You can’t believe this is Tanzania, yes ni Lushoto hiyo. Hii waterfall utaiona kwa mbali ukishaanza ingia tu kwenye mji wa Lushoto, sisi tuliamua kupatembelea siku yetu ya mwisho ambayo tulikua ndio tumeanza safari yetu ya kurudi Bongo. Kinachosikitisha ni kwamba eneo hili ni nzuri sana ila sijui serikali imelisahau maana wangepatengeneza vizuri na kuvutia watalii wengi tu na kuweza kuongezea kipato. Kwenye sehemu ya kuingilia eneo hili ambapo ndio unalipia shs. 2,000 kuweza kutelemka chini hali yake ni mbaya sana nilijaribu kwenda chooni kujisaidia mbona niliishia mlango ni pachafu ujawahi kuona. Inaonyesha ilikua ni hotel zamani sasa hivi pamekua kama gofu tu na linatumika kama vile sehemu ya kufundishia au sijui nini. Jamani eneo hili ni zuri sana kama wangeweza kujenga hotel nzuri tu au restaurant nzuri wangewavutia watalii wengi sana. Nikilinganisha na nchi nyingine nyingi ambazo nimepitia, kuna tofauti kubwa sana maana wenzetu wametupita sana na maswala ya utalii. Huku tukiwa na sehemu nzuri na nyingi ambazo zinavutia, nchi yetu inatakiwa kuamka na kuendeleza sehemu kama hizi na kukuza sekta hii ya utalii maana hakika nchi yetu ni nzuri na ya kuvutia.
Next day tuliamua kufanya tour kidogo around Lushoto na kujionea uzuri wa wilaya hii kunapendeza sana. Tulipata nafasi ya kutembelea Lushoto view hotel ambayo iko sehemu nzuri ila nilisikitika jinsi walivyoijenga na kuziba view ambayo ndio ingependezesha sana eneo hilo ambayo ni ya aina yake. Walitakiwa kuacha eneo kubwa wazi hata mtu akikaa restaurant aweze kuenjoy beautiful view lakini ukiwa ndani uwezi ona chochote kutokana na ujenzi walioufanya. Nilifurahia uamazi niliyofanya wa sisi kukaa Swiss Farm cottage ambapo kuna character ya aina yake ya kipekee ambapo kwangu mimi ni sifa kubwa sana kwa kuifanya sehemu kuwa nzuri zaidi.
Raha nyingine ya hii sehemu ni kuamka asubuhi na kufurahia sunrise ambayo inashine kwenye maua yenye unyevu unyevu uliotokana na baridi ya usiku ambapo ni baridi sana. Kama unavyoona picha ambazo nilipiga, asubuhi kunapendeza sana, I love this place kwa kweli. Nawashauri wanaokaa mijini ukitaka kupumzisha kichwa jaribu kwenda sehemu kama hizi ambapo utatuliza kichwa na utaenjoy ukimya na uzuri wake, huku ukijisoema vitabu. I love life like this ni za kipekee :))))))))
Jamani Swiss Farm Cottage ni nzuri sana, asante sana Adrienne kwa kunitambulisha nyumbani kwenu. Tulipapenda na kuzuri sana pia mama alitukaribisha na chocolate cake ambayo ilikua tamu ajabu wacha tule na kumaliza siku hiyo hiyo kesho yake tukaoda nyingine ya kuondoka nayo lol! Tulipapenda sana tena sana, cheers!!!!!:)))))
OMG! Sijui niseme nini I just love Lushoto, nilikua nakusikia tu toka kwa friends waliotokea huku kuwa ni kuzuri sana this time nikaamua nami niende. Ilichekesha sana some of friends waliniambia kuwa sitoweza fika huko maana barabara zake ni kazi sana kuendesha nikiwa ni mtaalam kwa maswala ya barabarani lol! Niliamua kujipanga mimi na wadogo zangu Tina na Flora tulianza safari yetu baada ya masaa matano tuliingia Lushoto. Kwa kweli ni pazuri sana tena sana na barabara yake ya kuingia huko bado ikiwa na hali nzuri ingawa ni ya enzi za mjerumani. Safari ilikua ni poa sana na tulikaa Lushoto kwa siku mbili, next time lazima nilete familia yangu huku Amani na Malaika watapapenda sana bila kusahau baba yao my hubby ambaye amezipenda sana picha za Lushoto! Kweli Tanzania yetu ni nzuri :)))))))
Nilifurahi kukutana na marafiki zangu kwa pamoja hapa na kupata lunch. Asanteni warembo kwa kufika na tulichekaje jamani, ndio raha ya Dar es Salaam hii jamani xoxo
Ilikua ni vizuri kukutana na Blandina, Festo na Gabu Langibori na kupata lunch pale Break Point Posta, ukiunganisha na story za miaka mingi pamoja na chakula kitamu basi mchana wetu ulienda vizuri sana. Walikua ni jirani zetu kipindi tunaishi Dodoma na nikaja kukutana nao kipindi nafanyia kazi Kigoma. Nakumbuka vizuri sana siku ambayo tumempoteza mama Blandina ndio alikuja kunipa taarifa kuwa mama yangu ametutoka. Utoto bwana nakumbuka alinipa news black & white kuwa mama yako amefariki wacha nikimbilie home huku nikiomba kuwa habari hii iwe si kweli lakini ndio hivyo ilikua imetokea. Kwa kweli tumetokea mbali sana, siku hii tuliongea mengi kweli. Baadae niliungana na mdogo wangu Tina na kwenda kuenjoy view pale Karambezi Sea Cliff Hotel na siku yangu ya kwanza bongo iliishia hapo. Hahahahaaaa…Bongo kuzuri bwana lol!