fika huko maana barabara zake ni kazi sana kuendesha nikiwa ni mtaalam kwa maswala ya barabarani lol! Niliamua kujipanga mimi na wadogo zangu Tina na Flora tulianza safari yetu baada ya masaa matano tuliingia Lushoto. Kwa kweli ni pazuri sana tena sana na barabara yake ya kuingia huko bado ikiwa na hali nzuri ingawa ni ya enzi za mjerumani. Safari ilikua ni poa sana na tulikaa Lushoto kwa siku mbili, next time lazima nilete familia yangu huku Amani na Malaika watapapenda sana bila kusahau baba yao my hubby ambaye amezipenda sana picha za Lushoto! Kweli Tanzania yetu ni nzuri :)))))))

4 thoughts on “Lushoto, Tanzania Mar 2012. Part 1”

  1. woh! pazuri sana, ngoja nijipange this easter! nic ukumbusho kwa kweli! au nisubiri hadi uje! ah ah, say hi to your family!

  2. Kweli pazuri mi ndio nipo leo baridi kali jua tangu asubuhi hadi sasa ,mchana halijatoka, kuna ukungu mwingi looo Lushoto pazuri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *