Raha nyingine ya hii sehemu ni kuamka asubuhi na kufurahia sunrise ambayo inashine kwenye maua yenye unyevu unyevu uliotokana na baridi ya usiku ambapo ni baridi sana. Kama unavyoona picha ambazo nilipiga, asubuhi kunapendeza sana, I love this place kwa kweli. Nawashauri wanaokaa mijini ukitaka kupumzisha kichwa jaribu kwenda sehemu kama hizi ambapo utatuliza kichwa na utaenjoy ukimya na uzuri wake, huku ukijisoema vitabu. I love life like this ni za kipekee :))))))))
Jamani Swiss Farm Cottage ni nzuri sana, asante sana Adrienne kwa kunitambulisha nyumbani kwenu. Tulipapenda na kuzuri sana pia mama alitukaribisha na chocolate cake ambayo ilikua tamu ajabu wacha tule na kumaliza siku hiyo hiyo kesho yake tukaoda nyingine ya kuondoka nayo lol! Tulipapenda sana tena sana, cheers!!!!!:)))))
OMG! Sijui niseme nini I just love Lushoto, nilikua nakusikia tu toka kwa friends waliotokea huku kuwa ni kuzuri sana this time nikaamua nami niende. Ilichekesha sana some of friends waliniambia kuwa sitoweza fika huko maana barabara zake ni kazi sana kuendesha nikiwa ni mtaalam kwa maswala ya barabarani lol! Niliamua kujipanga mimi na wadogo zangu Tina na Flora tulianza safari yetu baada ya masaa matano tuliingia Lushoto. Kwa kweli ni pazuri sana tena sana na barabara yake ya kuingia huko bado ikiwa na hali nzuri ingawa ni ya enzi za mjerumani. Safari ilikua ni poa sana na tulikaa Lushoto kwa siku mbili, next time lazima nilete familia yangu huku Amani na Malaika watapapenda sana bila kusahau baba yao my hubby ambaye amezipenda sana picha za Lushoto! Kweli Tanzania yetu ni nzuri :)))))))
Nilifurahi kukutana na marafiki zangu kwa pamoja hapa na kupata lunch. Asanteni warembo kwa kufika na tulichekaje jamani, ndio raha ya Dar es Salaam hii jamani xoxo
Ilikua ni vizuri kukutana na Blandina, Festo na Gabu Langibori na kupata lunch pale Break Point Posta, ukiunganisha na story za miaka mingi pamoja na chakula kitamu basi mchana wetu ulienda vizuri sana. Walikua ni jirani zetu kipindi tunaishi Dodoma na nikaja kukutana nao kipindi nafanyia kazi Kigoma. Nakumbuka vizuri sana siku ambayo tumempoteza mama Blandina ndio alikuja kunipa taarifa kuwa mama yangu ametutoka. Utoto bwana nakumbuka alinipa news black & white kuwa mama yako amefariki wacha nikimbilie home huku nikiomba kuwa habari hii iwe si kweli lakini ndio hivyo ilikua imetokea. Kwa kweli tumetokea mbali sana, siku hii tuliongea mengi kweli. Baadae niliungana na mdogo wangu Tina na kwenda kuenjoy view pale Karambezi Sea Cliff Hotel na siku yangu ya kwanza bongo iliishia hapo. Hahahahaaaa…Bongo kuzuri bwana lol!
Nimefika hapa kwa mara ya kwanza 2000 ambapo niliamua kwenda kuangalia nilikotoka. Baba alirudi kwao the end of 90’s, na kuweka makazi yake. Naambiwa kuwa nilishaletwa hapa nikiwa na miaka miwili. Kwa sasa baba anaishi kijiji cha Burere, wilayani Rorya mkoani Mara. Kijiji kikiwa karibu sana na Kenya yaani wanasema ukiwa hapa unaweza tembea tu kuingia nchi hii ya Kenya, kwa kweli ni mbali sana tena sana. Ukitaka kuja huku inabidi ujipange kisawa sawa. Tangu mwaka 2000 nimefanikiwa kurudi kama mara mbili hivi zaidi. Ila mara zote hizo sijafanikiwa sana kuzunguka kijijini kwa sababu ya kutokua na muda wa kutosha. Nimekua naingia jioni na kuondoka asubuhi, hata ndugu zangu wengine hapo hawanijui kabisa wananisikia tu. Ila nitapanga siku moja niende ili nipeleke watoto wangu wakapaone nina uhakika watapapenda sana kama baba yao alivyopapenda.
Mwaka huu 2003 tulikua tumetokea Mwanza ambapo tulifika kwa njia ya ndege na kuchukua basi ambalo lilitufikisha Musoma. Mume wangu alifurahi sana kuona mazingira ya barabarani na kupata nafasi ya kushangaa shangaa maisha ya maeneo haya.
Kwa kusema ukweli kijiji hiki ni kizuri sana, mume wangu alipofika hapa hiyo 2008 alishangaa sana uzuri wa kijiji hiki hasa view ya lake Victoria inapendeza kweli. Anasema kuwa kuna fresh air ya ajabu huku ambayo ni adimu sana kuipata. Nakubaliana nae hapa kweli si mchezo na uzuri wake ebu jionee mwenyewe jinsi panavyopendeza.
Mume wangu alipata nafasi ya kuzungukia kijiji na kupiga picha nyingi tu maana alikaa siku nne kwa hiyo alikua na muda wa kutosha kuenjoy fresh air. Kitu kingine kilichomfurahisha sana ni pale watoto walivyokua wakimfuata kila sehemu huku wakimuita mzungu, mzungu akikumbuka huwa anacheka sana. Alifurahi sana kwa kipindi chote alichokua hapa ila anasema kulikua hakuna shower eti alikua anatumia kikombe na ndoo kujimwagia maji anasema laiti kungekuwa na shower. Kweli mzungu aachi asili yake ila kila kitu kingine alipenda sana na alifurahi kweli nao wanakijiji walimfurahia sana kupata mgeni kama yeye.
Aug. mwaka huu nikiwa nimeongozana na ndugu zangu tulifika kijijini kwa njia ya gari ambapo tulidrive toka Dar. Uwezi amini kwenda na kurudi tulitumia zaidi ya kilomita 3000, hakika huku kwetu ni mbali haswa. Tulikuja kwa madhumuni ya kujenga kaburi la mdogo wetu Michael tunashukuru tuliweza kufanikisha hii shughuli kwa haraka na kuweza kurudi Mwanza siku hiyo hiyo. Hatukuwa na muda mrefu maana kaka yangu na wadogo zangu walitakiwa kurudi kazini pia mimi nilitakiwa kurudi kwa watoto wangu ambao walikua karibu ya kufungua shule.
Kwa ujumla nchi yetu Tanzania ni nzuri sana, kuna vijiji vingi ambavyo vina uzuri wa hali ya juu kama serikali yetu ingevitengeneza na kuweka mahitaji muhimu kama vile maji safi, hospitali, shule nzuri, umeme na mahitaji mengi muhimu watu wengi wangekuwa na moyo wa kurudi kuishi huko. Kwa mfano kijiji hiki ni kizuri sana kingeweza kuvutia watalii wengi kama kungekuwa na hayo mahitaji nadhani watu wangeweza hata kujenga nyumba za holiday watu wawe wanaenda pumzika huko maana kwa hii view watalii wangekuja tu.
Safari hii ilikua ni mara yangu ya tatu kuja kwenye jiji hili, tofauti ni kwamba safari zote mbili za mwanzo nilikuja kwa njia ya anga na sio barabara. Hii ilikua ni adventure nzuri sana kwangu na wote ambao tulikua kwenye safari hii, tulianzia safari yetu Dar kupitia Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga then Mwanza. Ni safari ndefu sana ambayo ilikua inatupeleka kijiji cha Burere, wilaya ya Rorya huko Musoma. Tulijumlasha kilomita zote na kupata zaidi ya kilomita 3,000 tulitumia kwenda na kurudi Dar. Safari hii ilituchukua siku nne ambapo tuliweza maliza kilomita zote hizo, tunamshukuru mungu tulisafiri salama na kurudi salama na safari ilikua ya mafanikio makubwa ingawa tulichoka sana.
Madhumuni ya safari hii ilikua ni kwenda kujenga kaburi la mdogo wetu ambaye alifariki karibu miaka 10 iliyopita. Safari hii ilitujumuisha watoto wote wa Fatuma yaani marehemu mama akiwepo kaka yetu mkubwa Hassan, mimi, mdogo wangu aliyenifuata Obuya ambaye tulimpitia Mwanza ndipo anapoishi na mdogo wetu wa mwisho Tina. Pia tulikua na ndugu yetu Flora pamoja na Hamis ambaye alitusaidia sana kwenye maswala ya gari pamoja na udereva, ambapo walikua wanasaidiana na Hassan.
Tulianza safari yetu kutokea Dar saa kumi na mbili asubuhi na tuliwasili Moro mida ya saa 3 asubuhi hivi. Ila tulichelewa kutoka Moro kuelekea Dodoma kwa sababu ya tatizo dogo la gari ambapo ilituweka mpaka mchana ndipo tulianza safari yetu ya kuelekea Dodoma. Tuliwasili Dodoma kwenye mida ya saa tisa jioni hivi baada ya kujisaidia na kupata lunch tulianza safari yetu ya kuelekea Singida. Tuliwasili Singida kwenye mida ya saa kumi na mbili jioni hivi hapa hatukukaa kabisa baada ya kucheki gari na kujisaidia tuliendelea na safari yetu ya Shinyanga. Tuliwasili Shinyanga usiku kwenye mida ya saa nne hivi pia hatukupoteza muda baada ya kucheki gari na kujaza mafuta tulianza safari yetu ya Mwanza, tuliingia kwenye jiji hili kwenye mida ya saa saba usiku tukiwa hoi, choka kabisa na kuamua kulala hapa.
Asubuhi ya saa kumi na mbili tulianza safari yetu ya kuelekea Musoma ambapo tulipitiliza moja kwa moja kuelekea kijijini bila kuingia Musoma mjini. Tuliwasili kijijini kwenye mida ya saa sita hivi na kufanya shughuli iliyotupeleka na kumaliza kwenye saa kumi na mbili jioni na kuanza safari yetu ya kurudi Mwanza, tuliingia Mwanza kwenye saa nne usiku hivi baada ya kutafuta msosi na kula maana tulikua na njaa sana toka tule asubuhi ya siku hiyo hatukula chochote tulielekea hotelini na kulala. Kesho yake asubuhi tulianza safari yetu ila kabla ya kutoka mjini gari lilileta matatizo kidogo ikabidi tulipeleke garage, ilituchukua mpaka mida ya mchana hivi kabla ya kuanza safari yetu ya kuelekea Shinyanga.
Tulianza safari yetu ya kuelekea Dar kupitia Shinyanga, Tabora lakini si mjini, Singida, Dodoma, Moro then Dar. Safari hii tuliamua kulala Dodoma ambapo tulifika hapa kwenye saa mbili au tatu usiku hivi. Tulipata nafasi kwenye Veta hotel ambayo kwa ujumla ilikua nzuri. Kesho yake asubuhi tulielekea kwenye makaburi ya Kizota kwenda kutizama kaburi la mama ambapo alizikwa karibu miaka 21 iliyopita. Baada ya hapo tulipata breakfast na kuanza safari yetu ya kuelekea Dar mnamo karibu saa tano hivi.
Tuliwasili Dar kwenye mida ya saa kumi jioni hivi ila kutokana na foleni ilitufanya kuwasili home kwenye saa kumi na moja jioni. Kwa kweli safari hii ilikua ya mafanikio makubwa, ilikua ni adventure nzuri sana ambapo wote tuliokuwa kwenye msafara huu tunakubaliana nalo sote tulifurahi sana. Nina plan ya kurudia tena hii safari in the future ila this time nataka nisiwe na haraka ili nipate muda wa kulala kwenye mikoa yoyote hii ili nipata muda mzuri wa kuitembelea sio kama hii safari ambapo tuliingia na kupita tu. What an adventure, I love it!
Safari hii ilikua ya mafanikio sana ambayo ilinipeleka mpaka kijijini Musoma. Nilikaa Dar kwa kipindi kifupi tu ila nilifurahi sana hasa kwa kupokelewa vizuri na wifi na kaka yangu, asanteni sana guys! Pia kitu kikubwa ambacho kilinifurahisha kuliko ni kuweza kufanikisha kilichonileta na pia kukutana na watoto wate wa Fatuma, I hope mama huko aliko alismile kwa furaha. Ni muda mrefu sana tangu sote tuwe pamoja karibu miaka 15 hivi na kuweza kufanikisha kitu muhimu kwetu sote. Kitu kingine ambacho this time nilienjoy sana ni misosi wifi yangu ni mtaalam kwa mambo haya basi si kupika, wacha tule, I wonder why niliongeza more than 3kg kwa chini ya siku 10 tu. Kwa ujumla this trip ni ya furaha kubwa..
Safari hii niliamua kwenda kupumzika kidogo peke yangu. Nilipata nafasi nzuri ya kukaa na mdogo wangu this time pia nilipata nafasi ya kumpeleka mdogo wangu wa mwisho kwenda kuangalia kaburi la mama huko Dodoma, kitu ambacho najivunia sana maana baada ya kufika na kuliona roho yangu ilisuhuzika mno nadhani huko aliko anasmile.
Malaika alifurahia sana Tanzania maana this time alikua amekua kidogo anaelewa karibu kila kitu. Neno alilochukua sana ni Jambo, basi yeye kila mtu mweusi anamuita from Jambo maana anamuita mama yake ametokea Jambo eti ndio Tanzania, watoto bwana wanachekesha sana, basi akiitamka hiyo jambo yake sasa inaleta raha kweli.