Raha nyingine ya hii sehemu ni kuamka asubuhi na kufurahia sunrise ambayo inashine kwenye maua yenye unyevu unyevu uliotokana na baridi ya usiku ambapo ni baridi sana. Kama unavyoona picha ambazo nilipiga, asubuhi kunapendeza sana, I love this place kwa kweli. Nawashauri wanaokaa mijini ukitaka kupumzisha kichwa jaribu kwenda sehemu kama hizi ambapo utatuliza kichwa na utaenjoy ukimya na uzuri wake, huku ukijisoema vitabu. I love life like this ni za kipekee :))))))))
Jamani Swiss Farm Cottage ni nzuri sana, asante sana Adrienne kwa kunitambulisha nyumbani kwenu. Tulipapenda na kuzuri sana pia mama alitukaribisha na chocolate cake ambayo ilikua tamu ajabu wacha tule na kumaliza siku hiyo hiyo kesho yake tukaoda nyingine ya kuondoka nayo lol! Tulipapenda sana tena sana, cheers!!!!!:)))))
OMG! Sijui niseme nini I just love Lushoto, nilikua nakusikia tu toka kwa friends waliotokea huku kuwa ni kuzuri sana this time nikaamua nami niende. Ilichekesha sana some of friends waliniambia kuwa sitoweza fika huko maana barabara zake ni kazi sana kuendesha nikiwa ni mtaalam kwa maswala ya barabarani lol! Niliamua kujipanga mimi na wadogo zangu Tina na Flora tulianza safari yetu baada ya masaa matano tuliingia Lushoto. Kwa kweli ni pazuri sana tena sana na barabara yake ya kuingia huko bado ikiwa na hali nzuri ingawa ni ya enzi za mjerumani. Safari ilikua ni poa sana na tulikaa Lushoto kwa siku mbili, next time lazima nilete familia yangu huku Amani na Malaika watapapenda sana bila kusahau baba yao my hubby ambaye amezipenda sana picha za Lushoto! Kweli Tanzania yetu ni nzuri :)))))))
Nilikwenda msalimia my friend Christina ofisini kwake
Another friend of mine
And another one, she's so cute
And another one
I met them outside Chef Pride restaurant and invited them to join me for lunch. OMG! They brightened my day
My new friends
They are so cute!
Maggie
My baby sis Tina with Maggie
My baby sis Tina
At Karambezi Sea Cliff Hotel with Maggie
Karambezi Sea Cliff with baby sis Tina
Karambezi Sea Cliff Hotel
Karambezi Sea Cliff Hotel
My salad
At Karambezi with friends Salome, Kay, Sharon, Maggie and baby sis Tina
At Karambezi with friends Salome, Kay, Sharon, Maggie and baby sis Tina
Salome
Sharon, Salome, Kay and Maggie
Tina, Salome, Kay and Sharon
With Tina, Kay, Sharon and Salome
Sea Cliff Hotel
Sea Cliff Hotel
Sea Cliff Hotel
Sea Cliff Hotel
Sea Cliff Hotel
Protea Apartment
Salome
Salome
With Salome
Nilifurahi kukutana na marafiki zangu kwa pamoja hapa na kupata lunch. Asanteni warembo kwa kufika na tulichekaje jamani, ndio raha ya Dar es Salaam hii jamani xoxo
Breakpoint Posta with Blandina na kaka zake Festo and Gabu
Was yummy! Mambo ya Karambezi Sea Cliff Hotel
Sea Cliff Hotel
Karambezi Sea Cliff Hotel
My lovely mdogo Tina at Karambezi Sea Cliff Hotel
My second day in Bongo bado sijaanza kula chakula kitamu, wait and see the last day...hahahaaaa...
Breakpoint Posta with Blandina na kaka zake Festo and Gabu
Ilikua ni vizuri kukutana na Blandina, Festo na Gabu Langibori na kupata lunch pale Break Point Posta, ukiunganisha na story za miaka mingi pamoja na chakula kitamu basi mchana wetu ulienda vizuri sana. Walikua ni jirani zetu kipindi tunaishi Dodoma na nikaja kukutana nao kipindi nafanyia kazi Kigoma. Nakumbuka vizuri sana siku ambayo tumempoteza mama Blandina ndio alikuja kunipa taarifa kuwa mama yangu ametutoka. Utoto bwana nakumbuka alinipa news black & white kuwa mama yako amefariki wacha nikimbilie home huku nikiomba kuwa habari hii iwe si kweli lakini ndio hivyo ilikua imetokea. Kwa kweli tumetokea mbali sana, siku hii tuliongea mengi kweli. Baadae niliungana na mdogo wangu Tina na kwenda kuenjoy view pale Karambezi Sea Cliff Hotel na siku yangu ya kwanza bongo iliishia hapo. Hahahahaaaa…Bongo kuzuri bwana lol!
Nyoka huyu alikuja msalimia mume wangu alipokua kijijini 2008. Alikua anadonoa donoa kiatu cha Mr. fikiria kama angekuwa hana viatu mbona ingekuwa balaa
Tulijenga kwa muda wa masaa 5 na nusu tu
Kaburi la mdogo wangu Michael
Ujenzi wa kaburi ukiendelea
Barabara ya kijiji
Burere village
Harakati za kukausha samaki kijijini
Sehemu wanayokaushia samaki
Hello Tina
Dala dala boat za huko
Pembeni ya ziwa
Tina kwa raha zake
Wavuvi wakiwa kazini
Tina huyo kwa raha zake kijijini
Flora akiwa kijijini
Kijijini Burere
Love this pic, kijijini Burere
Tina choka kabisa
Mawe haya yanapatikana tu ukanda wa ziwa Victoria
Kijijini Burere
Around kijiji
Around kijiji
Flora kwa raha zake
Tina akiwa Lake Victoria
Look! I'm flying
View ya namna hii inapatikana tu Burere
Wewee...baby sis Tina
Flora kijijini Burere
Jamani mnaona hiyo view? Flora kwa raha zake
Burere
Tina kijijini Burere
Tina akiwa ziwani. Ni mara yake ya kwanza kukanyaga maji ya Lake Victoria
Flora akifurahi na watoto
Garden ya baba kijijini yuko karibu sana na ziwa
Kijijini Burere
Super model toka Burere hahaaa..Flora
Mbona kijiji kilikoma hahahaa...Flora
Flora akifurahia view ya lake
My baby sis Tina
Tina akienjoy upepo wenye afya kijijini
Miguu ya warembo Tina na Flora kijijini, si vumbi hilo
Kaburi la mdogo wangu Michael ambalo tumeenda jenga
Kijijini Burere
Miguu ya masista du kijijini, mbona watanimaliza lol! Flora na Tina
Mrembo Flora kijijini, Aug. 2011
Mrembo Tina akiwa kijijini Burere, Aug. 2011
Mvuvi wa samaki kijijini Burere, jamani sijui huyu Sangara au Sato
Wavuvi wa samaki huko kijijini
Rorya, mdogo wangu kutoka kwa mama mwingine huko kijijini
Watoto kijijini Burere
Watoto kijijini waki enjoy soda. Mume wangu alipiga picha hii 2008
The bridge kwenye river Mara, inasemekana mto huu una mambo wengi na hatari sana
Burere village
Sunset ya nguvu kijijini Burere
Sunset kijini Burere
Sunset in Burere Village
Kijijini burere, mume wangu alipokua huko 2008
On the way to Musoma 2003
Kituo cha basi on the way to Musoma 2003
Mume wangu alimfurahia sana huyu mama, on the way to Musoma 2003
Tulipiga picha hii on the way to Musoma 2003
What a beautiful picture, tulipiga picha hii Musoma 2003
The view of Musoma
Niko pembeni ya Lake Victoria, Musoma 2003
Nimefika hapa kwa mara ya kwanza 2000 ambapo niliamua kwenda kuangalia nilikotoka. Baba alirudi kwao the end of 90’s, na kuweka makazi yake. Naambiwa kuwa nilishaletwa hapa nikiwa na miaka miwili. Kwa sasa baba anaishi kijiji cha Burere, wilayani Rorya mkoani Mara. Kijiji kikiwa karibu sana na Kenya yaani wanasema ukiwa hapa unaweza tembea tu kuingia nchi hii ya Kenya, kwa kweli ni mbali sana tena sana. Ukitaka kuja huku inabidi ujipange kisawa sawa. Tangu mwaka 2000 nimefanikiwa kurudi kama mara mbili hivi zaidi. Ila mara zote hizo sijafanikiwa sana kuzunguka kijijini kwa sababu ya kutokua na muda wa kutosha. Nimekua naingia jioni na kuondoka asubuhi, hata ndugu zangu wengine hapo hawanijui kabisa wananisikia tu. Ila nitapanga siku moja niende ili nipeleke watoto wangu wakapaone nina uhakika watapapenda sana kama baba yao alivyopapenda.
Mwaka huu 2003 tulikua tumetokea Mwanza ambapo tulifika kwa njia ya ndege na kuchukua basi ambalo lilitufikisha Musoma. Mume wangu alifurahi sana kuona mazingira ya barabarani na kupata nafasi ya kushangaa shangaa maisha ya maeneo haya.
Kwa kusema ukweli kijiji hiki ni kizuri sana, mume wangu alipofika hapa hiyo 2008 alishangaa sana uzuri wa kijiji hiki hasa view ya lake Victoria inapendeza kweli. Anasema kuwa kuna fresh air ya ajabu huku ambayo ni adimu sana kuipata. Nakubaliana nae hapa kweli si mchezo na uzuri wake ebu jionee mwenyewe jinsi panavyopendeza.
Mume wangu alipata nafasi ya kuzungukia kijiji na kupiga picha nyingi tu maana alikaa siku nne kwa hiyo alikua na muda wa kutosha kuenjoy fresh air. Kitu kingine kilichomfurahisha sana ni pale watoto walivyokua wakimfuata kila sehemu huku wakimuita mzungu, mzungu akikumbuka huwa anacheka sana. Alifurahi sana kwa kipindi chote alichokua hapa ila anasema kulikua hakuna shower eti alikua anatumia kikombe na ndoo kujimwagia maji anasema laiti kungekuwa na shower. Kweli mzungu aachi asili yake ila kila kitu kingine alipenda sana na alifurahi kweli nao wanakijiji walimfurahia sana kupata mgeni kama yeye.
Aug. mwaka huu nikiwa nimeongozana na ndugu zangu tulifika kijijini kwa njia ya gari ambapo tulidrive toka Dar. Uwezi amini kwenda na kurudi tulitumia zaidi ya kilomita 3000, hakika huku kwetu ni mbali haswa. Tulikuja kwa madhumuni ya kujenga kaburi la mdogo wetu Michael tunashukuru tuliweza kufanikisha hii shughuli kwa haraka na kuweza kurudi Mwanza siku hiyo hiyo. Hatukuwa na muda mrefu maana kaka yangu na wadogo zangu walitakiwa kurudi kazini pia mimi nilitakiwa kurudi kwa watoto wangu ambao walikua karibu ya kufungua shule.
Kwa ujumla nchi yetu Tanzania ni nzuri sana, kuna vijiji vingi ambavyo vina uzuri wa hali ya juu kama serikali yetu ingevitengeneza na kuweka mahitaji muhimu kama vile maji safi, hospitali, shule nzuri, umeme na mahitaji mengi muhimu watu wengi wangekuwa na moyo wa kurudi kuishi huko. Kwa mfano kijiji hiki ni kizuri sana kingeweza kuvutia watalii wengi kama kungekuwa na hayo mahitaji nadhani watu wangeweza hata kujenga nyumba za holiday watu wawe wanaenda pumzika huko maana kwa hii view watalii wangekuja tu.
Flora yuko hoi mafua yamekamata haswa na safari ndio kwanza imeanza
Tumefika Dodoma
Dodoma
Baby sis akiwa Calman Cafe, Dodoma
Flora akiwa Calman Cafe Dodoma
Tukianza kuingia Singida
Beautiful sunset ndani ya Singida
Beautiful Sunset, Singida
Singida
Tulisimama hapa kwa ajili ya kujisaidia
Sunset in Singida
Tukianza safari ya kuelekea Shinyanga
Kutoka Singida kuelekea Shinyanga
Hotelini Mwanza
Mwanza
Tulikumbana na huu ukungu wakati tunatoka Mwanza kuelekea Musoma
Ukungu Mwanza ilikua kazi sana kuendesha gari hakuna kuona
Sunrise Mwanza
Beautiful sunrise in Mwanza
Sunrise Mwanza
Mwanza
Uswahilini Mwanza
Tukiwa tunaingia Shinyanga
Njiani tukiingia Shinyanga
Tukielekea Shinyanga
Njiani kuelekea Shinyanga
Shinyanga
Shinyanga
Shinyanga
Shinyanga
Shinyanga
Shinyanga
Tukitokea Shinyanga kuelekea Singida
Njiani tukitokea Shinyanga kuelekea Singida
Nyumba za vijiji Shinyanga
Kuelekea Singida
Wamasai wakiwa wamevalia kuelekea Gulio karibu na Singida
Njiani tulikutana na gulio karibu na Singida
Gulio karibu na Singida
Mapori ya Singida
Njiani tukitokea Singida kuelekea Dodoma
Njiani kuelekea Dodoma
Tukiikaribia milima ya Sekenke, Singida
Tukiivuta milima ya Sekenke
Milima ya Sekenke, Singida
Tukiwa ndani ya milima ya Sekenke
Tukiwa Senkeke
Milima ya Sekenke
Sekenke
Karibu tukimaliza milima ya Sekenke
Kuna kona kali sana
Kuna kona hatari sana
Tumemaliza salama milima hii ya Sekenke
Tunaingia Singida
Singida
Ili ziwa dogo liko Singida
Tumeanza safari ya kuelekea Dodoma
Sunset Singida
Safari ya Dodoma imeanza
Veta Hotel Dodoma
Veta Hotel Dodoma
Veta Hotel Dodoma
Veta Hotel Dodoma
Gari iliyotupeleka na kuturudisha na kumaliza kilomita zaidi ya 3,000
Veta Hotel Dodoma
Hotel tuliyofikia Dodoma
Dodoma
Bungeni Dodoma
Dodoma
Tulikula chakula kitamu sana hapa, Dodoma
Tulikua tunajiuliza ili gari limepambwa kwa ajili gani haswa tulikosa jibu je wewe unaweza tusaidia. Tulikumbana nalo Dodoma
Group nzima ya safari yetu, kutoka kushoto Hassan, Flora, Hamis na Tina. Dodoma
Nikiwa na kaka Hassan na mdogo Tina, Dodoma
With my kaka nadeka. Dodoma
Love u guys, mwaah!
Tumefanana ehe!
Nyumba vijiji Dodoma
Tukielekea Morogoro, Acacia Tree
Acacia Tree
Tumeanza kuona milima ya Morogoro
On the way to Morogoro
Tumeingia Morogoro
Morogoro
Morogoro
Milima ya Uruguru
Milima ya Uruguru, Morogoro
Milima ya Uruguru, Morogoro
Nikiwa mwanza 2003
Mwanza 2003
The view of the lake from Tilapia Hotel Mwanza 2003
The view of the Lake Victoria
The view from Tilapia Hotel, Mwanza
Safari hii ilikua ni mara yangu ya tatu kuja kwenye jiji hili, tofauti ni kwamba safari zote mbili za mwanzo nilikuja kwa njia ya anga na sio barabara. Hii ilikua ni adventure nzuri sana kwangu na wote ambao tulikua kwenye safari hii, tulianzia safari yetu Dar kupitia Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga then Mwanza. Ni safari ndefu sana ambayo ilikua inatupeleka kijiji cha Burere, wilaya ya Rorya huko Musoma. Tulijumlasha kilomita zote na kupata zaidi ya kilomita 3,000 tulitumia kwenda na kurudi Dar. Safari hii ilituchukua siku nne ambapo tuliweza maliza kilomita zote hizo, tunamshukuru mungu tulisafiri salama na kurudi salama na safari ilikua ya mafanikio makubwa ingawa tulichoka sana.
Madhumuni ya safari hii ilikua ni kwenda kujenga kaburi la mdogo wetu ambaye alifariki karibu miaka 10 iliyopita. Safari hii ilitujumuisha watoto wote wa Fatuma yaani marehemu mama akiwepo kaka yetu mkubwa Hassan, mimi, mdogo wangu aliyenifuata Obuya ambaye tulimpitia Mwanza ndipo anapoishi na mdogo wetu wa mwisho Tina. Pia tulikua na ndugu yetu Flora pamoja na Hamis ambaye alitusaidia sana kwenye maswala ya gari pamoja na udereva, ambapo walikua wanasaidiana na Hassan.
Tulianza safari yetu kutokea Dar saa kumi na mbili asubuhi na tuliwasili Moro mida ya saa 3 asubuhi hivi. Ila tulichelewa kutoka Moro kuelekea Dodoma kwa sababu ya tatizo dogo la gari ambapo ilituweka mpaka mchana ndipo tulianza safari yetu ya kuelekea Dodoma. Tuliwasili Dodoma kwenye mida ya saa tisa jioni hivi baada ya kujisaidia na kupata lunch tulianza safari yetu ya kuelekea Singida. Tuliwasili Singida kwenye mida ya saa kumi na mbili jioni hivi hapa hatukukaa kabisa baada ya kucheki gari na kujisaidia tuliendelea na safari yetu ya Shinyanga. Tuliwasili Shinyanga usiku kwenye mida ya saa nne hivi pia hatukupoteza muda baada ya kucheki gari na kujaza mafuta tulianza safari yetu ya Mwanza, tuliingia kwenye jiji hili kwenye mida ya saa saba usiku tukiwa hoi, choka kabisa na kuamua kulala hapa.
Asubuhi ya saa kumi na mbili tulianza safari yetu ya kuelekea Musoma ambapo tulipitiliza moja kwa moja kuelekea kijijini bila kuingia Musoma mjini. Tuliwasili kijijini kwenye mida ya saa sita hivi na kufanya shughuli iliyotupeleka na kumaliza kwenye saa kumi na mbili jioni na kuanza safari yetu ya kurudi Mwanza, tuliingia Mwanza kwenye saa nne usiku hivi baada ya kutafuta msosi na kula maana tulikua na njaa sana toka tule asubuhi ya siku hiyo hatukula chochote tulielekea hotelini na kulala. Kesho yake asubuhi tulianza safari yetu ila kabla ya kutoka mjini gari lilileta matatizo kidogo ikabidi tulipeleke garage, ilituchukua mpaka mida ya mchana hivi kabla ya kuanza safari yetu ya kuelekea Shinyanga.
Tulianza safari yetu ya kuelekea Dar kupitia Shinyanga, Tabora lakini si mjini, Singida, Dodoma, Moro then Dar. Safari hii tuliamua kulala Dodoma ambapo tulifika hapa kwenye saa mbili au tatu usiku hivi. Tulipata nafasi kwenye Veta hotel ambayo kwa ujumla ilikua nzuri. Kesho yake asubuhi tulielekea kwenye makaburi ya Kizota kwenda kutizama kaburi la mama ambapo alizikwa karibu miaka 21 iliyopita. Baada ya hapo tulipata breakfast na kuanza safari yetu ya kuelekea Dar mnamo karibu saa tano hivi.
Tuliwasili Dar kwenye mida ya saa kumi jioni hivi ila kutokana na foleni ilitufanya kuwasili home kwenye saa kumi na moja jioni. Kwa kweli safari hii ilikua ya mafanikio makubwa, ilikua ni adventure nzuri sana ambapo wote tuliokuwa kwenye msafara huu tunakubaliana nalo sote tulifurahi sana. Nina plan ya kurudia tena hii safari in the future ila this time nataka nisiwe na haraka ili nipate muda wa kulala kwenye mikoa yoyote hii ili nipata muda mzuri wa kuitembelea sio kama hii safari ambapo tuliingia na kupita tu. What an adventure, I love it!
With my brother Hassan and baby sis Tina at the Airport. Love this guys kupindukia
With my brother Hassan, nasema asante sana kaka.
With my brother Hassan
With my brother Hassan, mi penda sana weye
The family
With my brother Hassan and baby sis Tina at the Airport. Love this guys kupindukia
At the Airport with my brother Hassan & baby sis Tina, love u sana sana guys
My wifi Mariam, love u Mamu sana tu.
Mambo ya siku ya Eid hayo, too bad nilikua naondoka baada ya masaa machache hapo
With my old friend Blandina tangu tukiwa 11yrs old
Southern beach Kigamboni
Kipepeo beach Kigamboni
With my old friend Sarah since the 90's
Flora
Masaki Sea Cliff
Masaki Sea Cliff
Sea Cliff
Happy Flora
Flora at Sea Cliff Hotel
Flora wangu huyo
Sea Cliff Hotel
The view from Sea Cliff Hotel
Aawww..Mama Doris what a strong woman, tunakupenda sana.
With Alice, Agnes & Emmy
With Alice, Agnes & Emmy
Mdogo wangu huyo pendeza weye
Baby sis Tina
Watengenezaji wa BBQ
Mambo ya Kiti Moto hayo
Linda's farewell party at Uncle Gondwe & Aunt Sarah place
Mambo ya BBQ
At Linda's farewell party
Uncle Gondwe & Aunt Sarah place
Uncle Gondwe & Aunt Sarah place
Jimmy, Tina & Queen
Warembo wetu
Yummy!
Mambo ya wifi yangu hayo
Muda wa kufuturu huo
Mambo ya kufuturu hayo kwa mamu
Safari hii ilikua ya mafanikio sana ambayo ilinipeleka mpaka kijijini Musoma. Nilikaa Dar kwa kipindi kifupi tu ila nilifurahi sana hasa kwa kupokelewa vizuri na wifi na kaka yangu, asanteni sana guys! Pia kitu kikubwa ambacho kilinifurahisha kuliko ni kuweza kufanikisha kilichonileta na pia kukutana na watoto wate wa Fatuma, I hope mama huko aliko alismile kwa furaha. Ni muda mrefu sana tangu sote tuwe pamoja karibu miaka 15 hivi na kuweza kufanikisha kitu muhimu kwetu sote. Kitu kingine ambacho this time nilienjoy sana ni misosi wifi yangu ni mtaalam kwa mambo haya basi si kupika, wacha tule, I wonder why niliongeza more than 3kg kwa chini ya siku 10 tu. Kwa ujumla this trip ni ya furaha kubwa..
Nilipokutana na rafiki mpya tukiwa maeneo ya Sinza
Maeneo ya Mabibo nimekaa huku jamani
Level 8 Kempinski Hotel
Baby sis Tina at Kempinski Hotel
Dar by night
Posta by night
The view from level 8 Kempinski Hotel
Night out at Kempinski Hotel
The view from Bongoyo Island
At Bongoyo Island beach
At Bongoyo Island beach
Tina & Flora at Bongoyo Island
Beautiful beach, Bongoyo Island
Bongoyo Island, beautifu beach with white sand
Bongoyo Island
At Bongoyo Island
Bongoyo Island
Bongoyo Island, beautiful beach
My baby sis Tina
Boat iliyotufikisha beach
Flora akiwa kwenye boat ndogo inayotufikisha Bongoyo Island kabisa
Baby sis Tina
The Bongoyo Island
The Bongoyo Island
Flora in the boat
Near Yatch Club
The view of Masaki from the boat
With baby sis Tina at Slipway on our way to Bongoyo
Tina & Flora at Slipway on our way to Bongoyo Island
With baby sis Tina at Kempinski Hotel
Kempinski Hotel
Kipepeo Village Beach Kigamboni
Nikiwa Kipepeo Village Kigamboni
Flora at Kipepeo Village Kigamboni
At Kipepeo Village Kigamboni with vijana Deborah, Tina & Flora
At Kipepeo Village Kigamboni
Safari hii niliamua kwenda kupumzika kidogo peke yangu. Nilipata nafasi nzuri ya kukaa na mdogo wangu this time pia nilipata nafasi ya kumpeleka mdogo wangu wa mwisho kwenda kuangalia kaburi la mama huko Dodoma, kitu ambacho najivunia sana maana baada ya kufika na kuliona roho yangu ilisuhuzika mno nadhani huko aliko anasmile.
With Kay & baby sis Tina at Golden Tulip Salsa night
Malaika
Malaika with her cousin Mikiko(Imani)
At Slipway
Malaika with Masai at Kipepeo Beach
Malaika at Kipepeo Beach
Ndani ya kivuko
Watu wakitoka ndani ya kivuko
Kivuko kinachovusha watu kuelekea na kutoka Kigamboni
Kivuko
With Malaika at Marry Brown
Southern Beach Kigamboni
At Slipway
Nikiwa na Malaika Slipway
Malaika & Ryan tukiwa lunch pale Rose Garden
Kigamboni feri
Malaika na Kifaranga
Tembelea ndugu na jamaa, Malaika akifurahia Kifaranga
Southern Beach Kigamboni
Malaika akicheza Kipepeo beach
Malaika wangu akiwa Kipepeo beach
Malaika akifurahia beach Kipepeo
Malaika at Kipepeo beach Kigamboni. Beautiful beach
Malaika at Slipway
At Slipway
At Slipway
Malaika akiwa Slipway
Nilikwenda msalimia rafiki Christina ofisini kwake pale Masaki
Mdogo wangu Tina, Check point posta for lunch
Malaika at Jaki place
Malaika with her bibi mkubwa at Jaki place
With Malaika ndio kwanza tumewasili
With Malaika & Flora, Airport tukiwa ndio tumewasili
Golden Tulip Hotel, Theo akinifundisha kucheza Salsa.
With Kay & mdogo wangu Tina. Salsa night at Golden Tulip Hotel
Bongo by night
With my old friend Mage toka Sec School
Malaika alifurahia sana Tanzania maana this time alikua amekua kidogo anaelewa karibu kila kitu. Neno alilochukua sana ni Jambo, basi yeye kila mtu mweusi anamuita from Jambo maana anamuita mama yake ametokea Jambo eti ndio Tanzania, watoto bwana wanachekesha sana, basi akiitamka hiyo jambo yake sasa inaleta raha kweli.